Halotel internet mnakera sana, mwogopeni Mungu

Halotel internet mnakera sana, mwogopeni Mungu

Labda Dar ndo inawasumbua kwa kweli, mi huniambii kitu kwa halotel, speed kama 4G naunganisha WiFi katika TV kutokea katika simu naangalia YouTube inakwenda kama nimeweka Deck haikwami hata nukta.

Mitandao kongwe kwangu ni kwa ajili ya kupokelea na kupiga tu, Data ni Halotel baaasi.
 
Bila shaka Halotel imeanza kupata jam.Binafsi nimeamua kurudi zangu tigo maana hamna namna nyingine
 
Ila tuwe wakweli, katika mitandao ya simu yote ni hovyo ila Halotel kuna uafadhari kidogo.

Ninatumia laini yao ya Chuo, Tsh 500 unapata Mb 600 kwa wiki, Tsh 1500 unapata MB 1220 dk 15 kupiga mitandao yote na dakika za kutosha kupiga Halotel kwa wiki.

Na kasi yao ipo vizuri hata kama itasoma 2G lakini bado utadownload vizuri tu bila shida.

Tofauti na mitandao mingine, Kasi ya 3/4G ni ya konokono ikibadili 2G ndio hudownload chochote na pengine isifunguke kabisa itabakia Loading....

Wengine wanasema Bundle zao zina wahi kuyeyuka, hii ni kwasababu ya kasi yao kubwa.

Sasa chagua uende ambako bundle haliwahi kuyeyuka na kasi yake ni ndogo na si ajabu mpaka muda wake unaisha haujatumia hata Mb 100 kati ya 500 ulizojiunga au uende ambako bundle linawahi kuyeyuka ila linaisha kihalali.
 
Halotel Zamani walikuwa wazuri sana ila sasa hivi wamejiunga na siasa MB 600 wanalamba sana hata usipopakuwa video humalizi masaa 3 hata kama unachat !!!
 
Kwakweli internet ya halotel ni janga, matatizo aliyohainisha mleta uzi ni kweli kabisa,
Mi natumia kwny simu lkn iko slow kinoma, labda kwakua ni Dar maana naona wa mikoani mnasifia halotel internet.
Kwa dar halotel inachagua maeneo ila ukipatia inaposhika speed yake ya 3G ni zaidi ya 4G kwa mitandao mingine yote, mi natumia line za mitandao yote nabadilisha kila wakati ila halotel kwa speed ya net wengine wanasubiri sana
 
Afub zina wahi sana kukata asee tofaut na matumiz yake
 
Halotel wako vizuri sana,kuliko hao wengine,ila kama wanakuzingua chukua hatua.
 
Hatamimi imeanza kunizingua ntahama sasahivi, otherwise labda kipindi cha mwanzo wateja walikuwa wachache now wameongezeka, they must do changes. Tutaondoka kweli.
 
Matatizo yako labda huku Mbeya, njombe, Ludewa had maporin huko halotel ndo kama mkomboz wetu popote kambi Halotel wapo vizuri sana
 
Kusema ukweli net strength ya halotel imeshuka kinoumaaaaa.
 
Back
Top Bottom