Hamad kufikishwa kamati ya maadili ya CUF, asema Mtatiro

Hamad kufikishwa kamati ya maadili ya CUF, asema Mtatiro

Kwanini usiende ccm ukaungane na lowassa wako kumsaida kutimiza ndoto yako na yake? rejea hii "Edward Ngoyai Lowassa for ccm chairman-2012",wewe kama sio ccm magamba mawili yaliyobaki basi utakua unalipwa pesa nyingi sana lowassa kwa debe hili zito unalompigia,siamini kama great thinker kama wewe unaweza kuingia gharama hivi hivi tu kupromote project ya mtu mwingine katika chama kingine tofauti na chama chako!huo ni uongo...ni sawa sawa kumkuta mtu kavaa t shirt na kapelo za ccm zimeandikwa lowassa for ccm chairman halafu mtu huyo akajifanya sio ccm!hii sio kweli,na hili ni tatizo,upinzani bongo unashidwa kusonga mbele kutokana na kuwa na mamluki kama wewe!
Pole sana ni wengi wenye mtazamo kama wako, kifupi mimi huwa sitawaliwi na itikadi naangalia haki inapotakiwa itendeke, haki ya mtu haiangalii wewe ni CCM ,Chadema, wala CUF.

Kama EL ataonewa nitasema kama Zitto atatetereka nasema kama ninavyosema leo kwa HR, kwa ninavyoifahamu CUF it is just a matter of time HR atakuwa nje ya ulingo. Kuhusu mimi kulipwa for your information EL huwa namuona tu kwenye TV lakini nilimkubali kwenye utendaji wake wakati akiwa PM kwa muda mfupi akaanzisha na kuisimamia project ambayo hadi leo inajulikana kama shule za kata, kifupi alithubutu.
 
Katika taarifa ya TBC saa mbili leo mtatiro anasema Hamad Rashidi amesaliti chama. Wanajamii nataka kujua amekisaliti chama kwa vipi? Mapanga waliyokatana wana CUF pia yameonekana.
 
nakuheshimu kama mpiganaji wa ukweli saaana ila kwa hili mkuu umepotoka
Sijapotoka Nyakageni, naomba kafanye homework ili umjue HR ni nani, kinachomsumbua ni tamaa ya madaraka hana lolote, kama angekuwa na busara wala asingeutaka ukatibu kwa njia anayotumia(fujo). Kwa hiyo akija CDM (sina uhakika kama ana gutz hizo) atakuja kuvuruga hata mafanikio madogo yaliyopatikana, kama ni mzigo wa Shibuda unatutosha.
 
Sijapotoka Nyakageni, naombia kafanye homework ili umjue HR ni nani, kinachomsumbua ni tamaa ya madaraka hana lolote, kama angekuwa na busara wala asingeutaka ukatibu kwa njia anayotumia(fujo). Kwa hiyo akija CDM (sina uhakika kama ana gutz hizo) atakuja kuvuruga hata mafanikio madogo yaliyopatikana, kama ni mzigo wa Shibuda unatutosha.

Huyu HR kuna mambo mengi ya ukweli amesema kuhusu Seif..lakini utaratibu anaoutumia kupata madaraka ni mbaya sana..kwa level yake na umri wake..

Angeweza kupata uenyekiti wa chama au ukatibu mkuu lakini si kwa kuanza kuvuruga chama kwanza ndio upate madaraka ..hilo litamgharimu sana..

hataondoka CUF, watanyamazishwa kwa sasa somwehere in future watajiondokea wenyewe kwasababu hawatawezi kupenya tena..
 
Laana ya unafiki itawatafuna hawa CCM b mpaka tone la mwisho.Sitosahau hotuba ya hamad rashid na habib mnyaa waliyotoa bungeni wakati wa kujadili mswada wa katiba,jinsi walivyoilaani chadema na kuonyesha ubaguzi wa waziwazi kwa watu wa Tanzania bara.Hii dhambi itawala mpaka wamalizane wote.

umeona eee. Mwisho wa ubaya ni aibu tupu. Mi ile siku machozi yalinitoka. Machozi yetu hayatamwigika bure.
 
