Hama hama ya Wapinzani na matokeo yake

MakaDik

JF-Expert Member
May 31, 2019
238
134
Waliohama Toka Vyama Pinzani kwenda CCM na Wameshindwa Kura Za Maoni. Je, Hii Ni Ishara Kwamba Tulipodhani Wananunuliwa Na Kwamba Waliahidiwa Kitu Ilikuwa Dhana Potofu? Au Tusubirie Teuzi Zingine

Uchaguzi Uliopita Kulikuwa Na Usemi Huu "bora Kusimamisha Jiwe Kupitia Upinzani Kuliko Kumsimamisha Mtu Wa CCM" Na Sehemu Nyingi Walifaulu!

Je, Waliohama Ndiyo Mawe Yale Yaliyokosa Mwelekeo Yakasukumiwa Upande Mwingine ambako leo Yamepigwa Nyundo Ya Kushindwa Na Kubaki Kutoa Machozi Ya Vumbi Kwa Kuwa Walikurupuka? Nini Ni Nini?

Nashindwa Kupata Majibu.
 
Wamepata walichokistahili ni watu ambao hawana misimamo bali ni watu wanaopenda madaraka hao watu nadhani kuna chakujifunza hapa kwa waliyowakuta.
 
Chezea Wajumbe wewe!! wanafyeka bila kujua uliahidiwa tam tam.... daaaaadeeeki
 
Wamepata walichokistahili ni watu ambao hawana misimamo bali ni watu wanaopenda madaraka hao watu nadhani kuna chakujifunza hapa kwa waliyowakuta.
Ni Kweli Huu Ndio Mshahara Wao Na Ni Elimu Kwa Sisi Wengine
 
Labda mwenye Chama awarudisheee...!! Ila wajumbe aisee wanataka pesaaa alafu ukiwapaa wanakupiga za usoo piaa
 
Hao
tapatalk_1595659759521.jpeg
 
Huo mnada wa kununuliwa wajumbe hawakushirikishwa. Tajiri alienda tu kununua bila kujua kuwa mchungi ndo anajua palo na malisho. Kimbembe ni walionunulika walipokuja gundua kuwa wanaojua malishoni ni wengine na huwapeleka wenye chapa zao. CCM sio kadi bali ni ukada wa kuzaliwa
 
Mie namuwaza yule aliyesababisha mrembo Akwilina akauawa, kisha akasababisha wenzie waliompa Ubunge kufungwa na kutozwa mamilioni ya shilingi. laana iwe nae daima
 
Kushindwa kura za maoni haimaanishi hukununuliwa.


Ulinunuliwa na viongozi wa juu ila kura zinapigwa na wajumbe wengi walidhani watapitishwa na viongozi waliowanunua
 
Back
Top Bottom