Ukiomba mkopo Halotel kwa ajili ya dharura muda wa maongezi majibu utakayojibiwa utatamani uhame mtandao saa ile ile.
Jibu lao alieliandaa nadhani ni MWEHU wa akili kwa sababu unaambiwa utapata mkopo endapo laini yako iko matumizini kwa zaidi ya miezi 3 wakati laini ina zaidi ya miaka 3 na zaidi. Pia unaambiwa huwezi kupata mkopo mpaka uwe una salio lisilozidi kiasi fulani cha pesa.
Sasa kama nina salio kwa nini niombe mkopo?
Tunawaomba Halotel watoe hiyo lugha chafu inayonuka uvundo wa dharau ya hali juu.
Bora wewe mkopo, mie nilijiunga kifurushi nikakatwa pesa halopesa ila kifurushi hakikuungwa. Nikawapigia, kwanza kuwapata tu ni issue unapiga hadi unatamani kughairi, linakuja kupokea likaka linaongea kama nimemchukulia mume. Nilichukia na simu nikakata.
Ungepewa huo Mkopo ungekuja Kuwasema (Kuwasiliba) hapa JamiiForums? Watanzania ni watu wanafiki na Nongwa mno. Ndiyo maana Ukanyimwa hata huo Mkopo wenyewe.
Mimi siwataki hata kuwasikia hawa kenge, yaani nimefanya muamala, lakini nawapigia wananiambia nisubiri masaa 24, daah, yaani nimeshindwa kuangalia hata mpira