Hapa kweli kuna mapenzi/ndoa?!

Hapa kweli kuna mapenzi/ndoa?!

Kaka pole ila mm ni mwanamke nakushauri huyo mwanamke atakusumbua sana , huyo analake jambo ,atakuwa kajazwa maneno na ndugu zake !! ...

Hana msimamo hajui nini maana ya kukwama hata kama unamoenda ujue hilo sio fungu lako sio kila uhusiano huwa unaishia kwenye ndoa



Sent using Jamii Forums mobile app
Huu ujumbe umenigusa sana, nashukuru mno dada angu kwa kushare nami juu ya hili, ubarikiwe sana!
 
Habari wanajamvi! Naomba niende moja kwa moja kwenye mada ili niweze pata ushauri toka kwenu.
Nimefahamiana na huyu binti tangu mwaka 2014, wakati huo akiwa bado ni mwanachuo na mimi nikiwa muajiriwa (kazini) tayari. Nilimpenda sana kiasi ya kuweza kupunguza idadi ya mabinti niliokuwa na urafiki nao wa kimapenzi kwa sababu tu huyu binti ndie alieuaminisha moyo wangu kuwa ndio "the one". Kwa kuwa nina kipato, hakika hakuwahi kukosa hizi huduma za mwanaume kwa mpenzi wake. Na hakika katika urafiki wetu wote amekuwa/alikuwa kweli ni binti sahihi kwangu!
Nia yangu ya dhati ya kumuoa aliifahamu kadiri siku zilivyokuwa zinasonga na ombi lake kwangu lilikuwa nimpe muda amalize chuo ndipo taratibu zingine zifuate.
Hakika mpaka naandika uzi huu ni kwamba siuelewi mwenendo wa mwenzangu.
Mwaka jana mwezi wa 06 niliweza kwenda kwao na kuchumbia rasmi na ilipofika mwezi wa 11 nikapeleka mahari kama ambavyo familia zote mbili zilikubaliana na ka-engagement party kalifanyika.
"November" hiyo hiyo familia yangu ikatangaza tarehe ya harusi kuwa ingekuwa ni mwezi wa tano 2020.
Kutokana na mambo makubwa mawili ya kifamilia ya upande wangu yanayonikabili na mimi ndio nikiwa "provider" wa yote hayo, sikuwa na budi ya kufanya kikao cha dharura na familia yangu mwanzoni mwa mwezi December mwaka jana, nadhima kuu ikiwa ni ku-review ila tarehe ya harusi ambayo tuliisema kule ukweni mwanzoni mwa mwezi wa 11 mwaka jana, 2019.
Familia yangu ilinielewa na kufikia maamuzi ya kuwajuza wakwe wetu kwa kuwaeleza kiundani zaidi, na kuwapa taarifa kuwa tutasogeza harusi kutoka mwezi wa 5,2020 uliopangwa awali na sasa harusi itakuwa ni mwezi wa 08,2020.
Sasa cha kushangaza ni kwamba nikashangaa ghafla mwenzangu akaanza kuninunia bila sababu ila baada ya kuongea nae kwa kirefu akanieleza sababu kuwa hana uhakika na mimi kama kweli nitamuoa na kwamba nimemdhalilisha kwao kuwa ataonekana ana mume mtarajiwa asiye na mipango na kwanini tulishatangaza mwezi wa ndoa ilhali tulikuwa tunajua tutakuja kuibadili (hapa ndio niliishiwa nguvu maana nafahamu matatizo huwa hayaji kwa taarifa).
Na hivi niandikapo uzi huu wanajamvi, ni kwamba tangu mwezi wa 12 katikati ya mwaka jana na mpaka leo hii, mwezi huu wa 2,2020, tumewasiliana kwenye simu mara mbili tu na ni kwa msg na ambazo wala hazihusu kwanini yeye amekuwa hajibu msg zangu na wala haihusu yeye kunijibu kuwa kwanini amekuwa hapokei simu zangu!
Wanajukwaa, naombeni ushauri wenu katika hili, nini nifanye? Pana mapenzi tena hapa? Pana ndoa kweli hapa?
Mkuu kabla ya wakwe kuambiwa, ulimuelewesha kuwa italazimu kureview tarehe ya harusi?
Au kwa lugha nyingine ni wakati gani yeye alijua hayo maamuzi ya kureview tarehe?
 
Mkuu kabla ya wakwe kuambiwa, ulimuelewesha kuwa italazimu kureview tarehe ya harusi?
Au kwa lugha nyingine ni wakati gani yeye alijua hayo maamuzi ya kureview tarehe?
Kabla ya wakwe kupewa taarifa, nilimtaarifu huyu mwenzangu na kumueleza sababu, ofcourse ilikuwa ni lazima mimi nimweleze yeye kama mpenzi wangu, taarifa kwenda kwa wakwe halikuwa ni jukumu langu, hilo lilibaki kuwa ni jukumu la mshenga!
Nilipomjuza tu, response yake ikawa "kwanini sasa mlitaja tarehe ya harusi huku mkijua mtakuja kuibadili............"
Kwenye uzi wangu wa msingi, nililigusia hili!
 
