Hamchoki na mikutano ya waandishi wa habari? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamchoki na mikutano ya waandishi wa habari?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 12, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi watu hawajachoka bado na mikutano ya waandishi wa habari ambayo kila siku huzaa mikutano mingine ya waandishi wa habari ambayo nayo ilitanguliwa na mikutano ya waandishi wa habari? Inaudhi!

  Yaani, utaona jambo limetokea na katika kutokea kwa jambo hilo basi kiongozi anaamua kuita waandishi wa habari na kuwajulisha juu ya jambo hilo (au kutowajulisha kiundani). Akimaliza anaruhusu maswali mawili matatu, anatabasamu, anagonga na meza halafu waandishi hao wanaondoka na kwenda kuandika.

  "Waziri ajibu mapigo", "Mheshimwa X,Y aunguruma" n.k n.k

  Siku chache baadaye kiongozi mwingine naye anaitisha mkutano na waandishi wa habari na kuanza kujibu mapigo ya yule mwingine. Wakati anafanya hivyo, yule wa kwanza anaandaa mkutano mwingine wa waandishi wa habari.

  Lengo la hawa wote ni kujaribu kuonesha kuwa wako juu ya mambo yanayowahusu na kuwa hakuna aliyetayari kupikuliwa na mwingine. Katika kufanya hivyo, utaona viongozi wa kisiasa na watendaji wa serikali na hata taasisi mbalimbali wanatembea na namba za simu za waandishi wao rafiki; waandishi ambao hawachelewi kufika kwenye eneo la "tukio" na ku "cover" story.

  Cha kuudhi zaidi ni kuwa katika kufanya hivyo waandishi hao wanahitaji kupatia posho ya kutembea, posho ya kalamu, posho ya kupigwa na jua na wakati mwingine wanatakia kuhakikishiwa kuwa lile gari lililokuwa gereji linatoka kabla ya jumatatu kwa msaada wa mheshimiwa huku mheshimiwa wetu akiahidiwa "stori" nzuri ambayo itaonekana haimpendelei au kumharibia.

  Tukiwa bado tunashangaa kinachoendelea tunasikia kuwa kuna mkutano mwingine wa waandishi wa habari ambapo serikali imeamua kutoa onyo na kukemea "vikali" tabia "fulani".

  Sasa nimegundua kuwa mikutano ya waandishi wa habari ni siri mojawapo ya kuficha kinachoendelea. Watawala wetu wameshagundua kuwa kwa kadiri ya kwamba wanazungumza na waandishi wa habari na kutoa maelezo marufu (haijali kama wanachokielezea kina umakini) basi wananchi watakuwa wanajua!!

  Ndiposa, nimefikia hitimisho kuwa watawala wetu wakiwa wanalala kitanda kimoja na kujifunika mashuka ya ulaghai wamekula njama ya kutupatia taarifa za kutuliza hasira, kiu, kero na kisirani ambao wao wenyewe wametujengea.

  Wanajua Watanzania wanaridhika kwa taarifa mbalimbali. Ndipo utaona kwenye magazeti na kwenye matangazo mbalimbali taarifa za serikali na wizara mbalimbali zimejazana huku kila kukicha mkutano mpya wa waandishi wa habari umeandaliwa.

  Sasa najiuliza lile swali ambalo nililiuliza kabla ya kutoa ripoti ile ya Meremeta; tunajua ili kiwe nini? Maana kama ni kutaka kujua tu kwa kweli tunajua sana yaani tunajua hata yale ambayo kujua kwake kunatufanya tuwe wahitimu wa kozi ya ujuaji wa ufisadi ambayo darasa lake ni ukumbi wa MAELEZO na wakufunzi wake ni waheshimiwa walioishiwa hoja.

