Hamad Rashid: CHADEMA ni chaka la wanaokimbia CCM

Cuf ni tawi la ccm, ccm ni kichaka cha mafisadi na watu wanaohujumu maliasili za nchi hii, nani asiyejuwa?

Cuf siyo chama cha upinzani tena kilishapewa haruwa ya gnu zanzibar
 
Mmmh ndiyo maana kuna wanasiasa na wataalam wa siasa. Huyu jamaa ndiye anaonekana smart kwenye chama chake CUF. Na kama huyu genius wa CUF anaongea huu upupu (pupuka) sasa waliobaki itakuwaje? Kasahahu kuwa hata yeye alikuwa CCM.

Hilo ni swali la msingi: Genius wa CUF anapochemka, waliobaki inakuwaje
?

Lakini yeye ni tofauti na ndio maana kaenda CUF. Ama kweli wengine akili zenu hamzitumi. Hivyo unamlaumu kwa kusema ukweli kuwa kila anaeondoka na kila anaepingana na CCM nyinyi huwa ndiyo swahiba wenu? Hili nalo unakanusha na kuliona upupu. Kwa mie ninaejuwa maana ya upupu nakupongeza kwa sifa za bure ulizompa Hamadi Rashid kwa kusema kile ambacho kiko wazi. Upupu humuwasha mtu na hilo ndilo lilokufanya uruke, upupu unakuwasha.
 
Niliwahi kumwambia Jussa na Rashid juu ya kile kinachoitwa serikali ya umoja wa kitaifa na muungano na CCM na wao wakasema kuwa sisi tunapenda CUF imalizike bara, Hivyo nikawambia kuwa Chama cha Upinzani Tanzania ni CHADEMA ilikuwa kabla ya uchaguzi mkuu na pia yeye mwenyewe ameona, Ila kwao kusema CHADEMA ndio watu wanazidi kuona kuwa wao ndio wasaliti wakubwa, badala ya kutumia muda wao mwngi sana kusema mabaya ya CCM wao wanatumia kusema CHADEMA hapa ndio kuna tofauti kubwa sana kati ya CHADEMA na CUF.. CUF bara imekufa na imekufa na kule Zanzibar wamebaki demokrasia hivyo hakuna upinzani. Ukweli ni kuwa mti mzuri CHADEMA ndio unatupiwa mawe. Rashid jenga upya CUF na siyo kusema CHADEMA
 
Wakuu,
Msiyafanyie dhihaka maneno ya Hamad Rashid kwa sababu ndiye sauti kubwa ya CUF leo baada ya ndoa yao na CCM..

Kinachonishangaza ni pale Hamad Rashid anapodai CDM ina mahusiano ya karibu na CCM wakati ni wao walifunga doa hata kabla ya uchaguzi mkuu..
Na kama mnakumbuka waliombwa na Chadema ku pendekeza mgombea wao kiti cha Spika wakakataa na kumchagua Anna Makinda wa CCM kwa shinikizo kutoka Zanzibar.. kisha baada ya hapo wakataka ati kuungana na CDM baada ya kuwapiga chini bungeni huyu Rashid akitamba ktk vyombo vya habari ati wanataka sana kuungana na CDM....

Hivi kweli wanachama wa CUF hasa bara wanashindwa kuliona hili kwamba nguvu ya CUF imeelekezwa visiwani, huku bara hakuna agenda ila wameachwa na Lipumba wao.. Maamuzi yote yanatoka Zanzibar na kwa maslahi ya Wazanzibar kisha wepesi kunyooshea CDM kidole kama CCM kwa kila hoja wako nyuma ya mabwana zao.....

Sasa hizi nyege gani jamani hawa CUF..Kwa CCM wanaunga mkono hadi sera za CCM bungeni, wamekula njama na CCM kuchukua hata kamati za bunge, lakini bado wamtutakana CDM hali CUF inatumia Ilani ya CCM ktk kuijenga Zanzibar.

