masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,172
Hatimaye baada ya takriban miaka 10 iliyopita Jiji la Mbeya limeamua kujenga City Mall ya kisasa pale sehemu inaitwa "Uhindini".
Sehemu hii katikati ya Jiji kulikuwa na soko na vibanda vya biashara vilivyoteketea kwa moto. Haya nimaendeleo chanya.
Hata hivyo kero ya kuingia mjini Mbeya toka aidha Mbalizi au Uyole inaendelea kuwa kero kubwa sana.
Jiji halina mipango mbadala, hata kuboresha side roads na service roads (ya main roads) hakuna maendeleo hayo.
Hata ile barabara ya mchepuko toka Uyole hadi Mbalizi, iliyoahidiwa na Waziri Kamwelwe inaelekea ilikuwa ahadi tu.
Jiji lazima liwe na mipango yake mbadala kuondoa kero hii.