Njaa Mbaya
JF-Expert Member
- Jul 4, 2012
- 666
- 175
Halima mdee yeye kushughulikia issue za wapiga kura haonekani mshahara wa magufuli ndiyo unanatatua kero za wakazi wa kawe kweli?
Wachache watakuelewa.Wanaoshangaa swali la Mdee ni wengi wa watanzania wasiojua haki zao.
Kama wenye 40 m wanapunguziwa ni haki kujua mshahara na marupurupu ya Rais.
Poa tu! Yeye ni muajiriwa na wananchi.Tunakoelekea Rais ataambiwa ataje na matumizi yake binafsi na ya familia
kwani kuna dhambi?Tunakoelekea Rais ataambiwa ataje na matumizi yake binafsi na ya familia
wewe hoja yako niniAmekosa hoja huyo
Ataje ya kwake kwanza anayopewa na CDM na vyanzo vingine. Leo kakurupuka sijui alijificha wapi muda wote ?Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee amemuomba Rais John Magufuli kuweka wazi posho na marupurupu anayoyapata ili Watanzania wajue kiasi halisi anachokipata mbali na mshahara wake.
Mdee ambaye ni mbunge wa Kawe, alitoa ombi hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Sokoni, Jimbo la Mtama mkoani Lindi, uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo.
Kauli hiyo ya Mdee imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kutaja mshahara wake kuwa ni Sh9.5 milioni kwa mwezi.
“Juzi Rais anasema eti mshahara wake Sh9.5 milioni, sasa atutajie posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho anakipata,” alisema Mdee. Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh3 milioni, lakini kuna posho mbalimbali kutokana na kuhudumia wananchi.
“Sisi wabunge mshahara wetu katika hati ya mshahara unasomeka Sh3 milioni, lakini posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika Sh10 milioni, Rais atuambie na yeye posho zake ni kiasi gani,” alisema Mdee.
Chanzo: Mtembezi