Binafsi nilikuwa mtumiaji mzuri wa mtandao wa Tigo, baada ya kuona wanazingua nikahamia voda nao pia nikawahama baada ya kupandisha vifurushi vyao na kuanza kunyonya mb km wananyonya maziwa, baada ya voda nikahamia halotel ambayo niliona ni wakombozi halisi kwani vifurushi vyao ni affordable lkn pia MB hazikimbii km ilivyo Tigo na Voda.
Tatizo limeanza
Majuzi nilijiunga kifurushi wakanipa GB 1, sija download chochote chenye ukubwa wa kushangaza km kawaida yng, lkn nimekuja kuta mb zimeisha, yn nimeingia Jf tu mb kwisha, na kilichonipa wasi wasi ni pale nilicheki salio, mara ya kwanza nimecheki nikakuta mb 146 nikashangaa ckuamini, kucheki tena nkakuta 110, nkacheki tena ikabaki 0 baadaye nacheki imerudi 94.
Unaweza ukaona hapo wizi wenyewe ulivyo, mtu anaweza akasema ni matumizi yng lkn ukweli ni kwamba mpk nalalamika it means kuna mchezo mchafu wameuanza, jana ucku nimejiunga GB1 hapa nnavyoongea zishabaki mb300, na hakuna vurugu zozote kubwa nimefanya, nmewapigia wananiambia niangalie data usage, ss najiuliza hiyo data usage nani kabadilisha, wkt cm yng mda mwingi ninayo mm mwenyewe. Naomba wakuu mnijuze tatizo hili ni mm tu au na nyie limewakumba.