Halima Mdee amkana Mkono

Halima Mdee amkana Mkono

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
mdee.jpg
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee

Siku moja baada ya Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kusema amelishwa sumu akiwa London, Uingereza, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amemtaka kusema ukweli na si kulihadaa Taifa kwa uongo.

Mkono akizungumza na waandishi wa habari juzi kuelezea mwenendo wa afya yake, alisema lengo la kulishwa sumu ilikuwa ni kutaka kuharibu figo zake ndani ya saa 72 kitendo kilichoshindikana.

Mdee aliyekuwa na Mkono katika ziara hiyo alisema: "Hakuna ukweli wowote kwamba alilishwa sumu, nilikuwa naye kule na mazingira aliyoanza kuumwa hadi kupona kwake ni utata... awaeleze Watanzania anaumwa nini na si kusema alilishwa sumu.

"Nilikaa kimya baada ya kuripotiwa na gazeti moja (The Citizen) kwamba Mkono kalishwa sumu, sasa amezungumza tena nikaona si busara kukaa kimya wakati alilidanganya Taifa. Mkono waeleze ukweli watu mbona unawadanganya."

Mdee aliwataja baadhi ya wajumbe wa msafara huo wa watu 11 kuwa ni William Ngeleja (Mwenyekiti wa kamati hiyo), Mkurugenzi wa Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru), Dk Edward Hoseah, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika.

"Dk Hoseah ndiye aliyezungumza na daktari wa Mkono kwa kina zaidi na alimweleza kuwa ampatie dawa fulani, sasa kama kweli alilishwa sumu daktari wake alijuaje kuwa sumu hiyo inaondolewa na dawa hiyo aliyomwambia Hoseah ampe.

"Kama ni kutaka kutumia kivuli cha sakata la escrow, arudi bungeni tuijadili na tuimalize ila asiseme kuwa sijui wanataka kumuua ni uongo," alisema Mdee.

Kuhusu vitisho alivyodai Mkono kutumiwa kabla ya safari hiyo, Mdee alisema: "Kama kweli ni vitisho iweje tulivyokwenda aliamua kulala peke yake, wewe upo safarini na wenzako halafu ukatishwa kuuawa utakwenda kulala peke yako au utalala na wenzako?"

Mkono alisema anaendelea vizuri na anasubiri kujua hatima ya uchunguzi unaoendelea ili kubaini chanzo cha kulishwa sumu.

"Niko vizuri na afya njema... kama kuna mtu anawinda jimbo langu, mwambieni ameshindwa na wananchi wangu nawaeleza kuwa niko salama wasiwe na hofu. Ninataka kujua nani kanilisha sumu na kwa nini?

"Tukiwa uwanja wa ndege nilipokea ujumbe mfupi wa maandishi (hakutaka kuuweka wazi kwa sababu upelelezi haujakamilika), ukinitahadharisha kuwa makini, ujumbe ule ulinishtua kwa kweli,"alisema.

Source:
Mwananchi

http://www.mwananchi.co.tz/habari/K...kono/-/1597296/2535340/-/14ejtma/-/index.html
 
kwa leo pesa zetu za Escrow kwanza hadithi zingine baadaye!
 
Kumbe hii ngoma bado ni mbichi kabisa? Kha! Cry my beloved country. Things are falling apart.
 
Kwa hili, namuunga mkono Halima kwa kusema ukweli.
Hakuna mtu hadaa kama huyo Nimrod Mkono, ni tapeli wa fedha na maneno.
Inaelekea kachota kote kote, Tanesco na IPTL.
Mtu gani atalishwa sumu wiki iliyopita na leo anaongea na vyombo vya habari-tapeli huyo, kwisha!
 
Nilikataa na nitaendelea kukataa Mkono niliyemuona juzi anaongea hakuwahi kulishwa sumu,aeleze ukweli anachoumwa!
 
Naona baada ya Bilali wa BOT, Mwakyembe na Mwandosya kulishwa sumu, sasa wengine wameona kusema nimelishwa sumu ni ujiko wa kisiasa! Mkono pale alipo hata soda haruhusiwi kunywa kwa sababu za kiafya, leo anasema anaumwa figo sijui kwa sababu kalishwa sumu?
 
RUCCI

Mkono angelishwa sumu sijui kama angeamka? mwenyewe gonjwa siku nyingi ukiongeza sumu je! danganya watu hapa
 
Last edited by a moderator:
View attachment 205746
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee

Siku moja baada ya Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono kusema amelishwa sumu akiwa London, Uingereza, Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee amemtaka kusema ukweli na si kulihadaa Taifa kwa uongo.

Mkono akizungumza na waandishi wa habari juzi kuelezea mwenendo wa afya yake, alisema lengo la kulishwa sumu ilikuwa ni kutaka kuharibu figo zake ndani ya saa 72 kitendo kilichoshindikana.

