Halmashauri jiji la Arusha inanyanyasa Wafanyabiashara wa nyama

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
86
280
Wafanyabiashara wa maduka jijini Arusha wamelalamikia Halmashauri ya jiji la Arusha Kutokana na hatua ya kufunga maduka Yao wanapokuwa wakidai leseni au Kodi mbalimbali Jambo ambalo linakiuka maelekezo ya Serikali ya kutofunga maduka ya Wafanyabiashara.

Miongoni mwa Wafanyabiashara hao, Juma msofe Mkazi wa uswahilini jijini hapa, amelalamikia utaratibu wa kufunga duka lake la Nyama na kusababisha kilo zaidi 60 za Nyama kuharibika .

Alifafanua kwamba Jana majira ya saa nne asubuhi maofisa wa Biashara walifika katika bucha lake na kumhoji muuzaji wa bucha Hilo, Juma Omari kuhusu leseni, ambaye Hata hivyo aliwajibu kuwa boss wake hayupo, ndipo walipoamua kufunga duka Hilo bila kijali bidhaa iliyopo ambayo ni kilo zaidi 60 za Nyama kuweza kuharibika.

"Walikuja watu wawili wakawa wanaulizia leseni niliwaambia kuwa mwenye duka hayupo waliniambia nitoke wafunge ,niliwaomba wasifunge Kuna Nyama kilo 60 itaharibika lakini waliniamuru nitika na kufunga kwa kuweka kufuri lao"alisema Juma Omari

Baadhi ya Wafanyabiashara wengine katika eneo Hilo wamedai kuwa utaratibu unaotumiwa na Halmashauri hiyo ni kinyume cha maelekezo ya Serikali inayokataza Wafanyabiashara kufungiwa biashara zao

Akiongea kwa njia ya simu afisa biashara jiji la Arusha, Edward aliwataka wafanyabiashara kufuata Sheria na kuacha kufanya biashara Bila leseni kwani Kwa kufanya hivyo ni kinyume cha sheria
 
Halafu mtu siku atakayofanya kitu cha ajabu wataenda kumwita gaidi, huo ni mwanzo tu hukobeleni kila mtu atakuja kumiliki bomba yake kulinda mali zake dhidi ya magaidi na wizi wa Serikali wanaoibia wananchi
 
Halafu mtu siku atakayofanya kitu cha ajabu wataenda kumwita gaidi, huo ni mwanzo tu hukobeleni kila mtu atakuja kumiliki bomba yake kulinda mali zake dhidi ya magaidi na wizi wa Serikali wanaoibia wananchi
Kwa hiyo unataka wafanye biashara Tena sensitive namna hiyo bila leseni?? Halafu mkikosa madawa hospitalini mnaanza kelele huku mnaunha mkono watu wasilipie leseni za biashara
 
Back
Top Bottom