Hamad Rashid: Nitaunda chama kipya!

Hamad Rashid: Nitaunda chama kipya!

EasyFit

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2011
Posts
1,269
Reaction score
1,082
• Maalim Seif kunena leo Ikulu Zanzibar

KIONGOZI mashuhuri wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, amesema ataunda chama kipya na kikubwa cha siasa ikiwa atafukuzwa uanachama kwa kufuata taratibu na kanuni za Chama cha CUF.

Hamad alisema chama atakachounda mara baada ya kutoka CUF kitasheheni viongozi wengine walioko ndani ya chama hicho ambao hawakubaliani na uongozi wa sasa ambao umekifanya chama hicho kilichokuwa na nguvu kubwa kuwa dhaifu.

Hamad alibainisha hayo jana alipozungumza kwenye kipindi cha ‘Pambazuka’ kinachorushwa hewani na kituo cha televesheni cha Channel 10 na kuongeza kuwa haogopi kufukuzwa ndani ya CUF kama alivyotishiwa na baadhi ya viongozi wenzake wanaopingana, lakini akaonya kuwa hatua hizo zifuate kanuni na taratibu za chama.

Mbunge huyo wa Jimbo la Wawi alisema ikiwa viongozi hao watakiuka kanuni za chama za kumfukuza atawafikisha mahakamani kupinga kufukuzwa kwake, lakini iwapo ataridhika na taratibu zitakazotumika atashawishika kuunda chama kingine akishirikiana na viongozi wenzake.“Wakinifukuza sina mpango wa kuhamia chama chochote cha siasa, kwani mimi si malaya wa kisiasa. Nitawashawishi wenzangu tuanzishe chama chetu,” alisema.

Pamoja na hayo, alisema hata wakimfukuza chama hicho kitaendelea kuwa dhaifu kwa kuwa hivi sasa viongozi hawakiendeshi chama kama taasisi.“Nimefanya juhudi kubwa za kuimarisha chama Tanzania Bara, lakini pia kwa mujibu wa katiba kila mwanachama anapaswa kuimarisha chama katika eneo analoishi na mimi naishi Kinondoni, hivyo nilikuwa sahihi kuitisha mkutano ule, lakini cha kushangaza wakawaleta Blue Guards na kuwapiganisha na wanachama,” alisema.

Akizungumzia chanzo cha mzozo huo, Hamad alisema unatokana na kutangaza nia ya kutaka kuwania nafasi ya ukatibu mkuu na baadhi ya wanachama kuhoji masuala ya msingi ndani ya chama ambao anadaiwa kuwapandikiza.“Katika mkutano halali wa Baraza Kuu, Rakesh, Doyo Hassan na Yassin Mrotwa walihoji matumizi ya fedha za chama sh milioni 500 zipo wapi. Wakadai eti nimewapandikiza,” alisema.

Alisema alihoji matumizi ya sh milioni 307 katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, lakini mpaka sasa hajapatiwa majibu jinsi fedha hizo zilivyotumika.“Watu wanapohoji matumizi hayo, wanaambiwa ni kundi langu, lakini katika uchaguzi huo, Mtatiro anasema walitumia sh milioni 49 kukodi ndege mara tatu. Atuambie chenji yetu iko wapi?“Wanatumia rasilimali za chama kuchafua jina langu bila kunishirikisha.

Hivi kutangaza nia ya kuwania nafasi ya ukatibu mkuu imekuwa nongwa? Mbona Maalim Seif ametangaza nia hiyo katika mkutano wa baraza kuu?” alihoji.Alisema kuwa baadhi ya viongozi wanamtuhumu kuhongwa sh milioni 700 na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumshawishi Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) kugombea urais kwa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao na yeye awe mgombea mwenza na pia wanamtuhumu kukipa nguvu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).“Madai yote haya yanayoelekezwa kwangu hayana ushahidi wowote.

Mtatiro ananiita muasi, amepata wapi mamlaka hiyo? Ina maana ameshanihukumu bila ya kunisikiliza? Mbona hatuendi na kaulimbiu ya chama ‘Haki sawa kwa wote?’ “Mimi sina ukorofi, lakini wao wanatumia vikao kunichafua, sipewi nafasi nikizungumza kwenye vyombo vya habari naonekana mkorofi, sasa wanataka nifanyeje?” aliuliza mbunge huyo.Alionesha kushangazwa kwake na kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ambayo alisema ndani ya CUF haipo, labda kama imeundwa hivi karibuni.

Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad leo anakutana na waandishi wa habari Ikulu, Zanzibar. Hata hivyo haijajulikana nini atakiongea, ingawa kuna madai kuwa atazungumzia sakata hilo la mgogoro baina yake na Hamad Rashid.Katika siku za hivi karibuni kumezuka mzozo kati ya mbunge huyo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, uliosababisha kuzuka kwa mapigano makali na watu kadhaa kujeruhiwa baina ya wanachama wanaowaunga mkono.::Tanzania Daima::

UP DATE 22:51
quote_icon.png
By Julius Mtatiro
Hakuna kitu kama hicho, ni propaganda tu ambazo hazina maana yoyote ile. Mikataba ya kukodi helikopta niliisaini mie on line nikiwa igunga, malipo yalifanywa na ofisi kuu moja kwa moja kwenda kwa kampuni husika.

Kwa vyovyote vile fedha hazikupitia mikononi mwangu, lakini hata hivyo mikataba na malipo vyote viko sawa kabisa. kwa hiyo kama kwa ndugu yangu huyo hapo ndo anatafuta kashfa za kulazimisha amepotea njia.

Jambo la pili, kama kuna fedha zozote zimeibiwa na mtu yeyote ndani ya chama, vikao vya chama ndiyo huwasilishiwa hoja hii na ushahidi wake kisha vinafanya maamuzi. Kama kuna ubadhirifu wowote wa fedha haisemwi kwa maneno tu, atuwekee hapa helikopta ilikodiwaje, fedha zilipitia kwa nani na nani alikula ngapi, asiseme kirahisi namna hiyo.

All in all details za maswala yote haya chama ndo kitayatizama na kuamua. Hadi tunajibu hoja hizi zisizo na mweleko wala ushahidi wowote katika mitandao ni kwa sababu tu wachache miongoni mwetu wameacha misingi ya kuhoji masuala ya chama vikaoni, wamechanganyikiwa sasa wanahyahoji kwenye vyombo vya habari.

Chama kitawarudisha kwenye mstari na kwa hakika chama kitatangulia kwanza na maslahi ya mtu mmoja mmoja yatafuata nyuma yake. Juzi zilitolewa hoja mara ooh.... mtatiro bado mdogo,.......mara ooh...amejiuzia magari, mara.....ooh amekula 500 milioni...... mara ooh amekula pesa za helikopta. Hizi zote ni njia za kunirudisha nyuma katika ninachokisimamia.

Nitasimama kidete na umri huu huu unaoitwa mdogo, nitaongoza chama changu kwa sababu ndilo jukumu nililokabidhiwa na wanachama wenzangu hadi pale nitakapoacha mwenyewe au vinginevyo. Nataka kusisitiza akuwa kinachoingoza CUF ni katiba, na iwapo kiongozi yeyote anavunja katiba waziwazi na anataka kuvunja chama na kukiua, sitosita kusimama na kusema fulani unataka kuua chama, fulani umeasi.

Sitaogopa propaganda zozote ambazo zitatengenezwa juu yangu kwani najua hazitapata ushahidi hata siku moja.
Nina moral authority ya kuongea haya! Ninarudia tena, NINA MORAL AUTHORITY YA KUSEMA HAYA, NA SINA WASIWASI WOWOTE, NAJIAMINI, SIJAIBA HATA SENTI TANO KATIKA CHAMA CHANGU, NA HATA SIKU MOJA HAITATOKEA MTU AKAJA NA USHAHIDI HUO, HUYO ANAYETOA SHUTUMA HIZO AKAPUMZIKE ATULIE, KUZEEKA KWINGINE NI KUBAYA MNO. ASITAFUTE MTU WA KUFA NAYE.

