Halima Hussein has came back to my life as Fatma Bint Habib.

Halima Hussein has came back to my life as Fatma Bint Habib.

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
20,006
Reaction score
37,915
First of all her name is not Fatma Bint Habib ..Is Fatma Bint ..... Nimeficha jina la baba ake kwa sababu za ki intelijensia.

Back to my topic.

In 1994 nikiwa darasa la 3 katika shule ya msingi .... Nilitokea kumpenda sana binti aliyeitwa Swaumu Bint ........ She was my crush. To describe her in one sentence " She was the female version of my own self " I saw a lot of me in her . It was as if I was just loving myself ..her being a part of me. I was 8 and 9 years old in that year.

Swaumu ( sio jina lake halisi ) was born in 1983 so she was out aging me for two years.


JINSI NILIVYO KUTANA NA SWAUMU

Kuanzia naanza darasa la kwanza mwaka 92 hadi la pili mwaka 93 sikuwahi kufahamiana na Swaumu . Tulikuwa tunasoma mikondo na madarasa mawili tofauti . Nilifahamiana na Swaumu kwa Mara ya kwanza mwaka 1994 tukiwa darasa la tatu baada ya baadhi ya wanafunzi walio kuwa wanasoma mkondo mmoja na Swaumu kuhamishiwa darasani kwetu.

Nilifahamiana na Swaumu kupitia Tuition .

Baba angu alinipeleka Twisheni kwa mwalimu aliye kuwa anafundisha katika shule tofauti na niliyo soma Mimi . Mwalimu huyo alisifika kufundisha vyema Hisabati,Sayansi na English.

Nilipofika Tuition siku hiyo kwa Mara ya kwanza wanafunzj tulikuwa wachache so mwalimu akatuchanganya wanafunzi wa darasa la tatu la NNE na tano ndani ya chumba kimoja.

Baadae " akaanzisha Uzi " ' wanao soma darasa moja wakae pamoja' alimaanisha kama upo la tatu basi ukae pamoja na la tatu mwenzako.

Darasa la tatu tulikuwa wawili tu Mimi na Swaumu na.more interestingly wote tulikuwa tunasoma shule.moja.
Hivyo ndivyo nilivyo fahamiana na Swaumu.

Je unajua kitu.gani kiliendelea baada ya hapo? Mimi na Swaumu ilikuwaje ? Halima Hussein ? Fatma Bint Habib? ..

ITAENDELEA BAADAE


Part 2 :

Mimi na Swaumu tulipendana sana sana sana. Our love for each other was more Agape oriented then erotic.

Ni story ndefu sana but to make it short mwaka 1994 mwezi Desemba baba wa Swaumu aliuwawa kwa Risasi na watu wasio julikana.


Hapo ndo nilipo gundua kwamba

1. Baba wa Swaumu hakuwa baba yake mzazi. Mama Swaumu ni Mwera wa Lindi. Kabla ya kuja kuolewa Dar Es Salaam tayari alikuwa na watoto kadhaa akiwemo Swabahi ambae alikuwa ndo kitinda mimba. Swabahi alikuja DAR kuishi na mama yake baada ya mama ake kuolewa na mzee huyo.

2. Hata surname alilo kuwa akitumia Swaumu lilikuwa jina la huyu baba ake wa kambo.

3. " Baba" wa Swaumu alikuwa mpigaji.Alikua anapiga kwa styles nyingi sana .. Kubwa zaidi alikuwaga ana foji tiketi za mechi za Simba na Yanga na events nyingine kubwa kubwa ..Yani kama Yanga au Simba wanacheza Taifa basi mzee anakuwa na tiketi zake tayari.Vijana wake wanaenda kusuply tiketi mtaani.

Kaja siku Kandabongoman kufanya onyesho Dar es salaam, tiketi utapata kwa mzee Yule tena kwa bei pungufu..


Inasemekana aliwadhulumu wenzake wakamtumia.majambazi.

Baada ya kifo.cha baba yake wa kambo Swaumu na mama ake wakarudi kwao.Lindi.

Mpaka Leo hii i cant still sense the pain that I felt .. Lilikuwa ni.pigo kubwa sana katika.maisha yangu. Swaumu aliniachia pengo kubwa sana ndani ya nafsi yangu. It was if a very big thing was just taken out of my heart by force.


However kwa sababu ya utoto na nini ilinichukua muda mfupi sana kisahau kuhusu Swaumu.


MWAKA 1995 : NAKUTANA NA HALIMA BINT HUSSEIN.

ITAENDELEA
 
Dah...
Hakunaga mapenzi matamu kama ya msingi aisee.

Huko hakunaga drama wala kuwaza kugegedana.
Ni full true love.

Bahatu nzuri huyo uliyemtaja yumo humu JF.
 
Back
Top Bottom