Halmashauri ya Jiji la Dar ifute kiingilio stendi kuu ya Mabasi Ubungo

Hii ndp Tzee kaka kuna wajanja wachache hawatoijasho wao wanapiga pesa kimagumash tuu.. ndo mana hata Mbunge wa jimbo hana kauli uskute nae yupo kwenye mpango
Tanzania bhana ful magumashi
 
Nafukuzia tenda ya kiingilio cha muhimbil nayo itakuwa mia 2 kwa wataotaka kuwaona wagonjwa maana wataganyika mna hela sana ampend kuoj kwann malipishwa sehemu kama ile UBUNGO ambapo ndan ukiingia kujisaidia c bure unalipa tena
 
Inasikitisha hali ilivyo Ubungo bus terminal; vumbi, madimbwi ya maji yanayosababishwa na mvua nk, sielewi ni kwanini Halmashauri ya Jiji inaendelea kukusanya kiingilio katika hali iliyopo. Vijana wanaoingia ndani ya kituo hicho kujitafutia riziki kwa kuuza pipi, vitambaa, wanakamatwa na askari wa jiji na kusingiziwa kesi kwamba wanawabughudhi abiria.

"Kuna bosi wa maaskari wa halmashauri ya jiji anapita kukusanya, tusipompa anatubambikia kesi, tunapelekwa mahakama ya jijji kisha Segerea, ndio nchi yetu inavyoendeshwa", anasema kijana anaeitwa Hamisi.

Naomba kuikumbusha Halmashauri kuwa, kiingilio kwenye kituo hicho kilianzishwa kwa lengo kuwa mtu akiingia akute usafi umefanyika na pia anapotaka kujisaidia aweze kuingia msalani bila malipo. Ajabu siku hizi getini unalipia na ukienda msalani unalipia tena!

Hii ni dhuluma, hebu wahusika jiulizeni malipo ya getini niya nini? Hivi ni kwanini mnamuongezea raia wa chini mzigo? Hata kama ni kubuni njia ya kuingizia mapato halmashauri jaribuni kubuni njia zisizo na dalili ya dhuluma ni laana.
 
Patageuka dampo la mateja,vibaka na vyangu!Tunatakiwa kuongeza mapato na hcho nı chanzo kimojawapo.
 
Sijapinga kuongeza mapato elewa,ilitosha tu kulipia getini kisha unapo ingia utumie huduma ya choo kwa mchango ulioutoa getini,
 
Ngoja madiwani wa Ukawa waapishwe mambo yatabadilika hapo. Meya wa jiji atatoka Ukawa
 
Patageuka dampo la mateja,vibaka na vyangu!Tunatakiwa kuongeza mapato na hcho nı chanzo kimojawapo.

Kama lengo lako ni kuepuka kuwa dampo la mateja, vibaka na vyangu mbona hamkuweka barrier pale chalinze kuzuia hao watu kuingia Dar. Kama huelewi mleta mada anamaanisha nini si ukae kimya? Ama wewe ni mmoja ya watu wanaofaidi wizi huo hapo basi terminal?

Kwa michango hiyo ilitakiwa mtu ukiangia humo ndani ukutane na huduma za kibinaadamu zinazolingana na kodi hiyo na sio hicho kinachoendelea hapo. Tabia hii ipo kila mahali nchi hii, unakuta watu wanakusanya kodi lakini hudumu haiendani na kodi inayolipwa.

Unakuta wasimamizi wa miradi hiyo wanaporomosha manyumba ya bei mbaya, huku wakimiliki magari ya bei chafu, lakini hata kujali wanapopati riziki hawakumbuki. Halafu anatokea mtu kama wewe unatetea huo upuuzi huo.
 
...subiri ukawa washike Halmashauri, tenda atarudishiwa Kingunge na kila kitu kitakuwa shwari !:poa
 
Sijaona umuhimu wa kuwachangisha watu, wahusika wakuu wafute tu hicho kiingilio
 
Inakera sana, ukizingatia stand ilivo mbovu kias kile. Kwanza huwa sielewi tafsiri iliyoandkwa kwenye ile tiketi: "Ushuru wa kusindikiza abiria" hiv ina maana gani??
 
Inakera sana, ukizingatia stand ilivo mbovu kias kile. Kwanza huwa sielewi tafsiri iliyoandkwa kwenye ile tiketi: "Ushuru wa kusindikiza abiria" hiv ina maana gani??

Alafu waandishi wetu hawa wa kibongo hata hawalihoji hilo je vile viingilio pale ubungo ni mradi wa faida ya nani serikalini? Waweke wazi nadhani inaingia pesa nyingi sana pale
 
Kwanini ifutwe? Huoni kama itakua ni kero kubwa kwa wasafiri?maana ata asiye na shida humo atakua anaingia tu na usalama utakua zero. So think twice.
 
Kwa yoyote anaye husika;

Hii ni kero ninayoileta kwako mfumo wa swali, nauliza hivi makusanyo ya shilingi za kitanzania mia mbili (200/-) kwa kichwa kama kiingilio pale Ubungo stand ya kwenda mikoani ni kwa maslahi ya nani?

Nauliza hivi kwa kuzingatia ukweli kuwa ndani ya stand hakuna huduma yoyote itolewayo bure hata choo inampasa msafiri alipie TZS. 300/- na choo chenyewe hakina hadhi.

Natamani mbunge wa Ubungo apitie pale akajionee maana naona kama Mh. Mkuu wa Wilaya jambo hili limemshinda.

Nawasilisha kwa nia njema
 
Back
Top Bottom