Hama hama ya wanasiasa ni uzalendo,usaliti au kukua kwa demokrasia?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
34,671
40,918
Sasa tupo kwenye kupatwa kwa siasa zetu za vyama vingi kwa hama hama ya wanasiasa wetu.

Tafsiri zipo nyingi ila hizi Chache zimebeba mawazo ya wengi;

1. Kukua kwa demokrasia.

WaPo wanaosema demokrasia yetu imekua kwani watu WaPo kwenda watakako wakati wowote.

2. Uzalendo.

Kwa ajili ya mapenzi makubwa kwa nchi Yao wanaona ni Vyema kuungana na fungu lililo jema.

3. Usaliti.

Kukana imani zao za awali pamoja na wale walioweka matumaini kwao inaonekana kama usaliti.

Je lipi hasa Kati ya hayo matatu limebeba tafsiri sahihi ya hama hama za viongozi na wanasiasa?
 
Ni ubora duni wa wanasiasa pamoja na mpangilio hovyo wa vyama vyetu. CCM ina mtindo ambao uliigwa na vyama vingine. Yaani ukiwa Mkiti basi wewe ni yote. Unafuta na kuingiza watu wapya upendavyo. Kwa CCM labda tusema ni uraibu wa chama Kimoja, sasa CDM, UDP, TLP imekuwaje nao wanakuwa na abosolute power kwa wengine?

Namkumbuka Cheyo akisema, ".... Jidulamabambasi, OUT!" Akifukuza wanachama kama wapangaji wake. Leo hii Mbowe anatuhumiwa wizi/matumizi hovyo ya chama na mali zake, yeye kimya! Haoni sababu ya kujibu kwa kuamini ni chama chake, yeye ni supreme. Lipumba anaachisha watu uanachama, watu kimya na wengine wanalazimika kujikomba ili awapende.

Swali ni je, Tuendelee kulea wanasiasa kwa kodi zetu wakati ubora wao ni duni kiasi hiki?
 
Biashara zaidi.
Huwezi sema usaliti maana hakuna walichokuwa wanasimamia walienda na vibes kama sasa.
Uzalendo hapa hakuna kabisa. Sidhani kama hata kabla wamewatendea haki wananchi walowapa kura zao katika uongozi wao.
Demokrasia kwa heri.
 
Ni ubora duni wa wanasiasa pamoja na mpangilio hovyo wa vyama vyetu. CCM ina mtindo ambao uliigwa na vyama vingine. Yaani ukiwa Mkiti basi wewe ni yote. Unafuta na kuingiza watu wapya upendavyo. Kwa CCM labda tusema ni uraibu wa chama Kimoja, sasa CDM, UDP, TLP imekuwaje nao wanakuwa na abosolute power kwa wengine?

Namkumbuka Cheyo akisema, ".... Jidulamabambasi, OUT!" Akifukuza wanachama kama wapangaji wake. Leo hii Mbowe anatuhumiwa wizi/matumizi hovyo ya chama na mali zake, yeye kimya! Haoni sababu ya kujibu kwa kuamini ni chama chake, yeye ni supreme. Lipumba anaachisha watu uanachama, watu kimya na wengine wanalazimika kujikomba ili awapende.

Swali ni je, Tuendelee kulea wanasiasa kwa kodi zetu wakati ubora wao ni duni kiasi hiki?
Lakini mkuu hao si ndio walikuwa wakiitwa majembe huko walipo? Huo udhaifu wao umeanza kuonekana Leo?
 
Kwani wanaohama ni ccm?
Pungz kuwashwawashwa
Ccm ndio inafanya manunuzi.. inatumia mabilioni ya pesa za wavuja jasho kununua wapinzani then wanaitisha uchaguzi uchwara huku wakitumia vyombo vya dola kuhakikisha wanashinda!
 
Lakini mkuu hao si ndio walikuwa wakiitwa majembe huko walipo? Huo udhaifu wao umeanza kuonekana Leo?
Wakati mwingine unahitaji muda ili kugundua upumbavu na udhaifu wa mtu. We now see the stupidity in these parochials who pose to gain a national status.
 
Wanaohama mpaka sasa hawajatuambia lolote kuhusiana na CCM kufanya lolote.
Unataka waseme nini wakati wameshapewa Mlungula na kuhakikishiwa nafasi yao ya ubunge iko pale pale. We hujiulizi kwanini wakihamia ccm wanapitishwa kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani bila kura za maoni?! Na isitoshe kwenye chaguzi ccm inatumia vyombo vya dola kulazimisha ushindi
 
Wapemba hamtawasikia kwenye hama hama. Wao hawategemei ajira na vyeo vya serikali
 
Wakati mwingine unahitaji muda ili kugundua upumbavu na udhaifu wa mtu. We now see the stupidity in these parochials who pose to gain a national status.
Kwa maana kwamba vyama husika ni dhaifu mpaka kuruhusu watu dhaifu wanakuja baadae kuonekana kuwa dhaifu na kuzidi kukishoofisha chama
 
Unataka waseme nini wakati wameshapewa Mlungula na kuhakikishiwa nafasi yao ya ubunge iko pale pale. We hujiulizi kwanini wakihamia ccm wanapitishwa kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani bila kura za maoni?! Na isitoshe kwenye chaguzi ccm inatumia vyombo vya dola kulazimisha ushindi
Mkuu hoja zako nyingi msingi wake ni hisia tu;

Katibu Mkuu wa CCM anasema kinachotumika ni busara zaidi Katika kuwapa waliohama kutetea nafasi zao za awali hayo mengine ni siasa tu za waliopoteza
 
Hakuna hata moja kati ya hayo. Umaskini una dimensions nyingi na miongoni mwao ndio hizo. Kinachoendelea ni indicator ya umasikini wetu tulionao tu pamoja na vyama kutokuwa na itikadi zinazofahamika. Lakini kubwa kuliko yote ni kutoeleweka kwa dhana ya vyama vingi na demokrasia.

Waafrika tunachelewa sana kuelewa mambo muhimu. Inaweza kupita miaka 200 ijayo ndipo tutajua maana na umuhimu wa democrasia na mfumo wa vyama vingi. Kwa sasa tunaona kama ni jambo tulioletewa tu. Sawa na miradi inayopelekwa vijijini, inakufa baada ya muda mfupi kwasababu hawaamini na wanaona kama wameletewa tu.
 
Mkuu hoja zako nyingi msingi wake ni hisia tu;

Katibu Mkuu wa CCM anasema kinachotumika ni busara zaidi Katika kuwapa waliohama kutetea nafasi zao za awali hayo mengine ni siasa tu za waliopoteza
Ukweli halisi unaujua sema ndio hivyo wewe na huyo msomi uchwara bashiriu mmeamua kujitoa ufahamu
 
Back
Top Bottom