Hamadi Rashid na Daudi Kafulila, Gongolamboto mwisho wa Lami

muhosni

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
1,108
152
Dar es Salaam kuna kituo cha basi huitwa Gongo la Mboto mwisho wa lami. Zamani hapo ndipo lami ya kutoka mjini ilikuwa inaishia na kwa hiyo daladala pia zilikuwa zinaishia hapo. Siku hizi kuna maendeleo zaidi Gombolamboto siyo tena mwisho wa Lami.

Uteuzi wa baraza kivuli la mawaziri wa leo tunaweza kusema ni Gongolamboto kwa akina David Kafulila na Hamad Rashid kwa maana ya kwamba katika safari yao ya kushirikishwa kwenye kambi rasmi ya upinzani hapo ndo mwisho wa lami. Hakuna uwezekano huo kwa sasa, LABDA baadaye, kama hiyo baadaye na wao watakuwemo.

Hawakupata uongozi wa kamati hata moja wala uwaziri kivuli. Lakini walihemshwa na support ya wabunge wa ccm na kusahau kwamba hawawezi kulazimisha uhusiano kwa kutumia kanuni za bunge. Sasa ccm wameshapata walichotaka, yaani kamati ya PAC kuongozwa na mtu wao (Cheyo). Habari imekwisha, Kafulila na Hamad wanauguza maumivu, Chadema wanachekelea na kusonga mbele.

I love politics, who loughs last loughs longer!!
 
:clap2:IMEKWISHA:clap2: Ni vema uwe makini na mtu unayeanzisha naye urafiki isiwe leo na kesho urafiki wenu ukaleta ukakasi na mwishowe mkatengwa na wote kukosa matunda ya urafiki wenu batili. "HAYA SASA NENDENI MKANYWE MAJI YA BETRI WASALITI WAKUBWA NYIE!!!!!!!!!!!!!
 
Kuna watu husema malipo ni hapa hapa lakini mimi sikutarajia wangepata malipo yao so soon na kwa aibu namna hii
 
Dar es Salaam kuna kituo cha basi huitwa Gongo la Mboto mwisho wa lami. Zamani hapo ndipo lami ya kutoka mjini ilikuwa inaishia na kwa hiyo daladala pia zilikuwa zinaishia hapo. Siku hizi kuna maendeleo zaidi Gombolamboto siyo tena mwisho wa Lami.

Uteuzi wa baraza kivuli la mawaziri wa leo tunaweza kusema ni Gongolamboto kwa akina David Kafulila na Hamad Rashid kwa maana ya kwamba katika safari yao ya kushirikishwa kwenye kambi rasmi ya upinzani hapo ndo mwisho wa lami. Hakuna uwezekano huo kwa sasa, LABDA baadaye, kama hiyo baadaye na wao watakuwemo.

Hawakupata uongozi wa kamati hata moja wala uwaziri kivuli. Lakini walihemshwa na support ya wabunge wa ccm na kusahau kwamba hawawezi kulazimisha uhusiano kwa kutumia kanuni za bunge. Sasa ccm wameshapata walichotaka, yaani kamati ya PAC kuongozwa na mtu wao (Cheyo). Habari imekwisha, Kafulila na Hamad wanauguza maumivu, Chadema wanachekelea na kusonga mbele.

I love politics, who loughs last loughs longer!!

toka amdhalilishe mbowe kwa uhodari wa kupangua hoja! hamad anachukiwa mno na CHADEMA! lakini ukweli unabaki palepale mnahitaji kujifunza toka kwake
 
Hapo alipo Kafulila na Hamad wakimuona mbunge wa chadema inakuwa kama mtu aliyetoroka jela ameona polisi. Hawakujua haya yote kabla ya kutafuta sifa kwa ccm?
 
ha! ha! haa! wabunge wenyewe ndio hawa kina LEMA na Mr 2? hamad hawezi kuhofia vilaza wewe umemsahau?
 
Uteuzi wa baraza kivuli la mawaziri wa leo tunaweza kusema ni Gongolamboto kwa akina David Kafulila na Hamad Rashid kwa maana ya kwamba katika safari yao ya kushirikishwa kwenye kambi rasmi ya upinzani hapo ndo mwisho wa lami. Hakuna uwezekano huo kwa sasa, LABDA baadaye, kama hiyo baadaye na wao watakuwemo.

Mungu akusamehe hujuwi ulitendalo!
 
ha! ha! haa! wabunge wenyewe ndio hawa kina LEMA na Mr 2? hamad hawezi kuhofia vilaza wewe umemsahau?

wewe tuliza akili yako bana, muziki ambao Lema amenanzisha Arusha ndio huu ulioshikisha adabu serikali, ccm, na bunge zima. Kila kiongozi wa serikali akisimama lazima aoneshe alivyokerwa na matukio ya Arusha, ccm nao, Bungeni ndio usipime. Wapiga kura wa Lema ndio wameimarisha mshikamano na mbunge wao kupita hata wakati wa uchaguzi. Spika anamuogopa anaomba taarifa ipelekwe ofisini kwake ili akabembeleze kwa kificho.

Katika siasa mtu anataka mafanikio gani zaidi ya hayo? The guy is just too hot for you
 
CDM hawajaenda bungeni kulala kama walivyo CCM, hawajaenda kwa rushwa km CCM. CCM wako kule kwa maslahi yao binafsi ndo maana utasikia utangulizi ktk kuongea wanataja hadi Bi wadogo wa mtaani eti kamfanikisha kuwa pale, shame on them
 
toka amdhalilishe mbowe kwa uhodari wa kupangua hoja! hamad anachukiwa mno na CHADEMA! lakini ukweli unabaki palepale mnahitaji kujifunza toka kwake

Hakuna kujifunza kutoka kwa mtu mnafiki wav kupindukia. Kwanza nadhani wengi wenu hamna habari kwamba Makinda alimtosa huyu Hamadi Rashidi ambnaye ukweli ni kwamba harakati zake zote za hujuma dhidi ya Chadema kumbe alikuwa anaimezea ile kamati ya Mashirika ya Umma -- POC, ile aliyopata Zitto. Alikuwa amepewleka maombi kwa Spika kuwamo katika kamati hiyo ili baadaye agombee uenyekiti. Badala yake Makinda akampeleka katika ile nyingine aliyopata.

Hamadi Rashidi ni mtu mwenye uchu sana wa madaraka!

Kwa hilo nampongeza Spika.

Kwa watakaouliza source yangu ni swahiba wangu aliyepo katika ofisi ya Spika ambaye alinihakikishia aliiona Fomu ya Hamadi kuomba kuwa katika POC.
 
Usimsahau Kafulila, ndiyo maana Chadema walimfukuza mapema
 
Back
Top Bottom