Hamad Rashidi ndiye aliyeisaliti Zanzibar

Hamad Rashidi ndiye aliyeisaliti Zanzibar

Kura mbili za rasimu zimepatikana kutoka kwa Hamad Rashidi mbunge wa Wawi imefahamika mjini Dodoma leo.

Katika hali ya kushangaza, Hamad Rashidi ndiye aliyepewa jukumu la kuwanunua wabunge wawili wa CUF (majina yanahifadhiwa) ili kukidhi akidi iliyotakiwa.

Wabunge hao ambao walikuwa wajumbe wa bunge maalum la katiba kabla ya kususia waliahidiwa kiasi cha shilingi milioni 250 za Kitanzania kila mmoja ili kufanikisha mpango huo. Aidha Hamad ndiye aliyepewa jukumu hilo la kuwashawishi huku wale waliopiga kura za siri za 'HAPANA' wakiwekwa kitako na Pinda pamoja na Seif Idd ili kukamilisha mpango huo.

Hamad Rashidi kwa sasa ndiye mtu anayejadiliwa zaidi hapa Dodoma kwa sasa kutokana na tukio hilo.

Updates...........
Hamadi Rashidi katika mahojiano na MWANANCHI JUMAPILI amekiri kuwashawishi wajumbe hao ili waipitishe rasimu ila amekana kuwanunua "Ni ushawishi wangu tu ili kuwakomoa CUF" alijigamba Rashidi.

Ila ukweli ni kuwa wajumbe hao waliahidiwa kiwango hicho cha fedha.

Pia wapo wa kura za siri waliopiga kura za 'HAPANA' takribani wajumbe 17 ingawa Hamadi Rashidi anatudanganya kuwa ni yeye aliwashawishi wapige kura za siri na wote walipiga za 'NDIYO' na anadai eti baada ya kupiga walikuwa wakimuonyesha ili athibitishe! Huu ni uongo wa wazi kabisa!!!!!
Wewe ni kutoka UKAWA ipi?! Ya Mangi ama Sultani?! Mbona hujatuwekea bayana Mara baada ya kupiga hizo kura Je hao wahishimiwa sana washapatiwa hivyo vifuta jasho vyao?! Makabidhiano ilikua wapi na Je unadhani Kama sio Hamad Rashid hiyo 2/3 ingepatikana ama la?! Mwisho Jeukiambiwa Kama hizi ndio zile siasa za KUSADIKIKA utakataa?!
 
baada ya kufukuzwa uanachama sasa ameanza kusaliti alikozaliwa,hajui kwamba laana hiyo itakiandama kizazi chake chote na amesahau kwamba kwa sasa ccm wamemtumia kama kondom NA hawana haja nae tena
Wasaliti ni wale wenye kutaka kurudisha zama za Masultani ambazo zishapita miaka mingi tu mara baada ya Mapinduzi na Mzee Karume kuingia madarakani na laana Mara nyingi inawapata wale walio wakosefu? Sasa Kama kutetea kile unachoamini ni usaliti basi na CUF wasaliti wakuu maana hakuna Mbunge wala muwakilishi aliyehudhuria bunge maalum ilhali walijua fika kwamba ndio eneo pekee la kuweza kuwapatia wafuasi wao Serikali ya Nkataba.
 
Tatizo alishawahi kufanya kazi melini huyu Hamad, ndiko walikomharibu. Baba gani anakuwa hivi? Itakuwa ni kitu cha mchele.
Ova
 
Kura mbili za rasimu zimepatikana kutoka kwa Hamad Rashidi mbunge wa Wawi imefahamika mjini Dodoma leo.

Katika hali ya kushangaza, Hamad Rashidi ndiye aliyepewa jukumu la kuwanunua wabunge wawili wa CUF (majina yanahifadhiwa) ili kukidhi akidi iliyotakiwa.

Wabunge hao ambao walikuwa wajumbe wa bunge maalum la katiba kabla ya kususia waliahidiwa kiasi cha shilingi milioni 250 za Kitanzania kila mmoja ili kufanikisha mpango huo. Aidha Hamad ndiye aliyepewa jukumu hilo la kuwashawishi huku wale waliopiga kura za siri za 'HAPANA' wakiwekwa kitako na Pinda pamoja na Seif Idd ili kukamilisha mpango huo.

Hamad Rashidi kwa sasa ndiye mtu anayejadiliwa zaidi hapa Dodoma kwa sasa kutokana na tukio hilo.

