Halotel wana chuma ulete saa hii. Nihamie wapi wakuu?

Halotel wana chuma ulete saa hii. Nihamie wapi wakuu?

Huu ni km uzi wa 5 nausoma kuhusu Halotel. Duh! Haya mambo ndiyo yalinifanya niache kununua vocha za tigo.
Kwa line lbda airtel wanavifurush vya bei nafuu na inategemeana na speed yake inategemea na maeneo. Sehemu zingine speed ya jet na sehemu nyingine ya kobe
 
Hawa smart hawana internet maana kipya kinyemi just as walivyokuja halotel ili tuhamie
 
Airtel wako sawa kwa 1000 unapata gb 2 ambazo zitaisha mbele ya macho yako, dk 100 airtel kwa airtel na dk 10 mitandao yote, hakuna wizi hapo.

Ila kuna maeneo ukikaa speed ya net hairidhishi sana.
 
Nimenunua kifurushi cha wiki chenye mb 1200 lakini zimeisha ndani ya nusu saa tena nimeingia jamii forums tu basi. Halafu huduma kwa wateja kuwapata ni ishu kweli kweli.
 
Airtel wako sawa kwa 1000 unapata gb 2 ambazo zitaisha mbele ya macho yako, dk 100 airtel kwa airtel na dk 10 mitandao yote, hakuna wizi hapo.

Ila kuna maeneo ukikaa speed ya net hairidhishi sana.
unatumia siku ngapi
 
Kwa kweli hamna mtandao wenye speed nzuri km halotel kati ya mitandao niliyowahi kuitumia
Tatizo halotel wamekua wezi siku hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
Vibaka kabisa wanatuchezea shere kwenye mb. Unajiona umepewa 1.2gb kwenye meter yao ila nadhani wanatoa less than that. Maybe hata mb700 tu halafu mbaya ukijiloga ku stream tu kwa youtube umekwisha.
 
Airtel wako sawa kwa 1000 unapata gb 2 ambazo zitaisha mbele ya macho yako, dk 100 airtel kwa airtel na dk 10 mitandao yote, hakuna wizi hapo.

Ila kuna maeneo ukikaa speed ya net hairidhishi sana.
Hiko cha buku 2 ni cha siku ngapi, mi nimesajili airtel juzi wapo vizuri bundle haliendi chap chap ila speed ndogo tofauti na halotel hata whatsapp call imenizingua sana. Napigaga sana Denmark ila airtel ina reconnect kila saa!
 
Kweli kabsa niwez nilijua labda matumiz yngu kumbe wananiibia

Sent using Jamii Forums mobile app
Wanaiba sana MB yani. Nadhani wanatoa MB kidogo halafu tunadanganywa ni 1.2GB zinayoyoma ndani ya siku mbili tu huna kitu unaambiwa umebakiza MB 5 mara wanakukatia huduma. Halotel ni weziiiiiiii mbayaaaa!!!!
 
Back
Top Bottom