Hii hoja haihitaji maneno mengi wala ubishi, ukweli uko wazi kabisa.
TANZANIA kwa sasa ni moja ya nchi masikini sana duniani na watu wake wengi kwa asilimia kubwa huishi katika umasikini mkubwa.
Inatia uchungu sana kuambiwa eti nchi yenu ipo kundi la nchi masikini kabisa na ombaomba huku mkijua kabisa hali hii husababishwa na wapumbavu wachache kwa maslahi binafsi na vimada wao.
Kiukweli moja ya chanzo kikuu cha umasikini wa taifa hili ni halmashauri zetu, watendaji wa halmashauri zote wamechangia kwa kiasi kikubwa umasikini huu, sio wakati tena wakucheka na hawa wapumbavu bali ni wakati wakuwajaza kwenye jela zetu, kuwafilisi na mwisho kuwaua kabisa.
Maneno mengi hatuyahitaji tena na tuko nje ya muda, ni wakati sasa wakutoa adhabu na hakuna adhabu nyingine zaidi ya kuwafilisi, kuwafunga jela za pembezoni na adhabu kali.
Vyomba vyote vya usalama ni mali ya serikali, Mh Rais ndio mtoa amri, sasa nini tunashindwa kuadhibu asilimia ndogo ya wapumbavu wanaoleta huu mkwamo?, watu zaidi ya mil 45 tunashindwaje na hawa wapumbavu wachache mpaka Taifa linakuwa maskini hivi.
INAKERA, eti tunaitwa moja ya taifa masikini duniani nasi tumekaa tu tumeridhika, huku wengine eti wanajiita wasomi na videgree, vimasters, viphd na wengine maprofesa sasa sijui unajiitaje msomi huku taifa lako ni masikini.