Halmashauri haina budi kuzuia magari kuingia katikati ya Jiji

Halmashauri haina budi kuzuia magari kuingia katikati ya Jiji

kimatire

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2008
Posts
371
Reaction score
94
Katika hali isiyo ya kawaida Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam haina budi kuzuia magari kuingia katika eneo lote la maduka Kariakoo na Katikati ya Jiji –( City Centre) siku za mwisho wa wiki yaani Ijumaa,Jumamosi na Jumapili.Kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 12 jioni kuwe na utaratibu wa kutokuruhusu magari au vyombo vyote vya moto kuingia katika maeneo hayo.

Hatua hii ni ya muhimu sana itasaidia kukabiliana na msongamano wa magari wakati wa shopping,Pia kupunguza walau kiasi cha hewa ukaa ndani ya Jiji.Pia itatoa fursa kwa waenda kwa miguu kuwa na wasaa mzuri wa kutembea na kutumia usafiri usio na uharibifu wa mazingira (Baiskeli na wala siyo pikipiki.)

Taratibu chache tu zitawekwa na zingine kubadilishwa.Naamini jambo hili linawezekana na litawajengea mazoea wakaazi wa Jiji kufanya mazoezi ya kutembea kwa miguu au hata kuendesha baiskeli.Kutapunguza matumizi ya kuwafanyisha askari wetu kazi za ziada.

Pia ni muhimu sana kwa mamlaka husika kuwadhibiti wafanya biashara ndogo ndogo ambao nao ni kero namba mbili wasipange bidhaa zao barabarani ili kutoa nafasi ya waenda kwa miguu kuwa na fursa nzuri ya kutembea.
 
Hii post imenikumbusha mbunge mmoja mkoani Tanga alipoulizwa anahitaji msaada gani akasema miswaki
 
Serikali haipo kwa ajili ya ku favor tabaka lolote lile la kijamii, kama huna gari hizo ni shida zako peke yako

Huyu jamaa anaongea kama vile ameshawah kwenda town weekend akapna namna kulivyo loose, watu wanaenda town kufanya kazi siyo shopping
 
Haya na hayo mapato ya parking watapata wapi
 
Siku za weekend town na kkoo hakuna hata foleni... siku za weekend foleni zinahamia kwenye nyumba za kulala wageni...
 
Back
Top Bottom