Hamadi Rashid na Daudi Kafulila, Gongolamboto mwisho wa Lami

Dar es Salaam kuna kituo cha basi huitwa Gongo la Mboto mwisho wa lami. Zamani hapo ndipo lami ya kutoka mjini ilikuwa inaishia na kwa hiyo daladala pia zilikuwa zinaishia hapo. Siku hizi kuna maendeleo zaidi Gombolamboto siyo tena mwisho wa Lami.

Uteuzi wa baraza kivuli la mawaziri wa leo tunaweza kusema ni Gongolamboto kwa akina David Kafulila na Hamad Rashid kwa maana ya kwamba katika safari yao ya kushirikishwa kwenye kambi rasmi ya upinzani hapo ndo mwisho wa lami. Hakuna uwezekano huo kwa sasa, LABDA baadaye, kama hiyo baadaye na wao watakuwemo.

Hawakupata uongozi wa kamati hata moja wala uwaziri kivuli. Lakini walihemshwa na support ya wabunge wa ccm na kusahau kwamba hawawezi kulazimisha uhusiano kwa kutumia kanuni za bunge. Sasa ccm wameshapata walichotaka, yaani kamati ya PAC kuongozwa na mtu wao (Cheyo). Habari imekwisha, Kafulila na Hamad wanauguza maumivu, Chadema wanachekelea na kusonga mbele.

I love politics, who loughs last loughs longer!!
Umepoteza muda wako wote huwo kuandika hii Thread yako Crackpot, wewe pamoja na wenzako kabla ya kuandika ungefanya utafiti hili kujua kanuni za bunge zipo vipi chaguzi zinaendaje, sasa wewe unafyatuka tu kwa mapenzi yako sasa muombe msamaha HAMAD RASHID, Gongo la mboto mwisho wa lami.

Kwani hicho cheo alichopata kinaitwaje tena?
 
Kwa udaku mpo juu,zungumzeni mambo ya maana acheni kujadili umbeya,wanaume wa siku hizi mna mapungufu,umbeya umewazidi na vijiba!!!
 
kwa udaku mpo juu,zungumzeni mambo ya maana acheni kujadili umbeya,wanaume wa siku hizi mna mapungufu,umbeya umewazidi na vijiba!!!

duh!!! Nadhani umekosea thred. Wazo lako ni zuri lakini umechangia thred nyinge. Labda nipe kazi nikutafutie thred uliyo taka kuchangia. HAPA WANAONGEA PURE POLITICS FROM THE GROUND.
 
Kwani kapata cheo? labda
GONGO LA MBOTO MWISHO WA LAMI

Lakini Ritz, kilichojuudhi hapo ni kipi. Kwamba hamadi hakupata uongozi wa kamati au hakupata uwaziri kivuli hata baada ya kujipendekeza sana ccm na kusababisha uchafuzi wa Hali ya hewa bungeni?
 
Back
Top Bottom