Kuchwizzy
JF-Expert Member
- Oct 1, 2019
- 1,072
- 2,306
Kuna hii kasumba ambayo watumiaji wengi wa Internet,haswa sisi wa Tanzania tunayo.Aidha tuna amini hivi au tumeshawahi kusikia kutoka kwa watu na sisi tukawaamini bila kutafiti
Na cha ajabu huwa na bishana na watu wengi sana kuhusu hili swali nikiwa najaribu kuwaelewesha
So baada ya kupitia baadhi ya nyuzi kadhaa humu Jukwaani nikaona pia kuna baadhi ya wana JF wengi tu pia tunaamini hivyo
Kuwa Tovuti au Applications kama Facebook,google,instagram,youtube,jamiiforums etc kwa kiasi fulani zinaingiza pesa kwa kutumia MB zetu
Au kwa namna fulani hivi zinabadili MB tunazozitumia kuwa Pesa
Ukweli ni kwamba,hakuna tovuti au App inayoingiza hata TSH 1 kupitia MB zako,
Tovuti au Apps karibia zote ni free,ikiwa na maana ya kuwa hakuna gharama yoyote utakayo itoa ku access hio tovuti
Kwanzia facebook,google,tiktok au tovuti na app yoyote unayoitumia
So swali litakalokuja kwako ni,kama hizi tovuti zote nazitumia bure,zenyewe zinaingiza vipi pesa?
Fun fact: Mark Zuckerberg mwanzilishi na mkurugenzi wa Facebook Inc anautajiri wa dola za kimarekani Billion 122.9,Larry mwanzilishi mwenza wa google ana utajiri
wa Billion 100.2 dola za kimarekani
Kivipi wanaingiza pesa wakati tovuti na App zao ni bure nitalijibu mwisho kwa maelezo mepesi zaidi,ila kina nani wananufaika kupitia MB zetu nalijibu hapa
Internet ina furahisha,wengi tunai-take for granted(tunaichukulia juu juu),lakini kuna organizations zinazofanya kazi usiku na machana kuhakikisha Internet ipo na inapatikana kwa
watu wote
Japo kuwa hakuna anayemiliki Internet,(waanzilishi wake walitupa for free) lakini organizations hizi kwa namna fulani inabidi zilipwe kwa kazi zinazofanya
Moja kati ya Organizations hizo ni ISP ( Internet Service Providers),
ISP kazi yake kubwa ni kukupa uwezo wa wewe kama mtu wa kawaida ambaye huna miundombinu yoyote inayotakiwa kukuunganisha wewe na Internet kupata internet
So ISP wanakupa access ya internet kupitia vifurushi,kama UNIT za LUKU zinazoisha kulingana na matumizi yako
Tofauti kwenye vifurushi vya internet,hatutumii UNIT kama kipimo,tunatumia Bit
Bit ni kiasi kidogo cha data/taarifa ambacho kinaweza kuhifadhiwa na Computer yako (Laptop,Desktop,Smartphone zote ni computer)
Taarifa inaweza kuwa chochote,kwanzia herefu,neno,maneno,picha,video,sauti,namba hata nukta pia inachukua kiasi cha bit kwenye computer
8 bits =1 Byte(B)
I Mega Byte(MB) = 1,000,000 Bytes(B)
Kwakua ISP(Mfano Halotel, Vodacom, Tigo etc) wana miundombinu inayohitaji gharama kui manage,ndipo tunapopaswa kuwalipa kwa kununua vifurushi vyao
ISP ndio wanufaika halisi wa MB zako
So ISP anapokupa 500 MB kwa mfano,maana yake unaweza kupakua/download taarifa zenye ukubwa wa bits billions 4,
Taarifa unazo pakua zikizidi hiko kiasi,ndio pale unapowaona Halotel wezi
Turudi kwenye swali letu la pili,tovuti na apps kama Facebook zinaingiza vipi pesa?
Sio pesa tu,Ma-Trillions ya pesa?
Kupitia Matangazo,tuseme wewe ni mpenzi wa viatu,pia ni mwanaume kwenye account yako ya Facebook au Instagram unapenda ku like content au picha zinazo husiana na viatu
Unaperuzi tovuti zinazohusiana na viatu,at the same time upo logged in Facebook
Katika huo mtiririko wote huo,Facebook wanataarifa muhimu kuhusu mapenzi yako kwa viatu
Kilometa kadhaa kutoka ulipo,kuna muuzaji wa viatu vya kiume,anataka wateja zaidi
So anaamua kutangaza bidhaa zake Facebook,Facebook wanachohitaji kutoka kwake ni aina ya bidhaa anazouza
Kazi ya kutangaza bidhaa zake anaiachia Facebook kwa kuilipa kiasi kadhaa cha pesa
Kwa kua Facebook tayari inawafahamu watumiaji wake kama wewe,inachofanya ni ku onyesha hio Post kwako,kama Sponsored Post
Kwa kua tayari una interest na viatu,kuna chance kubwa uta click hio post...na hapo Facebook ndio inapoingiza Cash
Kwa ushauri kuhusu Tech,Website,Apps, na digital marketing nicheki 0748333586
By the way unaweza vipi kuongea kwa kujiamini mbele ya hizo Camera bila ku sound kama Robot?