Kibaya zaidi muafaka wa CUF na CCM, hata kama uchaguzi wa mwaka 2015, chama cha CUF kitashinda kwa kura zozote zile ni lazima wataunda serikali ya mseto na CCM - Regardless.. Hivi kweli kuna ukaribu zaidi ya hapo..
CUF chagueni mume mmoja, mnamtaka CCM au CDM maanake umalaya wa kisiasa hautaweza kuwasaidia kwani wananchi wamekwisha shtuka..

Natabiri kwamba the next move CUF inajiandaa kutumia udini kwa maelekezo ya bwana wao na hakika mtafanya makosa makubwa sana...

Hivi ni lazima CUF iwe na Chadema? ikiwa CUF wenyewe ndio walivunja muafaka na CDM na kuunda ndoa yao na CCM kwa maslahi ya Zanzibar...
Je, kuna uongo au lililojificha hapa?
 
Hapa nanataka kujifurahisha tu. Ukiwachia viongozi vijana (baadhi yao), yeyote aliye na umri kuanzia miaka 30 alitoka CCM. Tukumbuke kuwa tulikuwa na CCM mpaka mwaka 1992, na wakati huo ilikuwa lazima uwe mwanachama wa CCM. Kwa hiyo yeye Hamad na viongozi wengi wa vyama vya upinzania walitoka huko kabla hawajaingia kwenye upinzani.

Maneno ya Hamad yananikumbusha maneno ya Juma Duni aliposema "Mwaka 1995 ndio mwisho wa utawala wa mtu mweusi" bila ya kujisahau kuwa yeye ikiwa hajacheka haonekani jinsi alivyo mweusi. Wanasiasa bana, wee wacha tu!
 
Hamad kwisha kazi!ww ulitaka waende wapi?CUF na Ccm mmeungana,kilichoko cuf ndicho kilichoko ccm,pia wanaangalia chama kipi kinapendwa na wtanzania,kip kinalengo la dhati la kumkomboa mTz,kipi kiko angalao 90% ya tz.uende cuf kiko 0.005% ya tz ili iweje?mwisho nimtie moyo kuwa kigogo wa ccm anayetoka pemba pekee ndiye anaweza kujiunga cuf.lakini wengine wote People' Power!

Hamadi alitaka uwaziri wa mgao toka serikali ya mseto wakamtosa. Akawaomba chadema umoja wa upinzani chadema wakagoma sasa ameona amalize ghadhabu zake kwa kupayuka. Pole mheshemiwa Hamad maana Chaka ulilolitamani kuingia linakukimbia
 
hamad rashid ni mhuni hizo ni siasa za kuwahadaa wajinga ili waamini chama cha chake tu, sasa basi ifikie hatua kwenye siasa wawe wanaongea ukweli wa mambo, hasa malengo makubwa ya vyama vya siasa.
 
Lipumba alikuwa CCM
Maalim alikuwa CCM
Juma Duni alikuwa CCM
Marhem Shaban Mloo (Apumzike kwa Amani) alikuwa CCM
Machano alikuwa CCM
Musobi alikuwa CCM
Mapalala alikuwa CCM
Hamad Rashid alikuwa CCM
Orodha ni ndefu unaweza kuiongeza
SIJAMUELEWA WALA SITAMUELEWA HAMAD RASHID JUU YA HILI
 
Hao Viongozi wote wa CUF walitoka Wapi? hata yeye alikuwa Mshauri wa Rais Mwinyi wakati huo haupati madaraka hayo kama wewe sio CCM
Huyu jamaa kenge kweli, hivi Maalim Seif Katibu mkuu wa CUF alikuwa waziri kiongozi alikuwa mwanachama wa chama gani?
 
Lipumba alikuwa CCM
Maalim alikuwa CCM
Juma Duni alikuwa CCM
Marhem Shaban Mloo (Apumzike kwa Amani) alikuwa CCM
Machano alikuwa CCM
Musobi alikuwa CCM
Mapalala alikuwa CCM
Hamad Rashid alikuwa CCM
Orodha ni ndefu unaweza kuiongeza
SIJAMUELEWA WALA SITAMUELEWA HAMAD RASHID JUU YA HILI
Muelewe kama zwazwa tu!
 
Back
Top Bottom