mayowela
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 2,125
- 1,757
Moja kati ya biashara ambazo zinaenda kwa promotion bila kupumzika mwaka mzima ni Telecom, ikifuatiwa na makampuni ya Bia, na Mabenki. Haipiti miezi mitatu utaona promosheni za bidhaa kutoka Voda, Tigo na Airtel.
Hasa mtanange kubwa nauona kwa Tigo na Vodacom; huyu akija na hiki, yule naye analeta chake, basi soko linachangamka na sisi watumiaji tunafaidikia na kurahisishiwa huduma mbalimbali.
Sasa hawa Wavietnam Halotel ni muda sasa, miezi kama miwili sikosei, sisikii matangazo yao redioni kwenye televisheni wala hawana bidhaa mpya sokoni, yaani hawana makelele kama wenzao ambao wako kwenye ushindani.
Maswali:

- Timu ya Marketing haina Mbinu/bidhaa ya kuinadi sokoni?
- Timu ya commercial wameishiwa mbinu/mikakati za kubuni bidhaa?
- Wameshindwa kuhimili soko la ushindani?
- Wanajihujumu wenyewe?