Mdee aliyekuwa na Mkono katika ziara hiyo alisema: “Hakuna ukweli wowote kwamba alilishwa sumu, nilikuwa naye kule na mazingira aliyoanza kuumwa hadi kupona kwake ni utata... awaeleze Watanzania anaumwa nini na si kusema alilishwa sumu.

“Nilikaa kimya baada ya kuripotiwa na gazeti moja (The Citizen) kwamba Mkono kalishwa sumu, sasa amezungumza tena nikaona si busara kukaa kimya wakati alilidanganya Taifa. Mkono waeleze ukweli watu mbona unawadanganya.”

Mdee aliwataja baadhi ya wajumbe wa msafara huo wa watu 11 kuwa ni William Ngeleja (Mwenyekiti wa kamati hiyo), Mkurugenzi wa Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru), Dk Edward Hoseah, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika.

“Dk Hoseah ndiye aliyezungumza na daktari wa Mkono kwa kina zaidi na alimweleza kuwa ampatie dawa fulani, sasa kama kweli alilishwa sumu daktari wake alijuaje kuwa sumu hiyo inaondolewa na dawa hiyo aliyomwambia Hoseah ampe.

“Kama ni kutaka kutumia kivuli cha sakata la escrow, arudi bungeni tuijadili na tuimalize ila asiseme kuwa sijui wanataka kumuua ni uongo,” alisema Mdee.

Kuhusu vitisho alivyodai Mkono kutumiwa kabla ya safari hiyo, Mdee alisema: “Kama kweli ni vitisho iweje tulivyokwenda aliamua kulala peke yake, wewe upo safarini na wenzako halafu ukatishwa kuuawa utakwenda kulala peke yako au utalala na wenzako?”

Mkono alisema anaendelea vizuri na anasubiri kujua hatima ya uchunguzi unaoendelea ili kubaini chanzo cha kulishwa sumu.

“Niko vizuri na afya njema... kama kuna mtu anawinda jimbo langu, mwambieni ameshindwa na wananchi wangu nawaeleza kuwa niko salama wasiwe na hofu. Ninataka kujua nani kanilisha sumu na kwa nini?

“Tukiwa uwanja wa ndege nilipokea ujumbe mfupi wa maandishi (hakutaka kuuweka wazi kwa sababu upelelezi haujakamilika), ukinitahadharisha kuwa makini, ujumbe ule ulinishtua kwa kweli,”alisema.

Source:
Mwananchi

Halima Mdee amkana Mkono - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Mmmmh! kifua kinaanza kujaa
 
Mtu kulishwa sumu hapa UK hiyo ni terrorism na vyombo vyote vya dola vingejazana kushughulikia.

Mkono analeta uongo wa kule vijijini ambako watu hawajui nini kinaendelea duniani.

Waingereza sasa wana wasiwasi mno na ugaidi. Hata mambo madogo wanayapa nguvu ndio iwe kulishwa sumu?

Mwambieni aseme alipelekwa hospitali gani hapo London kutibiwa?
 
Nilikataa na nitaendelea kukataa Mkono niliyemuona juzi anaongea hakuwahi kulishwa sumu,aeleze ukweli anachoumwa!

unajua hivi vizee havitaki kungatuka mpk viabishwe! Vimejichotea mahela tangu enzi za Uhuru lakini havitosheki!
Wacha kipewe sumu hakina effect yoyote ajuza! Hata kutembea kinapepesuka!
Kipeni sumu kirest in pc nyambaaf zake! Ulafi tuu!
 
Mtu kulishwa sumu hapa UK hiyo ni terrorism na vyombo vyote vya dola vingejazana kushughulikia.

Mkono analeta uongo wa kule vijijini ambako watu hawajui nini kinaendelea duniani.

Waingereza sasa wana wasiwasi mno na ugaidi. Hata mambo madogo wanayapa nguvu ndio iwe kulishwa sumu?

Mwambieni aseme alipelekwa hospitali gani hapo London kutibiwa?

Aliletewa mizizi ya kibongo na witchdoctor wake wa huku nyumbani!
 
Halimamdee kaeleeza magazetinileo akuna alielishwa sumu...akaeleza walipofika huko hata kabla ajala chochote h Ali ilikuwa tata akaaja Dk akaumuuliza Dk wa nkono anaumwa nini...dk wa mb akamwambia anaitaji dawa Fulani akinywa inakuwa haliyake poa...akauliza kama alilishwa sumu iweje Dk wake aseme MPE dawafudenge??gafla yukosawa

Akaomba nkono aeleze ukweli anaumwa niini badala ya kusingizia amelishwa sumu

Patamu

Kwako NN.tupe
 
Back
Top Bottom