Halima Mdee amsambaratisha Magufuli

Nimewahi kuishi Chato kwa muda miaka kadhaa, mwez uliopita tu ndipo nlipoondoka Chato, japo huu mkutano wa Halima Mdee hapa Chato nilikuwepo!! Iko hivi ktk jimbo hili la Chato kumng'oa Magufuli 2015 bado sijaona. Sio kwamba haiwezekani, inawezekana, lakini inatakiwa itumike nguvu na akili kubwa sana, Magufuli kafanya mambo makubwa sana sana Chato. Chato wanampenda kwa maendeleo aliyoyaleta kama vile barabara nzuri, umeme japo sio wa uhakika, huduma za afya na elimu amejitahidi, ujenzi wa ofis nzuri za halmashauri kwakeli Chato kaitoa mbali sana, huwez amin kwasasa barabara za lami zinajengwa mpaka vichochoroni kitu ambachohakifanyiki Kawe _DSM, ukiuliza hii barabara inaenda wapi utasikia "inaenda mwaroni/gatini, jineri n.k). Maghufuli ana vitu viwili vinavyoweza kumtoa madarakani ambavyo wananchi wamekua wakilalamika 1:Maghufuli anadharau wananchi masikin kwa kuwatolea lugha chafu, lugha chafu amekua akiitoa kwenye mikutano ya hadhara na wananchi. 2:Maghuli anakashfa ya kuwa chanzo kuua kiwanda cha PAMBA.
 

Na ajabu ni kwamba aliesababisha wasiwe na kazi za kufanya na wasiwe na ajira ni chama kilichopo madarakani!!
 
Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Halima Mdee jana alitikisa Jimboni Chato kwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara kuwahi kuhutubiwa jimboni hapo miaka ya karibuni.

Awali Mdee alilakiwa na umati mkubwa wa watu wakiwa na msururu mrefu wa magari,pikipiki,baiskeli huku akina mama wakiwa kandokando ya barabara wakipunga matawi ya miti.

Ujumbe mkubwa wa Halima Mdee kwa wanaChato ni kuikataa Katiba Haramu ya CCM na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Halima Mdee maarufu kama Tanzanian Iron Lady alipokea kadi 200 za watu walioamua kujitoa CCM na kujiunga Chadema.Huku mamia ya wananchi wengine ambao hawakuwa na chama wakijiunga pia Chadema.

Ikumbukwe jimbo la Chato linaongozwa na mbunge wa CCM John Pombe Magufuli ambaye ni waziri wa Ujenzi.

Ni simulizi hapa Chato kuanzia jana mpaka asubuhi hii kumzungumzia Halima Mdee na Chadema!
 
MAGUFULI hana jipya ni vuvuzela tu asahau kurudi bungeni 2015 imekula kwake janja yake ya nyani imestukiwa
 

Hapa ni Halima Mdee.Je akija Rais Mtarajiwa Dr Slaa Itakuwaje ...
 
Mkuu Kimbunga vaa miwani uone vizuri

Mkuu Molemo wakati naandika ulikuwa hujaweka picha!

Mbona UKAWA mnakulana wenyewe kwa wenyewe? Nimeona kadi ya CUF hapo. Ina maana nayo itachomwa moto? Huo ndio mwanzo wa ugomvi!!!
 
Last edited by a moderator:
Siasa bwana.....ni mchezo mzuri na mbaya.....umati wa watu hauwezi kutoa majibu positive....wengine wpo tu kusikiliza na kujiongeza maarifa ya jinsi nchi inavyooenda lkn sio kwamba upo pamoja nao....
 

poor mind set
 
kutumia akili ni juhadi na inataka busara. Kama umepiga msokoto hilo litakuwa gumu kwako . kumfananisha Magufuli na huyo msagaji
 

JF ni sehemu ya heshima, nilikuwepo kipindi mkutano unafanyika, aliyerudisha kadi ni mtu mmoja tu mke wa Huru Selemani na Mdee alitaja Magufuli wakaitikia "Juu" .Propaganda za uongo huwa sizipendi ni bora kukaa kimya.

Pia picha katika gazeti "..mkutano wa hadhara uliyofanyika juzi katika viwanja vya stendi ya zamani..." hii stendi tupo hapa kila siku hakuna mandhari kama haya katika stedni hii ya zamani, propaganda tuzifanye ila ziwe za ukweli tusilazimishe kudanganya jamani - very bad!

Huyu (Magufuli) ni kati ya viongozi wachache walioko huko magambani ninaowakubali wanavyojitoa kusaidia taifa na watu masikini. niliwahi kupata clip zake katika youtube:



​
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…