Njilembera
JF-Expert Member
- May 10, 2008
- 1,496
- 610
Kama 2 ziliwezekana kwanini 3 zisiwezekane??uzoefu wa serikali 2 upo wapi duniani?inakuwaje mtu anaongea kwa lengo la kufurahisha watu fulani?serikali 2 ni ulaghai wa ajabu!!nchi ndani ya nchi!!mipaka ndani ya nchi!!amiri jeshi wakuu wawili ndani ya nchi!!
Suruhisho hapa ni serikali moja
Watu wote wenye akili ya kuweza kupata A+ watakuja na jibu kama lako, na wale wanaoweza kujikongoja na kupata D ndio mashabiki wakuu wa serikali mbili. Wa serikali tatu ndio wamo katikati ya hizi marks mbili. Mwenye akili na aelewe tuliposimama!
Mwambie Marekani wana serikali tatu kwa maana wana United States (serikali ya Muungano) na utitiri wa serikali aina ya Tanganyika na Zanzibar (states). Hata kule Nigeria - wana Federal State halafu serikali nyingi (usiseme majimbo maana utararuliwa hapa).

Mbili zipo wapi Duniani
Katika kipindi cha jambo tanzania leo tbc one amesema hakuna haja ya serikali 3 kikubwa kutatua kero za muungano,maana hatuna uzoefu wa serikali 3 popote duniani
Ni Watanganyika ndio wanaodai Tanganyika yao,yeye Mzanzibari yanamhusu nini?
Atajibu nini iwapo ataulizwa kuwa mbona nyinyi Wazanzibari mna nchi ndani ya muungano halafu hutaki Watanganyika wapate nchi yao?
Huyu anamsaidia Pengo bila ya kujijua.
Uzoefu wa Serikali 2 uko wapi?
Katika kipindi cha jambo tanzania leo tbc one amesema hakuna haja ya serikali 3 kikubwa kutatua kero za muungano,maana hatuna uzoefu wa serikali 3 popote duniani
Ulitarajia mawazo gani kutoka kwa mbunge wa mahakama na pandikizi la ccm.
BiG up Mkuu, jibu zuri sana. Na kwambia Ben Saanane siku zote hana point.Tanzania
Hawa watu ni wehu, kila siku malalamiko yalikuwa Tanganyika imeifanya Zanzibar kuwa koloni lake sasa fursa ya kujitoa kwenye hilo koloni imepatikana , wanaanza mara ohh hakuna haja ya serikali tatu......wanaangaliaa Ubunge wao tu na wala sio masilahi ya Zanzibar hawa .......
kero hazitatuliki zilee... Tumekuwanazo tangu day one ya muungano...
Yeye kama mtu alierubuniwa kuigawa CUF sasa anataka kulipa fadhira miaka yote hamsini kero hizo zimeshindikana leo ndo zitaisha !!? Kwa kuwa yeye ni mzanzibar ningempongeza kama angependekeza seikali moja kuliko kuja na porojo zake hizo huyu mwanzilishi wa ADC.
Katika kipindi cha jambo tanzania leo tbc one amesema hakuna haja ya serikali 3 kikubwa kutatua kero za muungano,maana hatuna uzoefu wa serikali 3 popote duniani
Mambo ya chama yanawashinda mnataka serikali 3 mtapata?
Wajanja wote hawawezi kuunga mkono serikali tatu kwa dakika moja.
Oh!Kakaa sana bara anajisikia Mtanganyika.
Serikali 3 ni itakuwa moja ya kero kubwa za Muungano, ni ya kupiga vita kwa nguvu zote.