Halotel mmeanza kuiba MB zetu

Halotel mmeanza kuiba MB zetu

The best 007

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2019
Posts
42,480
Reaction score
98,527
Binafsi nilikuwa mtumiaji mzuri wa mtandao wa Tigo, baada ya kuona wanazingua nikahamia voda nao pia nikawahama baada ya kupandisha vifurushi vyao na kuanza kunyonya mb km wananyonya maziwa, baada ya voda nikahamia halotel ambayo niliona ni wakombozi halisi kwani vifurushi vyao ni affordable lkn pia MB hazikimbii km ilivyo Tigo na Voda.

Tatizo limeanza

Majuzi nilijiunga kifurushi wakanipa GB 1, sija download chochote chenye ukubwa wa kushangaza kama kawaida yangu, lkn nimekuja kuta mb zimeisha, yaani nimeingia Jf tu mb kwisha, na kilichonipa wasi wasi ni pale nilicheki salio, mara ya kwanza nimecheki nikakuta mb 146 nikashangaa sikuamini, kucheki tena nikakuta 110, nikacheki tena ikabaki 0 baadaye nacheki imerudi 94.

Unaweza ukaona hapo wizi wenyewe ulivyo, mtu anaweza akasema ni matumizi yangu lkn ukweli ni kwamba mpaka nalalamika it means kuna mchezo mchafu wameuanza, jana usiku nimejiunga GB1 hapa nnavyoongea zishabaki mb300, na hakuna vurugu zozote kubwa nimefanya, nmewapigia wananiambia niangalie data usage, sasa najiuliza hiyo data usage nani kabadilisha, wkt cm yangu muda mwingi ninayo mimi mwenyewe. Naomba wakuu mnijuze tatizo hili ni mimi tu au na nyie limewakumba.
 
Angalia flow ya MB yn ilikuwa 146 ikashuka 110 af ikapanda 116
Screenshot_2020-05-22-09-03-30.jpeg
Screenshot_2020-05-22-09-03-19.jpeg
Screenshot_2020-05-21-23-30-01.jpeg
 
kifurushi cha mega bando halopesa kimetulia.
alafu akibadili laini kutoka 3g kwenda 4g mb zinatembea kinyama yani.
ila yote kwa yote bongo tuna nafuu sana ya mawasiliano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha kwa TTCL imekufa au bado ipo?! Kuweni "wazarendo" kama uzalendo umewashinda acheni kulialia.
 
Mzee kama uli share net kupotia pc usiende moja kwa moja kutoa lawama kwa halotel

Juzi nilikua na cheki movie ambayo niliipakua usiku, kwa bahati mbaya haikua na subtitle halafu official lugha ya hiyo movie ni spanish. Nikajiunga bundle la buku nikapata GB1 nika download complete subtitles ya series yote ambazo zili cost MB chini ya 2.

Wakati nimemaliza kupakua hizo subtitles nikaendelea kucheki movie zangu ambazo zishakua downloaded, nikasahau kuzima data, movie hata katikati haijafika nikastukizwa ndugu mteja umebakiwa na MB 20
 
HALOTEL ,ni wahuni sana, namwelewa mtoa mada, mimi walikunywa mb zangu bila kuingia youtube nilisoma magazeti, nikaingia JF Gb 1 ikaishia hapo, nikaweka tena kwa matumizi yaleyale ikaisha kama mwanzo.Nikawapigia wa kwanza akaniambia nizime simu halafu niwashe mb zangu zitarudi hakuna kilichorudi,nikapiga tena akapokea mwingine aknieleza tofauti.Nikapiga tena sasa majibu yao ikawa ni matumizi yako ndio yamemaliza mb zako.
Nikahamia kwa muda nyumbani TTCL,nyumbani shida ni mtandao ndani ya jiji mtandao unakata kata.Nikarudi HALOTEL naona siku hizi wameacha kunywa mb zangu natumia kama zamani nimekuwa nao mwaka wa nne sasa.
 
Mm tatizo lilijitokeza juzi kati ila now fresh, ila gb 1 ya juzi wameinywa nikahisi wamechukua wafanyakazi wa tigo mana hao c mchezo,af u tube wala haili mb kiviile labda insta
 
Back
Top Bottom