Hamad Rashid avuliwa uanachama ADC

Hamad Rashid avuliwa uanachama ADC

Bado ni mgombea kwa mujibu wa tangazo la JECHA
Chama au mgombea wana uwezo wa kujitoa katika hatua yoyote ile ya uchaguzi. Hapa ADC inachotakiwa ni kuitaarifu Tume ya Uchaguzi kuwa hawana mgombea wa Kiti cha Urais kwa sababu waliyekuwa naye amefukuzwa uanachama, na siyo mwanachama wao tena.
 
Naona safari yake ya kurudi CCM imeshakamilika, sasa ana kila sababu ya kurejea kwenye chama chake cha zamani, maana hata michango yake bungeni kwa siku za karibuni, ilikuwa inaiunga mkono CCM.
 
Aliyekuwa mgombea Urais kupitia chama cha ADC Zanzibar amevuliwa uanachama wa chama hicho baada ya kuunga kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Rais na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi zanzibar ZEC, Bwana JECHA.

Dhambi ya usaliti malipo ni hapa hapa duniani.
huyu hamadi ni wakufuza zanzibar
 
Chama au mgombea wana uwezo wa kujitoa katika hatua yoyote ile ya uchaguzi. Hapa ADC inachotakiwa ni kuitaarifu Tume ya Uchaguzi kuwa hawana mgombea wa Kiti cha Urais kwa sababu waliyekuwa naye amefukuzwa uanachama, na siyo mwanachama wao tena.
Kama ADC wamemtimua kwa yeye kusapoti uchaguzi kurudiwa it means ADC hawaungi mkono uchaguzi kufutwa na kurudiwa,kama hawaungi mkono uchaguzi kurudiwa it means hakuna haja ya kuitaarifu ZEC kua Mgombea wao si mwanachama tena.Hapo ndipo CCM watatumia kama opportunity ya ku-assume kua Hamad bado mgombea kupitia ADC na kukamilisha matakwa yao.!
 
Aliyekuwa mgombea Urais kupitia chama cha ADC Zanzibar amevuliwa uanachama wa chama hicho baada ya kuunga kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Rais na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi zanzibar ZEC, Bwana JECHA.

Dhambi ya usaliti malipo ni hapa hapa duniani.
Arudi ccm rasmi,maana tushamjua kuwa yy si mwanamabadiliko!!!
 
Jecha kasema hakuna mabadiliko ya mgombea, ADC hawana mgombea?
 
Sijui wataongeza muda tena? Na sijui watachapisha tena karatasi za kura. Hata shetani anashangaa huu upuuzi unaoendelea
 
ADC ni kijichama kidogo sana lakini kimenipa matumaini makubwa sana , hongereni kwa uzalendo .
 
ni hivi , ukubwa wa laana ya usaliti umewekwa wazi sana ndani ya vitabu vitakatifu , hapo bado , kwa mujibu wa maandiko matakatifu yatamfika makubwa zaidi , shukrani zimwendee Mwenyezi Mungu ambaye aliweka utaratibu huu miaka mingi iliyopita .
Umenena maneno mazitio na muhimu sana katika maisha ya binadamu
 
Katika siasa hakuna kuona aibu, arudi tu kwenye chama chake cha zamani.
Nadhani itamuwia vigumu sana kurudi CUF, kwa sababu kadhia zake zilianza tangu enzi za bunge la katiba, wenzie waliposusia bunge la katiba yeye aliendelea kukaa ndani. Hasameheki
 
Aende CCM kwa wanafiki wenzake na hongera sana ADC kwa kazi nzuri mliyoifanya.
 
Aliyekuwa mgombea Urais kupitia chama cha ADC Zanzibar amevuliwa uanachama wa chama hicho baada ya kuunga kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Rais na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi zanzibar ZEC, Bwana JECHA.

Dhambi ya usaliti malipo ni hapa hapa duniani.
Nyiee! Mnamvua Rais uanachama wakati yeye ndo mwenye chama?
 
Aliyekuwa mgombea Urais kupitia chama cha ADC Zanzibar amevuliwa uanachama wa chama hicho baada ya kuunga kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Rais na Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi zanzibar ZEC, Bwana JECHA.

Dhambi ya usaliti malipo ni hapa hapa duniani.
Safi sana. Msaliti mkubwa huyu. Ajaribu TADEA. Huko anaweza kufahamiana na msaliti mwenzie Shibuda
 
Huyu Hamad Rashid ni walewale akina Jecha, tusubili tuone kama ma CCM hayata mlinda kwa kumuagiza Jecha amuweke katika wagombea urais kwa kigezo kua aligombea swali.
 
Kanunuliwa, ni mkakati wa bao la mkono ccm, waseme kura za hamad rashid kachukua shein.
 
Back
Top Bottom