Mie nilijiunga CUF peke yangu na nimefika hapa nilipo bila kubebwa wala kumtumikia mtu, Na ninaahidi kwa uwezo mungu nitakwenda mbele au nyuma bila kutegemea msaada wa mtu wala kubebwa.Nasimamia maadili ya chama, utamaduni wa chama changu. Kila kitu kitajulikana mbele ya safari, tutajua pumba na mchele, tutajua nani anasema ukweli na nani anadanganya, tuupe muda nafasi.Julius Mtatiro
 
KIONGOZI mashuhuri wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamad Rashid Mohamed, amesema ataunda chama kipya na kikubwa cha siasa ikiwa atafukuzwa uanachama kwa kufuata taratibu na kanuni za Chama cha CUF.
Hamad alisema chama atakachounda mara baada ya kutoka CUF kitasheheni viongozi wengine walioko ndani ya chama hicho ambao hawakubaliani na uongozi wa sasa ambao umekifanya chama hicho kilichokuwa na nguvu kubwa kuwa dhaifu.
Hamad alibainisha hayo jana alipozungumza kwenye kipindi cha ‘Pambazuka’ kinachorushwa hewani na kituo cha televesheni cha Channel 10 na kuongeza kuwa haogopi kufukuzwa ndani ya CUF kama alivyotishiwa na baadhi ya viongozi wenzake wanaopingana, lakini akaonya kuwa hatua hizo zifuate kanuni na taratibu za chama.
Mbunge huyo wa Jimbo la Wawi alisema ikiwa viongozi hao watakiuka kanuni za chama za kumfukuza atawafikisha mahakamani kupinga kufukuzwa kwake, lakini iwapo ataridhika na taratibu zitakazotumika atashawishika kuunda chama kingine akishirikiana na viongozi wenzake.
“Wakinifukuza sina mpango wa kuhamia chama chochote cha siasa, kwani mimi si malaya wa kisiasa. Nitawashawishi wenzangu tuanzishe chama chetu,” alisema.
Pamoja na hayo, alisema hata wakimfukuza chama hicho kitaendelea kuwa dhaifu kwa kuwa hivi sasa viongozi hawakiendeshi chama kama taasisi.
“Nimefanya juhudi kubwa za kuimarisha chama Tanzania Bara, lakini pia kwa mujibu wa katiba kila mwanachama anapaswa kuimarisha chama katika eneo analoishi na mimi naishi Kinondoni, hivyo nilikuwa sahihi kuitisha mkutano ule, lakini cha kushangaza wakawaleta Blue Guards na kuwapiganisha na wanachama,” alisema.
Akizungumzia chanzo cha mzozo huo, Hamad alisema unatokana na kutangaza nia ya kutaka kuwania nafasi ya ukatibu mkuu na baadhi ya wanachama kuhoji masuala ya msingi ndani ya chama ambao anadaiwa kuwapandikiza.
“Katika mkutano halali wa Baraza Kuu, Rakesh, Doyo Hassan na Yassin Mrotwa walihoji matumizi ya fedha za chama sh milioni 500 zipo wapi. Wakadai eti nimewapandikiza,” alisema.
Alisema alihoji matumizi ya sh milioni 307 katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, lakini mpaka sasa hajapatiwa majibu jinsi fedha hizo zilivyotumika.
“Watu wanapohoji matumizi hayo, wanaambiwa ni kundi langu, lakini katika uchaguzi huo, Mtatiro anasema walitumia sh milioni 49 kukodi ndege mara tatu. Atuambie chenji yetu iko wapi?
“Wanatumia rasilimali za chama kuchafua jina langu bila kunishirikisha. Hivi kutangaza nia ya kuwania nafasi ya ukatibu mkuu imekuwa nongwa? Mbona Maalim Seif ametangaza nia hiyo katika mkutano wa baraza kuu?” alihoji.
Alisema kuwa baadhi ya viongozi wanamtuhumu kuhongwa sh milioni 700 na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kumshawishi Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) kugombea urais kwa chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao na yeye awe mgombea mwenza na pia wanamtuhumu kukipa nguvu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
“Madai yote haya yanayoelekezwa kwangu hayana ushahidi wowote. Mtatiro ananiita muasi, amepata wapi mamlaka hiyo? Ina maana ameshanihukumu bila ya kunisikiliza? Mbona hatuendi na kaulimbiu ya chama ‘Haki sawa kwa wote?’
“Mimi sina ukorofi, lakini wao wanatumia vikao kunichafua, sipewi nafasi nikizungumza kwenye vyombo vya habari naonekana mkorofi, sasa wanataka nifanyeje?” aliuliza mbunge huyo.
Alionesha kushangazwa kwake na kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Maadili ambayo alisema ndani ya CUF haipo, labda kama imeundwa hivi karibuni.
Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad leo anakutana na waandishi wa habari Ikulu, Zanzibar. Hata hivyo haijajulikana nini atakiongea, ingawa kuna madai kuwa atazungumzia sakata hilo la mgogoro baina yake na Hamad Rashid.
Katika siku za hivi karibuni kumezuka mzozo kati ya mbunge huyo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Shariff Hamad, uliosababisha kuzuka kwa mapigano makali na watu kadhaa kujeruhiwa baina ya wanachama wanaowaunga mkono.


