bahati mbaya
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 578
- 193
- Thread starter
- #21
kweli wewe una bahati mbaya!pole sana.swali langu uliwezaje kumvumilia miaka yote 11? nini kimekufanya saa hizi uone ndo havumiliki?je kazidisha vituko au kuna kilichokuwa kinakufanya umvumilie kimepungua? na miaka yote hiyo umeshindwa kumtafutia shughuli ya kufanya ?!
Nilijitahidi sana kuwa karibu naye ili walau tuwe na shughuli ya pamoja lakini mwenzangu kwanza siyo muwazi kwa pesa yake. Siyo kwamba hana kabisa, amekuwa kikopa kwenye taasisi za fedha mbalimbali lakini hata shughuli zake anazofanya hazikui, ukitaka maisha yawe machungu hoji pale unapojua kuwa amepata mkopo mtagombana kila siku. Ikiisha ndiyo anakuwa mpole. Na mwaka huu nilikataa kumdhamini mkopo ndiyo mambo yamekuwa magumu kabisa maana anadai kuwa kama sikumdhamini natengemea atachangia nini?
Wakati alipokuwa nachukua mkopo hata mlichokubaliana kufanya hakifanyiki anaishia kusema kuwa analipa madeni ambayo mimi siyajuhi wala familia haihusiki nayo.
Ndiyo maana mgogolo umekuwa mkubwa zaidi kwa kipindi hiki.