Hamna kitu nachukia kama kumpa Fundi kazi halafu anawaachia vijana wake yeye akauwa anarandaranda tu

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,554
Mafundi wengi wanakera sana! Hasa mafundi magari na mafundi ujenzi. Unaelewana nae vzr kabisa lakini unakuta anawaachia vijana wake kazi.Yeye anakuwa kama Consultant anawasimamia tu.

Unakuta fundi magari yeye anafanya kazi kwa vidole tu yaani! Halafu manyoka ndo wanaumia mbaya kabisa.

Mafundi wakuu acheni hiyo tabia mkipewa kazi msijifanye nyie ni Consultants.
 
Umeelewa ulichoandika kweli
?
Hao madogo watakula wapi wasipofungua nati na kuchanganya cement ...
Huujui ufundi kaa kimya
Sio kila kitu kaundika hapa.
Mbona...huko makwenu...mnawatumikisha mabek 3 na msilee mtoto wenyewe...na mkambeba kwenda naye kazi?
Kila mtu anaridhiki yake
Bila wezi na waandamanaji...
Walinzi tutakulaje...
Mzunguko wa ridhiki huo

Cc.
Mshana
Bujibuji
Na wengine
 
Kama kaz inafanyika vizur bila kuharibika na kuchelewesha haina shida acha vijana wapige kaz
 
Bora awaachie lkn kazi ifanyike.

Kuliko awaachie afu waharibu kazi.
 
mkuu haya yalisanikumba na mimi nilichokifanya nikavunja mkataba na fundi then nikaajiri wale vijana.issue ya pili niliita mafundi kwa wakati tofauti wanifanyie kazi the wote wakakataa then akaja mmoja akasema nipe jiyo kazi kwa hela niliotaka mimi mwishowe wale mafundi wengine wakaja kuifanya ile kazi kama vibarua
 
na kwenye magari ndio mbaya sana watafungua kitu kina bolt 5 wakati wakirudisha hawafungi bolt tano walizozitoa watafunga 3 au 4 kama usipokuwa muangalifu imekula kwako
 
kuna kitu kinaitwa delegation, kama anaiamini timu yake wewe ni nani wa kumpangia, bora hata huyo ambaye anasimamia na mwingine humuoni kabisa, yan fund mtaalamu ashuke chini ya gari kufungua nati?
 
na kwenye magari ndio mbaya sana watafungua kitu kina bolt 5 wakati wakirudisha hawafungi bolt tano walizozitoa watafunga 3 au 4 kama usipokuwa muangalifu imekula kwako
Kuna balaa kagfungua bolt 5 halafu wakati wa kurudisha kafunga zote 5 halafu kuna 2 zimebaki hazina pakufungwa. Apo fundi anahangaika kujua ni wapi zimetoka, mwisho wa siku unakuta kuna sehemu hakujafungwa...
 
Na hilo jambo husababisha gharama za ufundi kuongezeka maradufu. Yaani fundi hugeuka kuwa mkandarasi au mshauri wa utaalamu. Sasa jiulize vijana wake anawalipa shilingi ngapi na yeye anabaki na ngapi? Mafundi wenye tabia hizo nilishaacha kuwatumia kitambo sana.
 
Shukuru akiwepo hata ye mwenyewe kusimamia kwa vidole, huwa wanaacha vijana na wao wanaenda kwenye tenda nyingine mpya kujionyesha kabla na huko hawajaacha vijana kuhamia tena kwenye tenda mpya
 
.....Jamaa ashakamta kazi zaidi ya moja!, hapo anazungukia vijana wake tu.....Uwezekano wa kazi kuwa chini ya kiwango ni mkubwa.
 
ni mipangilio ya kazi tu,uwezi kuwa injinia alafu usimamie kila kitu mwenywe,ndio maana kuna matabaka kwenye kazi.mjifunze na kuelewa sio mnalalama bila sababu za msingi
 
Yaan inakera saa nyingine vijana hawajui vizuri akitoka tu unakuta wamesharibu kitu then wanakuambia hiki kilikuwa kibovu
 
Mafundi wengi wanakera sana! Hasa mafundi magari na mafundi ujenzi. Unaelewana nae vzr kabisa lakini unakuta anawaachia vijana wake kazi.Yeye anakuwa kama Consultant anawasimamia tu.

Unakuta fundi magari yeye anafanya kazi kwa vidole tu yaani! Halafu manyoka ndo wanaumia mbaya kabisa.

Mafundi wakuu acheni hiyo tabia mkipewa kazi msijifanye nyie ni Consultants.
Bila kufanya hivyo hao vijana hawawezi kuwa mafundi na atakufa na maarifa yake.na hao vijana wakiwa mafundi nao watawaachia vijana. And that what's called EDUCATION.

Umepeleka kazi,mmekubaliana,umepewa muda,kazi itafanywa na ofisi sio mtu.Na huo ndio utaratibu.
 
Back
Top Bottom