[TD="bgcolor: #ffffff"]
Hamad Rashid: Nitaunda chama kipya
• Maalim Seif kunena leo Ikulu Zanzibar

na Tamali Vullu


[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF, align: center"]
amka2.gif
[/TD]
 
Muanzisha hii lazima utakuwa unatumia Laptop kutoka kwa Hu Jintao...thread ina matege!
 
Hamad Rashid aliibuliwa na Mkapa kwa kupewa ubunge wa upendeleo ('viti maalumu 10 vya rais'), umakini wake ukafanya wabunge wa upinzani wamteua kuwa kiongozi wa upinzani bungeni, siasa hubadilika, leo kaukosa ukuu wa upinzani bungeni (hata baada ya kuja na dhana ya minority group na kina Kafulila) ndo tunaona rangi yake halisi ya TAMAA na KUPENDA MAMLAKA anahangaika kuhasimisha CUF, Kama anadhani anaweza kuidhoofisha CUF basi aanzishe hicho chama ('utabiri wa Mayage atautimiza') tuuone mwisho wa mwanzo wake
 
Kumbe amejua atafukuzwa, nilizani anapigana kuijenga CUF kumbe alikuwa na lengo lake, watu wengine amejuaje chama atakachounda kitakuwa kikubwa.
 
Who will trust you this time you mean the business?
I bet you, in Africa now, there are so many confused people all around. Almost in all spheres.And the painful thing is the guys have the ability still yet to convince people to become followers.
 
Mbunge huyo wa Jimbo la Wawi alisema ikiwa viongozi hao watakiuka kanuni za chama za kumfukuza atawafikisha mahakamani kupinga kufukuzwa kwake, lakini iwapo ataridhika na taratibu zitakazotumika atashawishika kuunda chama kingine akishirikiana na viongozi wenzake.
Jamani naombeni msaada anasema endapo ataridhika na taratibu za kufukuzwa, sasa kama ataridhika kwa nini tena aunde chama kingine akiache kinachofuta taratibu? just thinking aloud.
 
Hana lolote huyu anatapatapa kwa kukosa madaraka baada ya kukosa kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni
 
Jamani naombeni msaada anasema endapo ataridhika na taratibu za kufukuzwa, sasa kama ataridhika kwa nini tena aunde chama kingine akiache kinachofuta taratibu? just thinking aloud.
Unakumbuka 'umaarufu' alioupata 'naibu waziri mkuu' wa kipindi cha Mwinyi! HR kapata umaarufu ndani ya cuf na sasa angependa kuwa kama A.L. Mrema
 
Hamad sasa ni wakati wa kuunda chama na kukiita wachuja nafaka! Sipati picha kitakavyowika...
 
Mie nashangilia kweli ninavyomuona Hamad akiweweseka........... aliwashambulia sana CHADEMA kwa sifa zote ambazo ndizo anazozitekeleza kwa sasa!!

Ni mnafiki, mzandiki, choyo, kigeugeu, mwongo, mbinafsi you name it

kweli siku hizi baya hulipwa hapahapa duniani
 
Alisema alihoji matumizi ya sh milioni 307 katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, lakini mpaka sasa hajapatiwa majibu jinsi fedha hizo zilivyotumika.

