Haoni umuhimu wa mawasiliano

Ambassador

JF-Expert Member
Jun 2, 2008
933
75
Ni mke mwema aliyetulia na kutekeleza vema majukumu yake ya ndoa. Tatizo lake anaposafiri kwenda nyumbani hawezi kupiga simu wala kutuma message mpaka atafutwe. Licha ya kulalamikiwa mara kadhaa ameshindwa kubadilika na kuna wakati alisema "mimi nakuwa na uhakika uko salalama". Yuko nyumbani kwa sasa na jana asubuhi alipata taarifa za mume kuugua lakini mpaka sasa hivi hajapiga simu kuulizia hali ya mume inaendeleaje. Nini kifanyike?
 
Waliopo upande wa pili wamtafute yeye!Kama tayari mume amejua weakness ya mkewe aanze kwa kumtafuta yeye tena bila kulalamika!In time atazoea nae ataanza!Yani amzoeshe mwishowe atashindwa kujizuia!
 
Kweli huyu Kiboko
Yaani hana hata hofu ya mmewe kama yuko salama ,anaendeleaje na mengineyo
Kweli huyu nashindwa kumuelewa ana matatizo gani
 
Mh... Inawezekana yupo kwa mwanaume kwa sababu alishaapa kwa hiyo ndoa, lakini hamfeel mumewe from the heart...

Inawezekana mumewe msumbufu na mkorofi awapo naye, hivyo akiwa mbali anajisikia nafuu kuepeka usumbufu wake...
 
Mh... Inawezekana yupo kwa mwanaume kwa sababu alishaapa kwa hiyo ndoa, lakini hamfeel mumewe from the heart...

Inawezekana mumewe msumbufu na mkorofi awapo naye, hivyo akiwa mbali anajisikia nafuu kuepeka usumbufu wake...

hata mie nahisi ni hivyo...
 
watu kam hao wapo, wala sio kwamba hampendi mme wake bali amezaliwa na hulika ya hivyo, kwani anataka kila kitu aanzwe au aelezwe.
Na kwake anajiona yupo safi kabisa bila shaka lolote, hivyo anachotakiwa ni kumuelewa na kumvumilia.
wanawake wa hivyo huwa ni bora liende kwani wanajali sana mambo yao wenyewe
 
<H2 class=posttitle>The Following User Says Thank You to Mallaba For This Useful Post:

Elia (Today)​

</H2>
 
kama ni mke mwema aliyetulia....basi hivyo vingine vipotezee......personally sijawahi kukutana na msichana halafu kwenye kuelezea yukoje nikaweka maneno "mwema" na "aliyetulia".....kwa hiyo kama we umempata mng'ang'anie.
 
Kuna mambo mengi.

1. Mvivu wa kutumia simu kama .......... anaweza akawa sebuleni simu iko chumbani siku nzima wala hajali
2. Hajui kutumia simu kama kuandika msg kama ..........
3. Ianmkera au ilishawahi muumiza siku moja
Nk
 
Mpigie simu mara kwa mara na kwa muda mrefu, baadaye taratibu ataingiza mawasiliano kwenye ratiba yake. Inawezekana hajazoea tu kuwasiliana mara kwa mara. Kama ni mwema na ametulia we komaa tu kasoro zingine ni ndogo ndogo sana.
 
Binafsi siyo mpenzi sana wa kupiga piga simu au kuandika meseji, hivyo huyo dada simshangai..
Huwa nahisi kama uvivu flani vile..............
Ila angalau akisafiri awe anatoa taarifa kuwa amefika salama, baada ya hapo sioni ulazima wa kupiga piga simu...
 
Duh pole kaka sababu nahisi unajihisi kama vile hakujali wala hakukumbuki, binafsi naona ni mwanamke wa kipekee maana wanawake wengi wakiwa mbali na wapenzi wao au waume huwa wanapenda mawasiliano sana. duh mimi napenda hata akienda chooni aniambie kama inawezekana. hahahahahaha!
 
Hapana huyu mwanamke ni tatizo, yaani hata mme akiumwa hajui hata kumjulia hali, hata enzi zile hamna simu haikuwa hivi, duh!

Hata mimi si mpenzi sana wa simu lakini nikisafiri angalau kila baada ya siku mbili au tatu naulizia hali ya familia, na mke nae huwa ananipigia kama nimempa namba ya simu. Aisee duniani watu tofauti tofauti na wengine ni mshangao kwa kweli!!!
 
Back
Top Bottom