Halotel kunani?

Halotel kunani?

We ndo umemaliza, mwenye akili ajiongeze nini hitaji kubwa kwenye hizo parameters kwa sasa.
hitaji kubwa kwa sasa kwa wateja ni DATA & Mobile money na ndiko wanakopiga pesa wote na sio calls na sms,
kikla mtandao una maeneo yake ya kujidai, Kwa Kanda ya Pwani TIGO mbabe, ila ukiendsa Kanda ya Ziwa VODACOM ni mbabe, Airtel magharibi huko na kusini kidogo,

mimi swali langu Halotel hawana product yoyote wanayoinadi sokoni kwa sasa maana hata redioni hakuna matangazo yao tena...
 
Halotel ni mtandao wa kijambazi wanaiba bando.
Alafu saizi vifurushi vyao vinatembea kama vinasombwa na mafuriko.
Jana nimewapigia simu kulalamikia bando linavyotembea mwendo wa Hussein bolt wananiambia ngoja tumtafute mtaalamu wetu atakupigia tunachukua no.yako.
Mpaka leo hawajapiga.Hovyo sana siku hizi.
 
Mimi Jana nimenunua kifurushi cha 2000 2GB Lakini mpaka kinaisha ubao ulikuwa unasoma 888MB Kwenye kipimo cha internet.
 
Moja kati ya biashara ambazo zinaenda kwa promotion bila kupumzika mwaka mzima ni Telecom, ikifuatiwa na makampuni ya Bia, na Mabenki. Haipiti miezi mitatu utaona promosheni za bidhaa kutoka Voda, Tigo na Airtel.

Hasa mtanange kubwa nauona kwa Tigo na Vodacom; huyu akija na hiki, yule naye analeta chake, basi soko linachangamka na sisi watumiaji tunafaidikia na kurahisishiwa huduma mbalimbali.

Sasa hawa Wavietnam Halotel ni muda sasa, miezi kama miwili sikosei, sisikii matangazo yao redioni kwenye televisheni wala hawana bidhaa mpya sokoni, yaani hawana makelele kama wenzao ambao wako kwenye ushindani.

Maswali:
  1. Timu ya Marketing haina Mbinu/bidhaa ya kuinadi sokoni?
  2. Timu ya commercial wameishiwa mbinu/mikakati za kubuni bidhaa?
  3. Wameshindwa kuhimili soko la ushindani?
  4. Wanajihujumu wenyewe?
Hawa halotel na star time me nahis ni ndugu
 
Hao voda na tigo wanazo hela za kuchezea tens nyingi ni za wizi wanawaibia sana wateja wao, Voda wanaiba kwenye vifurushi vya internet na tigo kwenye vifurushi vya maongezi tena voda ndio wamezidi yani GB 1 Ya voda usishangae ni Massa ma 3tu imekata, Kidogo halotel wapo fair sana kwenye dakika za maongezi na internet GB 1 ya halotel unaweza maliza 24 hrs tena hapo ume angalia video youtube mpaka umechoka still unazo data za kutosha, Voda ni kinyume chake.HAWA WANATAKIWA WAPIGWE BAN MIEZI 6 FOR POOR SERVICE OPERATION
 
Kwa wizi wa vifurushi voda ni BABA LAO.
 
kampuni NAFUU ya simu za mkononi kwa kwa sasa nchini ni TTCL, iwe internet, kupiga , SMS, ukitaka kujiridhisha MTAFUTE MTU ANAYEMILIKI LAINI ya TTCL, usisikilize mtu anyekwambia kwa kudhania
😂😂😂 TTCL niupuuzi kwenye internet last week nilikuwa na shughulikia ishu fulani ya serikali wametumia network ya TTCL kwenye hiyo project yao yaan ni mzigo tupu aifai hata.
 
😂😂😂 TTCL niupuuzi kwenye internet last week nilikuwa na shughulikia ishu fulani ya serikali wametumia network ya TTCL kwenye hiyo project yao yaan ni mzigo tupu aifai hata.
mimi hata sasa hivi natumia internet ya TTCL , na kifurushi cha sh.2500 niliweka JUMAPILI leo JUMATANO
 
Back
Top Bottom