Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,495
Mbunge wa Kawe Halima Mdee amefunguka na kusema kuwa katika wasanii wa bongo anamkubali zaidi Roma Mkatoliki kuliko Diamond na Alikiba kwa kuwa wawili hao wote ni waimba mapenzi tu pamoja na umaarufu wao na siku zote mapenzi wanayoimba hayasaidii nchi.
“Nampenda Roma Mkatoliki kwasababu anaimba hali halisi, unajua wasanii ni vioo vya jamii sasa inategemea msanii anataka atumike vipi, atumike kibiashara peke yake ama atumike katika kuelimisha jamii mambo yanayoendelea katika nchi yake,” Mdee aliamuambia mtangazaji wa kipindi cha Hot Stage cha Jembe FM, Jay Jay.
“Kwahiyo Roma above all, yaani wasanii wote, si Diamond, si Alikiba wote wanaimba mapenzi, ni wasanii maarufu wanapendwa lakini mwisho wa siku wanaimba mapenzi na mapenzi hayasaidii nchi, kinachosaidia nchi ni wewe kuangalia namna gani unaweza kutumia taalum yako kama kioo cha jamii.
Watu wanakusikiliza ili kuweza kupeleka meseji, sio kupeleka meseji ya uchochezi bali ya uelewa, kucreate awareness kwa wananchi ambao wanawasikiliza wasanii kwa kiasi kikubwa. Kwahiyo kwangu Roma Mkatoliki amekuwa akifanya kazi nzuri kutumia sanaa kama kuburudisha lakini at the same time kuelimisha.”