Hannah Mbajo: Wastaafu wengi wanakwama kwenye biashara sababu hawana uzoefu

Nyakijooga

Senior Member
Dec 9, 2018
123
202
Imeelezwa kuwa moja ya changamoto ambayo inawakumba Wastaafu wengi Nchini ni kukwama kwenye biashara sababu ya kukosa uzoefu.

Hayo yameelezwa na Meneja Masoko wa Benki ya Mwalimu (MCB), Hannah Mbajo wakati wa uzinduzi wa Kapu la MwalimuSanta, ambapo ameeleza kuwa kwa kutambua changamoto hiyo MCB imebuni njia itakayotumika kuwa suluhu la mafao ya kustaafu ili kuwasaidia wanaostaafu.

Amesema taasisi hiyo ni sehemu salama kwa Wastaafu kuwekeza ambao wanaweza kuchukua fedha zao wakati wowote huku wakijihakikishia usalama wa mali zao kwa kupatiwa bima.

IMG-20231206-WA0162.jpg
Ameongeza kuwa Kapu la MwalimuSanta linamruhusu mstaafu aliyewekeza fedha zake MCB kukopa Asilimia 80 ya fedha alizowekeza kupitia mkopo wa 'Mlinde Mstaafu'.

Mbajo alisema Kapu la MwalimuSanta limebeba bidhaa muhimu kwa wastaafu watarajiwa na waliostaafu tayari ambao watawekeza fedha zao kwa faida ya asilimia 12 kwa mwaka na kupata bila malipo bima ya nyumba na samani za ndani.

“Watuamini tuwawekee fedha hizo wakiwa na uhakika wa kupata faida kila mwisho wa mwezi au mwisho wa mwaka,” amesema Mbajo na kuongeza kuwa MCB imezindua Kampeni ya Kapu la MwalimuSanta ili kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka na kugawa zawadi mbalimbali kwa wateja wake.

"...Kapu la MwalimuSanta halikuishia hapo likaendelea kwa kuwalipia wastaafu bima ya nyumba kama anayo ama samani zote za ndani.

"Sote tunaona hivi sasa majanga mbalimbali yameongezeka kuna moto, mafuriko kama kule Manyara na hii ni kwasababu ya mabadiliko ya tabianchi hivyo tunamkinga mstaafu wetu na majanga ya aina yoyote," amesema Mbajo.

Akizungumzia bidhaa nyingine iliyopo kwenye Kapu la MwalimuSanta, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kidigitali cha MCB, Elilumba Kinyau alisema kapu hilo pia linagawa zawadi hadi sh. 50,000 kwa wateja wake watakaofanya muamala wa kiwango chochote bila kadi kupitia kwa wakala.

"Hii ni zawadi kwa wateja wetu watano kila wiki kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka mteja akitoa hela bila kadi kwa wakala wa MCB popote alipo atajipatia fedha taslim hadi sh 50,000 hapohapo," alisema Kinyau na kuongeza kuwa MCB ina mawakala zaidi ya 500 nchi nzima na huduma za benki kiganjani.

IMG_20231207_065819_665.jpg
 
Tatizo lingine na hawa wazee huwa wanakuwa wabishi sana wakishika hizo hela za mafao huwa hawasikilizi watu sahihi wanajifanya kuleta ujuaji na kwenda kwa watu wanaotaka wao wawashauri mwishowe wanaingia kwenye biashara ambazo zinawafujisha pesa na wanaishia firisika.

Halafu wakisha filisika wanakuja mikono nyuma wameufyata kwa watoto wao na familia zao, ndio maana unakuta watoto wanawanyali wazazi wao baada ya kustaafu sababu ya mambo kama haya.

Mzazi unatakiwa ukipata mafao kaa na watoto wako mtazame namna ya kuunda uchumi mpya na tena usisubirie kustaafu, mapema sana anza wajengea watoto wako misingi na akili za kiuwekezaji ili ukikaribia ule umri wa kustaafu tayari kunakuwa na functional base ya uchumi wako mpya wa maisha baada ya kustaafu.

Ila hawa wazazi wetu hawa, umri wa kustaafu alishashika tu zile hela, basi utashangaa anakuwa busy na watu anaowaamini yeye, mara unashangaa amenunua Coster used yenye majanga yake hii hapa kisa madalali wamemjaza upepo huko.

Au utasikia kanunua pagala ameanza kulijenga, au kanunua shamba na "Toyota pick up Hilux" ya kuendea shamba na wamempiga bei.

Wakati kumbe angetuliza kichwa kuna biashara ambazo hazihitaji mtaji wa million ila zina mzunguko mzuri sana wa pesa na kukuza mtaji ni rahisi.

Ukimwambia anakuona mtoto unaleta ujuaji kama sio kukupuuza basi atakuwa mkali na hela zake.

Tunawasaidiaje sasa
 
Huyu mrembo alikuwaga Mbongo flavor Kuna wimbo walimshirikisha Nature kama sio Dully nafikiri.
 
Back
Top Bottom