Nafikiri itakuwa busara kwa CCM-B kuvunja hiyo kambi na kurudi kwenye kundi la awali CCM-A
 
Tumewashauri sana kuhusu uendeshaji wao wa siasa lakini CUF hawashauriki.Hayo ndiyo matokeo yake.Namshauri Hamad Rashid aendelee kusambaza kijitabu chake cha YALIYOJIRI ili watu wazidi kuifahamu CUF kwa undani.
 
Si bora angesaliti tu Chama Chake Cha CUF, huyu ni msaliti mkubwa wa kila azma n jema lolote kwa wananchi wa kawaida kote Bara na Visiwani. Sitaki hata kusikia habari zake, bure kabisa na wala hakuna pale!!!!!
 
Huyu HR kuna mambo mengi ya ukweli amesema kuhusu Seif..lakini utaratibu anaoutumia kupata madaraka ni mbaya sana..kwa level yake na umri wake..

Angeweza kupata uenyekiti wa chama au ukatibu mkuu lakini si kwa kuanza kuvuruga chama kwanza ndio upate madaraka ..hilo litamgharimu sana..

hataondoka CUF, watanyamazishwa kwa sasa somwehere in future watajiondokea wenyewe kwasababu hawatawezi kupenya tena..
It is true HR anaweza kuwa na point na labda za kweli kuwa chama kimekufa hasa huku bara, lakini ni njia ipi itumike kumpunguzia Seif kazi anahitaji busara kidogo, bare in mind Seif alikoitoa CUF hadi leo kwa hiyo si busara hata haki kumbeza leave alone kumtoa kwa nguvu. Ninachoshauri HR akae na viongozi wenzake ajaribu kuwa-convince ni kwa nini anataka kuwa katibu mkuu aeleze ana sifa gani tofauti na alizonazo Seif. Najua swali hili huwa ni gumu sana kwenye interview nyingi, unaweza kufikiri una sababu lakini ukizi-present kwa wenzako zinaonekana si sababu.
 
eeeeeer wana jamvi huyu hamad si ndo yule mzee wa anti-chadema? hajakisaliti chama sema tu anataka ukatibu naye ale bata kama maalim, sasa maalim kashtukia dili la kupinduliwa so analinda kibarua chake...ikumbukwe kuwa maalim akichia ukatibu ikifika uchaguzi mwingine ndo kwisney yake, sasa kwa kuwa hamadi kaona mwenzake anakula vinono na yeye alikuwa anategemea mjengoni napo pameota mbawa ni bora aanze harakati ya kujitengenezea mazingira vizuri.... halafu hawa wote ni kama waarabu vileeeeee, so habari ya mapanga shaa na hata milipuko sidhani kama kwao ni ishu sanaaaaaaaa...ndo maana wamenza harakati ya kujaribu kuyatumia taratiiiibu
 
ndio maana daima nasema vyama vya upinzani Tanzania viko kimaslahi binafsi zaidi..! walianza NCCR sasa CUF.! Next time CDM..!

Mkuu next kitakuwa CCM, baada yakuwa chama Kikuu cha upinzani 2015!
 
this is going to be a very stiff, brutal and long drawn-out battle - lets keep watching
 
Binafsi nilikuwa namkubali sana Hamadi Rashid wakati akiwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni kabla CUF haijawa CCM B. Alikuwa anapanga hoja, mapigo ya chadema nahisi yanawasambaratisha na labda Hamadi anamawazo tofauti ya kuongoza chama ili kupambana na chadema lakini wenzake hawataki. Au ndio wanagombania madaraka? Kazi kwako ngoja tusubiri kamati ya maadili itakavyo amua. Wakiteleza kidogo tu CUF inapoteza mwelekeo.
 
Back
Top Bottom