- Thread starter
- #21
​so what??????????
Majibu ya swali lako haya hapa ''''
Mhe. Rais Jakaya Kikwete ni mtu makini sana. Leo nimeamini nabii hakubaliki kwao, ninaamini ata. Amenifanya nimejisikia proud sana leo kwenye mikutano mitatu niliyoshiriki pamoja naye, yeye akiwa panelist na marais na watu wengine mashuhuri duniani. Kauli yake ya kwanza ni namna alivyosema kuwa tunawaalika wawekezaji kwenye kilimo siyo wachukue ardhi ya wazawa bali wawe chachu ya kukuza uzalishaji wa wazawa wanaowazunguka through outgrower schemes. Alisisitiza hili kwa nguvu sana akisema 'not with me, my grandparents and parents will punish me if I do allow land grabbing from small-holder farmers because I am from the same history and lifestyle...even if they are dead still I fear them'...hadhira ilishangilia kwa maneno haya, na wengine walimpa heshima ya standing ovation. Aliyasema maneno haya mbele ya mkutano wa kilimo na lishe akiwa kwenye panel na Waziri Mkuu Mstaafu wa Japan, Mhe. Yoshiro Mori. Pia, Mhe. Rais Kikwete alifunika hadhira kwa namna alivyoelezea suluhisho la tatizo la ajira kwa vijana pamoja na mikakati iliyopo ya kuongeza ajira na kukuza uchumi. Nilipanga kuchangia lakini baada ya hotuba nzuri ya Rais wetu, niliamua kunyamaza, maana alinifilisi hoja zangu zote, japokuwa kabla ya hapo niliamini nina mchango mzito kwenye jambo ukizingatia nimelifanyia utafiti wa kina na kwa muda mrefu na ni jambo ambali ninalitafutia suluhu kwa vitendo - c.f. Hoja yangu binafsi kwenye Bunge la Februari''
mwisho wa kunukuu source- facebook wall ya kigwangala