KIM KARDASH
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 5,139
- 1,150
Hamad R hata kama yuko sahihi lakini strategy anayotumia ya kupambana kwa nguvu aslani hatafika popote mbele ya Seif. Ingawa hadi sasa sielewi nani anatumiwa kati ya Hamadi na Seif lakini HR aelewe Seif ndiye kashika mpini hata kama CCM wanamtumia HR hawatamuacha mshirika wao mkuu Seif.
kenge mimi wao vichenchede............hawataki wasi wao makenge wasio na mkia
Lipumba alikosea njia kuingia cuf,bora angebaki ccm,asingefanya pupa mkapa ilikua ampe uwaziri kumuandaa awe rais au waziri mkuu wa Tanzania,najua wengi mtashangaa lakini huu ndio ukweli,nitaumwaga hapa siku moja,mumjue lipumba alikotokea mpaka kufika hapo alipo,kiufupi akiwa chuo kikuu yeye alikua katibu wa TANU youth league wakati jk akiwa mwenyekiti wake,na ni hapo hapo chuo kikuu ndipo walikutana na kujuana na maalimu seif aliejiunga chuoni hapo katika mpango maalum wa kuwasukuma wazanzibar....
Shughuli pevu ilikuwa leo 13/12/2011 ambapo mbunge huyo wa wawi - Pemba alikuwa na ziara nyingine katika tawi la CHECHNIA lililoko kata ya mabibo. Baada ya walinzi wa taifa na wa wilaya kuzuia shughuli ya KOSOVO inaonekana hamad rashid na wenzie walijipanga zaidi na kukodi kundi kubwa la vijana wapatao 150 ili kulinda mkutano wake wa mabibo. Majira ya saa 8.00 mchana vijana kadhaa walianza kufika ukumbi wa mkutano wengine wakiwa na makoti na wengine wakiwa na kofia za mazoezi maarufu PAMA. Wengi wa vijana hao walionekana kuwa na nyuso nzito na baadhi yao walionekana kama wamepata kilaji kidogo.
Majira ya saa 9.00 walifika hapo ukumbini(ukumbi wa kukodi) wajumbe watatu wa baraza kuu la uongozi la CUF wakiambatana na baadhi ya wanachama wanaompinga MAALIM SEIF. Walipofika ukumbini wanachama na wananchi mbalimbali walianza kukusanyika. Wakati kusanyiko linaendelea ghafla gari ya ofisi kuu ya CUF ikapaki mita 100 hivi kutoka ukumbini. Baadaye walishuka walinzi wawili wa wilaya ya kinondoni na kwenda kwenye mlango wa ukumbi kuuliza kulikoni kikao hicho kifanyike bila wilaya kupewa taarifa?
Sijakuelewa.....tarehe 13/12/2011 saa 8 au 9 mchana bado haijafika! Na stori yako hii unaelezea kitu ambacho kimeshatokea...
Kama sikosei huyu Hamad Rashid aliwahi kuhojiwa na vyombo vya habari kuhusu ndoa yao na CCM kwamba hawaoni inauwa upinzani? nakumbuka jibu lake lilikuwa ni hili " Hatuwezi kuwaachia nguruwe shamba wale peke yao, ni lazima tule wote" mwisho wa kunukuru.
Inaonekana Hamad Rashid yeye amezaliwa ili awe mtu wa madaraka na ulaji tu maisha yake yote, kwa sababu ninavyofahamu mimi ukiongoza mageuzi ndani ya chama basi wewe usiwe mmoja wa wale frontliner, hapa ndipo alipoishiwa busara huyu Hamad Rashid, nadhani wangeongoza harakati hizi wengine halafu wangempendekeza yeye hiyo ingeingia akilini kidogo.