Halmashauri zinazoongozwa na CCM zaongoza kwa ubadhirifu

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Nimesoma gazeti Mwananchi kuhusu Ufisadi wa kutisha Serikalini. Pamoja na ufisadi huo, Halmashauri za Wilaya za Sengerema, Ludewa, Moshi, Kishapu, Kilindi, Monduli, Longido na Manispaa ya Ilala. CAG pia ameagiza kufanyike uchunguzi maalumu ktk Halmashauri za Arusha, Songea, Morogoro na Misungwi, zote hizo zinaongozwa na CCM.
MY TAKE
Ubadhirifu ktk Halmashauri ni kielelezo cha ufisadi Wizara mama TAMISEMI ya Mkuchika na Serikali kwa ujumla.
Wananchi tuukatae ufisadi huu kwa kutowapigia kura CCM.
 
Kwani ukiongoza kwa dhambi, utaongoza kwa kuchomwa moto? kama ni kweli tunawafanyaje hawa wanaCCM? kama sio kweli basi haina maana ya kusubiri mtu afanye dhambi kubwa ndo utoe adhabu.
 
Mkuu nimetupia macho kwenye report ya CAG nimeona madudu ya ajabu sana mfano, malipo yenye nyaraka pungufu, malipo hewa, mtu mmoja kulipwa mishahara zaidi ya mmoja n.k

Huu ni ushahidi wa ukosefu wa uadilifu wa watendaji wetu ambao wengi hawana hata vyama.
kwa maoni yangu hili ni tatizo kubwa sana na tukilileta kisiasa haitakuwa imetulia hata kidogo!

Kuna haja ya bunge letu kutunga sheria na adhabu kali maana naamini kama tungekuwa na sheria kali haya madudu yasingetokea kabisa.

Mkuu naona tunapaswa kwenda mbali zaidi ya kisiasa katika kuangalia huu uozo ambao unatendwa na hawa watendaji wetu.
 
ndo maana tunawaasa watz wajaribu upinzani waone na wao wanafanya nini kuliko kuendelea kuipa ccm nchi,na hiyo kweli kaka na tunajua hizo halmashauri mf.moshi v.ni balaa tupu
 
kuipenda ccm inakubidi uwe na akili ya maiti, huwezi kuwa mtu timamu uipende ccm.
 
ndo maana tunawaasa watz wajaribu upinzani waone na wao wanafanya nini kuliko kuendelea kuipa ccm nchi,na hiyo kweli kaka na tunajua hizo halmashauri mf.moshi v.ni balaa tupu

Kidogo kidogo watanzania wameanza kuelewa, huenda 2015 mambo yakawa mazuri, na CCM wakakaa bench!
 
Back
Top Bottom