Hamisi Kigwangalla
Nipo hapa jijini Yokohama, Japan. Nipo kwenye msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete kwenye mkutano mkubwa na maarufu duniani kuhusu Afrika unaojulikana kama TICAD V (Tokyo International Conference on African development). Kwa dakika chache jana Mhe. Rais Jakaya Kikwete aliniachia kiti chake, nikaa kwenye round table na marais wengine zaidi ya 50 wa nchi za Afrika! Can you imagine that? Kulia kwangu alikuwa Mhe. Michael Satta (Rais wa Zambia - a very charming fella!) na kushoto kwangu alikaa Mhe. Yoweri Museveni (Rais wa Uganda).
Leo tena nimepata fursa ya kuingia kwenye kikao kimoja na Mhe. Rais Jakaya Kikwete na humo tulikuwa kwenye bilateral meeting na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Mhe. Ban-Ki Moon. Pia nimepata fursa ya kujadili mambo kwenye vikao na Marais Jacob Zuma (South Africa), Ali Bongo Ondimba (Gabone); Rais wa World Bank, Dr. Jim Yong Kim; Rais wa Benki ya Afrika, Dr. Donald Kaberuka; Rais wa JICA, Dr. Akihiko Tanaka etc. Ziara hii imenifundisha mambo mengi ambayo sintoyasahau katika maisha yangu.
Nimepata pia fursa ya kumuelewa vizuri zaidi Rais wetu na namna anavyoielewa dunia, kukubalika kwake kimataifa, nafasi yake kati ya viongozi mashuhuri duniani na nafasi yetu kama Taifa katika dunia. Hongera Rais wetu Jakaya Kikwete, umenifanya nijisikie 'so proud to have you as our president, and to be a Tanzanian in a global world!' Ziara hii kwenye mkutano huu mkubwa wa kimataifa hapa Japan imenipanua zaidi uelewa wangu kuhusiana na diplomasia ya kimataifa na namna changamoto zinazotukabili sote kama raia wamoja wa dunia moja na namna zinavyopatiwa ufumbuzi wa pamoja, kwa namna ya umoja wetu kama binadamu.
MWISHO WA KUNUKUU. source ukurasa wa facebook kwenye wall ya kigwangala
Naona hapo baba ya rizmoko na hiyo suti si ile ya maleberali ya kiarabu?