Updates...........
Hamadi Rashidi katika mahojiano na MWANANCHI JUMAPILI amekiri kuwashawishi wajumbe hao ili waipitishe rasimu ila amekana kuwanunua "Ni ushawishi wangu tu ili kuwakomoa CUF" alijigamba Rashidi.

Ila ukweli ni kuwa wajumbe hao waliahidiwa kiwango hicho cha fedha.

Pia wapo wa kura za siri waliopiga kura za 'HAPANA' takribani wajumbe 17 ingawa Hamadi Rashidi anatudanganya kuwa ni yeye aliwashawishi wapige kura za siri na wote walipiga za 'NDIYO' na anadai eti baada ya kupiga walikuwa wakimuonyesha ili athibitishe! Huu ni uongo wa wazi kabisa!!!!!

Weka ushahidi kuonyesha kuwa walipewa fedha. Mbona mnapenda sana kutunga uongo kila kukicha, huwezi kuaminiwa kwa kutunga uongo bali kusema kitu ambacho kweli. Na vilevile usipende kutmiwa kwa ajili ya maslai ya wanasiasa.
 
Wakati gazeti la Mwa-na-halisi bado lipo halijafungiwa, kuna siku mwandishi alisema hivi " tataizo la Hamdi Rashid ni aina ya biashara anayofanya". Baada ya hapo hakufafanua. Mimi ikabidi nianze kuuliza watu mbali mbali je Hamad Rashid anaanya biashara gani? Nilipewa majibu yanayofanana. Yaani wote walinieleza aina hiyo hiyo ya biashara. Ni biashara flani ambayo imeshamiri sana Tanzania.
 
Kwa mujibu wa website ya BMK, wajumbe ni 630. Wabunge wote wa Bunge la Muungano 347, Wajumbe wote wa Wajumbe wa Baraza la wawakîlishi 82 na wajumbe 201, Kati yao, wajumbe sita wa baraza la wawakilishi ni wabunge wa bunge la muungango. Hivyo idadi inabaki kuwa 624. Ukiondoa mmoja aliyefariki, wanabaki 623. Katibu wa bunge jana ametangaza kuwa jumla ya wabunge wa Zanzibar ni 219 na watanganyika ni 411. Jumla ni 630.

Hizo hesabu sio sawa na ndio maana wamefunga website ya Bunge la Katiba maana ilikuwa inaonesha composition na namna wajumbe walivyobaki 624 badala ya 630. Na hapô hawakuzungumzia mmoja aliyefariki!
 
Akidi haijatimia kwa sababu wajumbe kutoka Zanzibar ni 212 lakini kura zilizopigwa zinaonyeshwa zilikuwa 219, hizi kura 7 za hewa zilitoka wapi? Kuna wajumbe 7 waliochaguliwa kinyemela ili kuhakikisha akidi inatimia? Ofisi ya Bunge na Sitta mbona wako kimya kuhusu hizi kura 7 ambazo hazijulikani zimetoka wapi?
Mkuu, kwani matokeo ya urais Zanzibar hutangazwa vipi?
 
Sio tetesi mkuu ni kwel alafu cha ajabu mwenyew anakili kabisa na kujitapa……!!
 
Website ya Bunge la Katiba imeshafungwa? Ni yaleyale ya muendelezo wa Hadith za kale kwamba palitokea Tume ya Katiba na Bunge la Katiba.......

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Nakumbuka kipindi huyu jamaa akiwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni watu walaweza hata kumtaja kwa nafasi ya uraisi.
Njaa mbaya sana...
 
Huyu jamaa ni hatari zaidi ya ukoma!
 
Kwa mujibu wa website ya BMK, wajumbe ni 630. Wabunge wote wa Bunge la Muungano 347, Wajumbe wote wa Wajumbe wa Baraza la wawakîlishi 82 na wajumbe 201, Kati yao, wajumbe sita wa baraza la wawakilishi ni wabunge wa bunge la muungango. Hivyo idadi inabaki kuwa 624. Ukiondoa mmoja aliyefariki, wanabaki 623. Katibu wa bunge jana ametangaza kuwa jumla ya wabunge wa Zanzibar ni 219 na watanganyika ni 411. Jumla ni 630.

Hizo hesabu sio sawa na ndio maana wamefunga website ya Bunge la Katiba maana ilikuwa inaonesha composition na namna wajumbe walivyobaki 624 badala ya 630. Na hapô hawakuzungumzia mmoja aliyefariki!

Kwa hiyo 7 ni wanyongeza?
 
Back
Top Bottom