  Tumekuwa ni mabingwa wasio na upinzani katika ujuzi wamadudu ya watendaji wetu na kama wataalamu wa siasa za kejeli tumeng'ang'ania vyeti vyetu. Tunajua Rais alikuwa wapi, akibembea nini na harusi ya mtu gani mashuhuri ilivutia vigogo; tunajua nani ana mimba na nani analala nani! Tumefika mahali tunajua hata vile ambavyo kimsingi ni vitu vya chumbani kwa mtu na mwenzake!

  Tumekuwa ni vigogo wa ujuzi usio na umuhimu - experts in irrelevant knowledge! Lakini ujuzi huu wote umetufanya tufanye nini nao? Je kujua kwetu yanayotokea Benki Kuu, Ikulu, Wizarani, na ujuzi wa malumbano ya vibosile wa siasa zetu umetusaidia nini zaidi ya kulisha udadisi wetu tu na kutufanya tuwe mabingwa wa kuwaeleza wengine ule ujuzi wetu?

  Kwamba tunaweza kusimulia kwa kina ufisadi wa EPA, ufisadi wa Mwananchi Gold, Richmond na mgongano wa maslahi wa kambi za RIchmond kumetufanya tuwe tofauti namna gani zaidi ya tofauti ya kujua zaidi?

  Leo hii watu wanaona madudu yanafanywa kwa jina la serikali yao na badala yake wanaamua kuitisha mikutano ya waandishi wa habari; leo hii waliokuwa vigogo wa nchi hii badala ya kusimama na kutaka hatua zichukuliwe na wao wenyewe kuonesha mfano wa mambo hayo wanabakia kuitisha waandishi wa habari na kutoa kauli nzito huku aliyeshutumiwa naye anakutana na wenzaka akiandaa majibu (bila ya shaka itakuwa mbele ya waandishi wa habari!).

  Well.. ngoja na mimi niitishe mkutano wa waandishi wa habari nilalamikie jinsi waandishi wa habari wanavyopoteza muda wa kukusanyahabari zisizonaumuhimu na kutujuza vitu ambavyo tayari tunavijua lakini wakivuria kama kaseti iliyokwama au santuri iliyogoma kwenye neno moja!

  Tafadhali waandishi wa habari mpo?

  Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
   
 2. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Umeichoka fani yako kungali asubuhi?
   
 3. S

  Shamu JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2009
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Waandishi wa habari, ndiyo Ukweli na Uwazi.
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  MKJJ:
  Pengine huu ni wakati mwingine muafaka wa kuweza kutumia teknologia ya internet kwa upana zaidi. Katika hili wewe binafsi upo mbele sana na umejitahidi vya kutosha kuweka mada zako katika web site zako na zingine zinazovuma na zenye watembeleaji wengi, lengo likiwa ni kufikisha ujumbe pasipo kuitisha mikutano ya waandishi wa habari.

  Tukirudi nyuma vyanzo vingi vya habari hapo nyumbani na hasa kuhusu misimamo binafsi ama ya asasi ama ya vyama ama ya serikali inategemea mikutano hiyo. Na hii inakwenda sambamba na utoaji wa bahasha, soda na lunch.

  Ingekuwa vipi iwapo waandishi wa habari hapo nyumbani wangekuwa wanashinda kwenye web site za Ikulu, asasi ama watu mashuhuri nchini mwao? si wangeweza kupata taarifa na misimamo yako juu ya mambo mbali mbali pasipo kukusanyika Idara ya Maelezo?

  Hata wewe binafsi usingekuwa unapoteza muda mwingi kutuma article zako kwenye magazeti, kwani wangeweza kuzipata kupitia kwenye mwanakijiji.com

  Au vipi kuhusu vyama vya siasa, kweli wanapaswa kuendelea kurumbana kupitia Idara ya Maelezo? Au wanajua kuwa sio waandishi wa habari na wasomaji wa habari ambao wanapitia kwenye website zao?

