G Jonathan Kamenge
Member
- Apr 8, 2023
- 24
- 15
Uko msamiati miongoni mwa wanazuoni wa Kikoloni kuelezea mtu ambaye kwa juhudi na maarifa yake pekee, bila usaidizi wa mtu ama mifumo au jamii fulani ya watu, huweza kufanikisha ama kufanikiwa kuinua maisha yake kwa viwango vya kushangaza. Hili laweza kuwa katika biashara, siasa na kadhalika, na wakoloni humuita mtu wa aina hii "self made" ama aliyejitengeneza mwenyewe.
Baada ya makala yangu juu ya niliyoipa jina "Millennials na GenZ na Siasa za Nchi yetu" kwenye majukwaa tofauti mtandaoni, wengi wamekuja na maoni tofauti. Wakati baadhi wamekuja na kashfa na mitusi (siwalaumu, naelewa hii ni dalili ya kukata tamaa hata kujaribu kutafakari juu ya hili), wako waliosema lawama zinapaswa kuelekezwa kwa chama kinachotawala nchini Tanzania cha CCM kwa "kuua Upinzani" na hivyo kufanya vijana wa sasa kupoteza dira ya mambo yahusuyo siasa. Wako waliodai serikali kupitia mkono wa Dola imewavunja moyo wengi na baadhi wakisingizia madhila yaliyomkuta mwanamuziki "Roma Mkatoliki" kuwa chanzo cha wasanii wetu kuogopa ama kuchukia kuzungumza siasa.
Ebu tutafakari. Kwanza ni je CCM inapaswa kulaumiwa kwa vijana kupoteza hari ya kujihusisha siasa za nchi yao!!? Jibu langu mimi ni "ndiyo". Kwa sababu hari na mapenzi ya siasa miongoni mwa vijana siyo na haijawahi kuwa "self made", mara zote hili limekuwa moja ya mazao bora kabisa ya huyu "Baniani mbaya" aitwaye CCM kupitia mfumo wake wa UVCCM kuandaa viongozi wajao; ni kutoka huko waliandaliwa wanasiasa wote waliowahi na hata wanaoendelea kuwa maarufu katika siasa za Tanzania. Ni CCM iliyoanzisha utamaduni wa kufundisha siasa mashuleni tangu shule za msingi, sekondari, vyuo na hata kwenye majeshi miaka mingi kabla ya ujio wa "Demokrasia" ya kimagharibi na kurejesha sera za vyama vingi, na hivyo siasa kugeuka sumu badala ya somo kwenye elimu msingi.
Wahenga tunakumbuka siasa likiwa somo tangu shule za msingi ambapo ufaulu katika masomo kama sayansi, kilimo, maarifa na siasa vilimpa mtu nafasi ya kwenda sekondari akiwa amejengewa uwezo wa msingi kushiriki vyema mfumo wa maisha wa jamii yake huko aendako. Baada ya 1995, tukabadili (nadhani tulipaswa kuboresha) mitaala na kuondoa kabisa baadhi ya masomo ambayo kimsingi ndiyo yaliyotusaidia wakati huo tukiwa watu milioni kumi na kidogo, tukiwa na wasomi wasiozidi 100 kujenga taifa la watu bora Afrika Mashariki na Afrika nzima, wenye makabila na lugha zaidi ya 120 na bado wanaweza kumaliza tofauti zao kwa majadiliano badala ya mtutu wa bunduki, walau kwa takribani miaka 60 sasa tangu uhuru wa bendera.
Wengi wetu (hata taliokuwapo wakati huo) hatufahamu kwamba hiki kiitwacho "upinzani" hakikuwapo Tanzania isipokuwa tu kwa ridhaa ya waasisi wa CCM baada ya mataifa ya magharibi wakati huo kutishia kutunyima "mikopo na misaada" hadi tutakaporuhusu aina yao ya "demokrasia. Ujamaa ukiwa umeanguka na ukomunist umedhoofu, wazee wetu wakaamua kuwaita kando vijana wao akina Mabere Marando, Mtei, Seif Sharif Hamad na wengine na kuwaagiza "kuanzisha vyama vya upinzani" ili kukidhi matakwa ya kidemokrasia ili pamoja na mambo mengine tuvuke kwenye hali ngumu ya uchumi wa dunia na wa kwetu hasa baada ya vita ya 1978 na Uganda.
Hapo "vikazaliwa" tena vyama vya upinzani na ukawa mwisho wa siasa mashuleni na nyimbo kama "Chama chetu cha Mapinduzi chanjenga Nchi, Nyerere ahaa na Mwinyi na Mwinyi, wajenga nchi.....". Sisemi tulipaswa kuendelea kuimba CCM, nasema tulipaswa kuendelea kuwafundisha watoto na vijana wetu siasa mashuleni kwa faida ya vizazi vijavyo. Labda ndiyo maana fikra tunduizi za siasa zinaonekana kukomea Generation X kwa sasa ndiyo pekee waliokuwa wa mwisho "kufaidi" masomo ya siasa.
Nasema lawama zote ni kwa CCM. Ndiyo, ni CCM aliyekuwa "mzazi" wa wataalamu ambao pia walikuwa na fikra tunduizi za kisiasa. Watu kama Profesa Baregu, Profesa Safari, Daktari Lwaitama ama Padre Willbroad Slaa, walikuwa mazao ya CCM na mafundisho yake ambao hata katika kuanzisha na kuongoza vuguvugu kubwa kabisa la "Uamsho wa kisiasa" kuwahi kuonekana hapa Tanzania kupitia CDM, walikopa karatasi moja ama mbili kutoka kitabu cha CCM, asomaye na afahamu.
Wakati walipoanzisha mfumo wa kushawishi vijana wasomi vyuoni kujiunga na siasa hazaza za upinzani na kuwapa majukwaa ya kufanya "recruitment" ya wenzao, ndipo wakazaliwa wanasiasa waliohamasisha wengi wa Generation X na hata baadhi ya Millennials kuingia siasa. Watu kama Zitto Kabwe, Halima Mdee, John Mnyika na wengine, ni mazao ya juhudi hizi ambazo nazo ni mazao ya mbinu na ubunifu wa CCM. Kwa hiyo ikiwa siasa zetu zimewakinai vijana, wazazi lazima kulaumiwa na wazazi ni CCM.
Nitarejea kujadili ikiwa serikali kwa mkono wa dola imewavunja moyo wengi wa vijana kujihusisha na siasa, ila kwa sasa hizi ni salaam nawasalimia!