Duuuh ngoja tuitazame kwa upande mwingine! Labda anakupa pressure kutest how much you need her, unajua mapenzi ya muda mrefu kama yenu mnakuwa mmeshakutana na changamoto nyingi saaana, ups and downs, wakati mwingine mpaka upendo kupoa(au kuhisi umepoa) kwa sisi wadada mara kadhaa huwa tunadhani sasa huyu mtu kwa vile kashanizoea saanaa ananichukulia poa, au kanichoka ndio maana hanipi priority fulani , mimi nikushauri kabla ukate tamaa for good( kumbuka umesema ni bint aliyetimiza vigezo vyako) kwa mara ya mwisho mkalishe chini mwache ajieleze vizuri sababu zake don’t pressure her during this, wewe wamfahamu vyema majibu yake kama yatakuridhisha you must try to work on it together
Mithali 13:12
Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua.
Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.

Kabla ya wakwe kupewa taarifa, nilimtaarifu huyu mwenzangu na kumueleza sababu, ofcourse ilikuwa ni lazima mimi nimweleze yeye kama mpenzi wangu, taarifa kwenda kwa wakwe halikuwa ni jukumu langu, hilo lilibaki kuwa ni jukumu la mshenga!
Nilipomjuza tu, response yake ikawa "kwanini sasa mlitaja tarehe ya harusi huku mkijua mtakuja kuibadili............"
Kwenye uzi wangu wa msingi, nililigusia hili!
 
Kabla ya wakwe kupewa taarifa, nilimtaarifu huyu mwenzangu na kumueleza sababu, ofcourse ilikuwa ni lazima mimi nimweleze yeye kama mpenzi wangu, taarifa kwenda kwa wakwe halikuwa ni jukumu langu, hilo lilibaki kuwa ni jukumu la mshenga!
Nilipomjuza tu, response yake ikawa "kwanini sasa mlitaja tarehe ya harusi huku mkijua mtakuja kuibadili............"
Kwenye uzi wangu wa msingi, nililigusia hili!
Mkuu pole kwa hizo changamoto, mtu mwenye majibu sahihi ya swali lako atabakia kuwa wewe mwenyewe.
Umedumu kwenye mahusiano zaidi ya miaka mitano, kuna kitu kiliwawezesha kukaa kwa muda wote huu.
Pia kumbuka kuwa kwa wadada, kuna muda ambao pressure ya kuwa ndani ya ndoa inakua kubwa zaidi. Kwa maelezo yako ni wazi kuwa huyo atakua kati ya 25-29. Na saa nyingine pressure inaweza kumfanya mtu afanye au aseme kitu ambacho sio sahihi kwa wakati.
Angali ni rahisi kwa familia yako kuelewa sababu yako ila ujue kwa familia ya mwenzio sio rahisi kihivyo kukuelewa hata kama wamesema wameelewa. Na ukumbuke huyo binti anaishi na ndugu zake na sio ndugu zako hivyo katika siku kuna uwezekano mawazo anayopokea kuhusiana na uamuzi huo mengi yakawa hasi.
Mawasiliano ni kitu muhimu kama utashindwa kuingia kichwani mwake na kumfanya aelewe mawazo yako. Ujue kabisa yeye sio mtu sahihi kwako na wewe sio mtu sahihi kwake
 
Ukimjali msichana kwa kila kitu alafu ukampa uhuru ukawa haumbani bani, anaamua kila anachojisikia yeye akiamini huwezi pinga maamuzi yake na huku ilihali wewe unaona jambo unalofanya lina manufaa kwa wote wawili badae, pigania penzi lako huenda shetani kamuingia hivo wewe usimuache nenda kwao siku ukiwa free waelezee wazee wake ukweli mpaka mwez wa6 mwaka2020 utaona uelekeo sahihi wa huyo mwenza wako then utanipa mrejesho.
NOTE:Mwanaume hazeeki hadi anaingia kaburini...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuh ngoja tuitazame kwa upande mwingine! Labda anakupa pressure kutest how much you need her, unajua mapenzi ya muda mrefu kama yenu mnakuwa mmeshakutana na changamoto nyingi saaana, ups and downs, wakati mwingine mpaka upendo kupoa(au kuhisi umepoa) kwa sisi wadada mara kadhaa huwa tunadhani sasa huyu mtu kwa vile kashanizoea saanaa ananichukulia poa, au kanichoka ndio maana hanipi priority fulani , mimi nikushauri kabla ukase tamaa for good( kumbuka umesema ni bint aliyetimiza vyako) kwa mara ya mwisho mkalishe chini mwache ajieleze vizuri sababu zake don’t pressure her during this, wewe wamfahamu vyema majibu yake kama yatakuridhisha you must try to work on it together
Mithali 13:12
Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua.
Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.
Hii imenipa comfort sana, shukrani mno!
 
Hii imenipa comfort sana, shukrani mno!
Yeah, sisi wanawake huwa tunafanya maamuzi kulingana na hisia zaidi, so makosa yetu mengi yanatokana na kutawaliwa zaidi na hisia( hisia zinatuchukua tunasahau kabisa vitu logic) na nyie wanaume ni mko kilogic zaidi kuliko kubebwa tu na hisia. So huwa tunakosea wakati wa kutoa ushauri tunasahau kabisa utofauti wetu wa kufikiri, kureason mambo na kuyafanyia maamuzi.
 
Back
Top Bottom