  Redio, Magazeti na television bado vina nafasi kubwa kuwa vyanzo vya habari nchini kuliko internet, nao habari huzipata kupitia mikutano hiyo!..
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  Dec 12, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kibunango.. nimejaribu sana mwaka huu kuwashawishi wanasiasa mbalimbali (wa upinzani na CCM) kuanzisha tovuti zao wao wenyewe ambapo wangeweza kutumia kutoa taarifa zao mbalimbali. Si unaona Tiger Woods anavyowafanyia; kujitokeza hadharani hajitokezi na hatoi nafasi kwa watu kumbana na badala yake anatoa taarifa tu kupitia kwenye tovuti. Matokeo yake vyombo vya habari vina monitor tovuti yake masaa 24 kuona kama kuna taarifa mpya.

  Kwa nyumbani tatizo ni kuwa taasisi, watu na idara zikianza kuwa na taarifa zao kwenye tovuti zao itaondoa kabisa ile interaction ambayo kimsingi inachochea vyombo vya habari kuwa sehemu ya mfumo wa kifisadi (nililianisha hili katika kuelewa mfumo wa utawala wa kifisadi).

  HIvyo utaona kuwa siyo katika maslahi ya wanasiasa au idara kuwa na sehemu zao wenyewe za taarifa kwani itaondoa nafasi ya ulaji na waandishi wa habari hawatafurahia hiyo kwani itawaondolea iile nafasi ya kukutana na watawala na kujaribu kuwazungusha. Hili unalopendekeza linaweza kusababisha njaa kubwa sana kwa waandishi wetu!
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Dec 12, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,598
  Likes Received: 18,598
  Trophy Points: 280
  Japo mimi si mwandishi wa habari, waandishi nawaona na kazi yao inaonekana.

  Mzee Mwanakijiji, ulitakiwa uwapongeze hao waandishi wetu kazi kwa nzuri ya reporting. Wengi wa waandishi ni mareporter hivyo kazi yao ni kuripoti, hicho ndicho walichofundishwa madarasani kwao, 5Ws and H, Who, What, Where, Where and How. Reporter sio kazi yake kuandika, 'So what' yeye ni kuripoti tuu, wa kuandika so wat and what does it mean, ni kazi ya ma analiysers watakao fanya analysis. Be fair kwa maripota wanafanya kazi nzuri ya reporting.

  Pia hao waitishaji Press Cconference, wanastahili pongezi, at least now people are opening up. Zamani hakukuwepo hata mtu wa
  Kuzungumza. Hizi na kujibishana kupitia press com ni heathy hata kama zinamwagwa pumba, out of pumba, ukipepeta vizuri, unapata chenga.

  Openesss ni heathy for the media, tunahitaji waandishi vicha zaidi
  Wazame zaidi kutafuta kilichofichwa na sio tuu ukasuku wa kulishwa wanacholishwa na kutapikia magazetini kwao na hata sis JF ni watafunaji wazuri tuu wa hizo media imputs.

  Fani ya uandishi Tanzania imevamiwa, ila kuna wachache wazuri wanaofanya kazi nzuri, wanastahili pongezi na kujengewa uwezo wafikie specialization ya kuwa waandishi bingwa kati fani maalum.

  Hongereni mareporters, hongereni watoa habari kazi inaendelea.
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Dec 12, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kamanda nimekuelewa sana! Hili tatizo halipo tu kwa waandishi wa habari tu, hata vyombo vingi vyenye kutengeneza habari hapo nyumbani wapo nyuma sana katika kutumia njia nyingine ya kutoa habari zaidi ya Mikutano.

  Hivi karibuni kulikuwa na mada ya Bembea hapa JF ambapo JK alishambuliwa sana. Kama ni kweli JK alipofika huko aliupdate profile kwenye facebook kwa maneno haya..
   
 8. M

  Mayolela JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2009
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 383
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu CCM damu nae,hoja zake za ovyo ovyo tu.na bendera lake la chama cha mafisadi.
   
Loading...