Halima Mdee amtaka Rais Magufuli ataje posho na marupurupu anayolipwa

Je, Majaliwa atazuia posho za milioni 10 kwa mwezi kwa Wabunge!? Au zuio ni kwa wafanyakazi wa taasisi za Serikali na umma tu!?:eek::eek::eek:
 
Kazi ya upinzani sio kusifu. Ndio hiyo, ni vyema tujue posho za viongozi wetu wakuu ili tuone kwa vitendo uzalendo wao. Iweje wao walipane posho kisha waondoe posho kwa watumishi wa umma huku wakisingizia kichaka cha Miradi ya maendeleo
 
Mayatima ajira zetu nasikia baada ya uhakiki zimeandikwa kwa penseli, ukimtingisha mkubwa anachukua mfuto.
 
Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee amemuomba Rais John Magufuli kuweka wazi posho na marupurupu anayoyapata ili Watanzania wajue kiasi halisi anachokipata mbali na mshahara wake.

Mdee ambaye ni mbunge wa Kawe, alitoa ombi hilo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Sokoni, Jimbo la Mtama mkoani Lindi, uliohudhuriwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo.

Kauli hiyo ya Mdee imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kutaja mshahara wake kuwa ni Sh9.5 milioni kwa mwezi.

“Juzi Rais anasema eti mshahara wake Sh9.5 milioni, sasa atutajie posho za kila siku ili kila Mtanzania ajue kiasi ambacho anakipata,” alisema Mdee. Mdee aliongeza kuwa wabunge wanalipwa mshahara wa Sh3 milioni, lakini kuna posho mbalimbali kutokana na kuhudumia wananchi.

“Sisi wabunge mshahara wetu katika hati ya mshahara unasomeka Sh3 milioni, lakini posho na pesa ya mambo ya utendaji ya mbunge inafika Sh10 milioni, Rais atuambie na yeye posho zake ni kiasi gani,” alisema Mdee.


Chanzo: Mtembezi
Ataje ya kwake kwanza anayopewa na CDM na vyanzo vingine. Leo kakurupuka sijui alijificha wapi muda wote ?
 
Back
Top Bottom