Halotel wananiibia data zangu

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,663
Kuanzia jana usiku mpaka leo nimeweka Mb 500 mara tatu kitu ambacho si cha kawaida maana sina matumizi ya kiasi hicho mwanzoni Mb 500 zilikuwa zinakaa mpaka siku tatu. Sasa sahiv ndo hatari zaidi maana nimeweka mb 500 hata nusu saa haijaisha tayari salio linaonesha ni Mb 170 zimebaki.

Hapo hapo nimeenda kwenye settings za simu wananiambia kuanzia tareh 24 May yaani jana usiku mpaka sasa data zilizotumika ni Mb 504 sasa nikipiga mahesabu hapa Mb kama 1000 zimepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Yaani nimeibiwa mchana kweupe Sh 1000 nzima ndani ya masaa machache. Hawa jamaa ni wezi wa kutisha. Sasa sijui naenda kudai wapi. Kwanini wanafanya hivi lakini? Regulators wapo wapi? Watu wanajiamulia tu saa yoyote kufanya wanachotaka.
 
Mkuu nawe waibie aisee maana hukuna jinsi. Jinsi gani sijui maana malalamiko ya watu kuibiwa na mitandao ya simu ni mengi ila mnyonge hana kimbilio tena ila yeye aibe sasa sheria ya mtandao inavaa suti na tai.
 
Kuanzia jana usiku mpaka leo nimeweka Mb 500 mara tatu kitu ambacho si cha kawaida maana sina matumizi ya kiasi hicho mwanzoni Mb 500 zilikuwa zinakaa mpaka siku tatu. Sasa sahiv ndo hatari zaidi maana nimeweka mb 500 hata nusu saa haijaisha tayari salio linaonesha ni Mb 170 zimebaki.

Hapo hapo nimeenda kwenye settings za simu wananiambia kuanzia tareh 24 May yaani jana usiku mpaka sasa data zilizotumika ni Mb 504 sasa nikipiga mahesabu hapa Mb kama 1000 zimepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Yaani nimeibiwa mchana kweupe Sh 1000 nzima ndani ya masaa machache. Hawa jamaa ni wezi wa kutisha. Sasa sijui naenda kudai wapi. Kwanini wanafanya hivi lakini? Regulators wapo wapi? Watu wanajiamulia tu saa yoyote kufanya wanachotaka.
Hata Mimi nimenunua mb1000 Jana usiku SAA tano kufika ahsubuhi sina mb
 
Inawezekana labda ni update zimefanyikwa kwenye programu, hizi zinatumia sana data
au kama uliacha wi-fi hotspot on bila password watu wakajiunga wakatumia
 
MB ZA 500 ZINAKAA HADI SIKU TATU? NIPE MAUTUNDU ULIKUWA UNAFANYAJE FANYAJE
 
nlijua kwangu tu aise nkazani live update au nn nikaondoa zote lakini wapi
 
Nadhani ndio umenunua line ya Halotel karibuni na bado ujaizoea.

Ata mimi ilinitokea nilivyonunua line ya Halotel mwaka jana mwezi wa 11 lakini baada ya kuibiwa kwa takribani week 2 mambi yalitulia nikanza kutumia MB 500 mpaka siku 3 .

Kubali kuibiwa lakini ufurahie speed ya internet
 
eka firewall au app yoyote inayopima matumizi ya data halafu ichunguze, mara nyingi watu wanaolalamika wanaibiwa data wanakuwa na matumizi ya chini chini ambayo wao hawayajui
 
Nikweli chief wengi huwa hawajui hicho kitu, mtu anaishia kusema kaibiwa kumbe kuna app zinatumia mb bila yeye kujua.
 
Ulidhani wewe ni mjanja kuliko hawa Wacambodia..umejisajili kama mwanafunzi kiujanjaujanja ili upate MB 500 kwa wiki..jamaa wamestuka na wamejua wewe ni mfanyabiashara sa nyanya chungu na bamia soko la Tandale...then wamelipiza.

Tulio zoea jiji tunasema ngoma droo. Ahahs
 
Kuanzia jana usiku mpaka leo nimeweka Mb 500 mara tatu kitu ambacho si cha kawaida maana sina matumizi ya kiasi hicho mwanzoni Mb 500 zilikuwa zinakaa mpaka siku tatu. Sasa sahiv ndo hatari zaidi maana nimeweka mb 500 hata nusu saa haijaisha tayari salio linaonesha ni Mb 170 zimebaki.

Hapo hapo nimeenda kwenye settings za simu wananiambia kuanzia tareh 24 May yaani jana usiku mpaka sasa data zilizotumika ni Mb 504 sasa nikipiga mahesabu hapa Mb kama 1000 zimepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Yaani nimeibiwa mchana kweupe Sh 1000 nzima ndani ya masaa machache. Hawa jamaa ni wezi wa kutisha. Sasa sijui naenda kudai wapi. Kwanini wanafanya hivi lakini? Regulators wapo wapi? Watu wanajiamulia tu saa yoyote kufanya wanachotaka.
Itakuwa kweli maana hata kwangu zinaenda kichiz
 
Back
Top Bottom