"Watu wanapohoji matumizi hayo, wanaambiwa ni kundi langu, lakini katika uchaguzi huo, Mtatiro anasema walitumia sh milioni 49 kukodi ndege mara tatu. Atuambie chenji yetu iko wapi?"Wanatumia rasilimali za chama kuchafua jina langu bila kunishirikisha. Hivi kutangaza nia ya kuwania nafasi ya ukatibu mkuu imekuwa nongwa? Mbona Maalim Seif ametangaza nia hiyo katika mkutano wa baraza kuu?" alihoji.
Mtatiro kajibu
Hakuna kitu kama hicho, ni propaganda tu ambazo hazina maana yoyote ile. Mikataba ya kukodi helikopta niliisaini mie on line nikiwa igunga, malipo yalifanywa na ofisi kuu moja kwa moja kwenda kwa kampuni husika. Kwa vyovyote vile fedha hazikupitia mikononi mwangu, lakini hata hivyo mikataba na malipo vyote viko sawa kabisa. kwa hiyo kama kwa ndugu yangu huyo hapo ndo anatafuta kashfa za kulazimisha amepotea njia.Jambo la pili, kama kuna fedha zozote zimeibiwa na mtu yeyote ndani ya chama, vikao vya chama ndiyo huwasilishiwa hoja hii na ushahidi wake kisha vinafanya maamuzi. Kama kuna ubadhirifu wowote wa fedha haisemwi kwa maneno tu, atuwekee hapa helikopta ilikodiwaje, fedha zilipitia kwa nani na nani alikula ngapi, asiseme kirahisi namna hiyo. All in all details za maswala yote haya chama ndo kitayatizama na kuamua. Hadi tunajibu hoja hizi zisizo na mweleko wala ushahidi wowote katika mitandao ni kwa sababu tu wachache miongoni mwetu wameacha misingi ya kuhoji masuala ya chama vikaoni, wamechanganyikiwa sasa wanahyahoji kwenye vyombo vya habari. Chama kitawarudisha kwenye mstari na kwa hakika chama kitatangulia kwanza na maslahi ya mtu mmoja mmoja yatafuata nyuma yake. Juzi zilitolewa hoja mara ooh.... mtatiro bado mdogo,.......mara ooh...amejiuzia magari, mara.....ooh amekula 500 milioni...... mara ooh amekula pesa za helikopta. Hizi zote ni njia za kunirudisha nyuma katika ninachokisimamia. Nitasimama kidete na umri huu huu unaoitwa mdogo, nitaongoza chama changu kwa sababu ndilo jukumu nililokabidhiwa na wanachama wenzangu hadi pale nitakapoacha mwenyewe au vinginevyo. Nataka kusisitiza akuwa kinachoingoza CUF ni katiba, na iwapo kiongozi yeyote anavunja katiba waziwazi na anataka kuvunja chama na kukiua, sitosita kusimama na kusema fulani unataka kuua chama, fulani umeasi. Sitaogopa propaganda zozote ambazo zitatengenezwa juu yangu kwani najua hazitapata ushahidi hata siku moja. Nina moral authority ya kuongea haya! Ninarudia tena, NINA MORAL AUTHORITY YA KUSEMA HAYA, NA SINA WASIWASI WOWOTE, NAJIAMINI, SIJAIBA HATA SENTI TANO KATIKA CHAMA CHANGU, NA HATA SIKU MOJA HAITATOKEA MTU AKAJA NA USHAHIDI HUO, HUYO ANAYETOA SHUTUMA HIZO AKAPUMZIKE ATULIE, KUZEEKA KWINGINE NI KUBAYA MNO. ASITAFUTE MTU WA KUFA NAYE.Mie nilijiunga CUF peke yangu na nimefika hapa nilipo bila kubebwa wala kumtumikia mtu, Na ninaahidi kwa uwezo mungu nitakwenda mbele au nyuma bila kutegemea msaada wa mtu wala kubebwa.Nasimamia maadili ya chama, utamaduni wa chama changu. Kila kitu kitajulikana mbele ya safari, tutajua pumba na mchele, tutajua nani anasema ukweli na nani anadanganya, tuupe muda nafasi.Julius Mtatiro
 
Duh! HR nilifikiri ulikuwa una point, kumbe hata wakifuata taratibu lazima utaondoka kuunda chama??

Sasa si ungeunda tu chama chako bila kuharibu CUF

What a stupidity?? kwani lazima unyee kambi kwanza au ulikuwa kwenye mission from very beginning
 
Back
Top Bottom