Hamis Taletale: Neno Rais litumike kwa Rais wa nchi na si wengine kama TFF


Nchi yetu ina Rais mmoja tu Samia Suluhu, ningeomba hizi Rais wa shirikisho au TFF zitoke, wawe na vyeo vyao. Wanapunguza heshima ya neno Rais, unakuta mtu ana vumbi, Rais hawezi kuwa na kiatu kina vumbi tunatakiwa tuheshimu, ndiyo maana mimi nilijiita Babu"- Babu Tale.

======

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Hamisi Taletale amependekeza neno Rais litumike kumtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Akiwa Bungeni amesema neno hilo kutumika kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) na wengineo linaishushia heshima

Ameshauri watu wapewe majina mengine ya Vyeo vyao akisema haiwezekani Rais akawa na viatu vyenye vumbi, ndio sababu yeye aliamua kujiita 'Babu Tale'
Jamani Morogoro tumeishiwa. Hiyo ndiyo kero yenu kubwa? Mbuge wetu kasimama eti hana jingine la kuwasemea watu wake. Kura zetu zimeharibika jamani.
 
Pia Jina Babu litumike kwa Watu wenye Busara tu na wazee si kila mtu.
 
Waliojukuu tu ndio wanafaa kuitwa 'Babu'. Hawezi mtu mpuuzi mpuuzi akaitwa babu.
Yes uko sahihi sana,yaani kwanza kabla hajaanza kukosoa viongozi wa juu wa baadhi ya taasisi kuitwa Rais,angeanza na kujikosoa yeye kwa kujipa jina la babu!.Yaani msela mavi kama yeye wa Manzese TipTop huo ubabu anaupataje?,haoni anawavunjia heshima mababu zetu?.Yaani huyu ni kilaza kabisa na hakua na sifa za kwenda bungeni.
 
Back
Top Bottom