Halima Dendegu: Mkuu wa wilaya nne

Ahsante kwa kujibu mapema, nilikuwa najaribu ku-research kama kweli wilaya hii ipo, maana you never know wilaya na mikoa inavyoongezwa siku hizi. Sie tulishazoea ileee yetu 20 na visiwani 5. Lakini sasa sijui imefikia mingapi.

Kwa sasa ili kutafutiana ulaji mpaka kwa mashemeji na mahawara imefikia mikoa 27 bara na 10 Zanzibar, unaweza check maana yaweza kuwa imeongezeka mpaka taarifa hii inakwenda hewani.
 
Ukuu wa wilaya ni cheo ambacho hakina tija kwa wilaya. Ni upotevu wa resources kugharamia watu ambao hawajui hata job descriptions zao. Hali kadhalika ukuu wa mkoa, ndio maana mikoa na wilaya hizo zinaweza kukaa muda wote bila kuwa na mikoa. Hao kazi zao ni kuongoza kamati za siasa na ulinzi wenye lengo la kuipamba CCM ambayo haina jema la kutambia. Kwa hiyo usidhani kama anafanya kazi kubwa. Hao wakitembelea vijiji au kata watendaji wa huko lazima wahangaike kutafuta mbuzi, bia na vingine kuwakarimu na ujumbe wao, zote kutoka kwenye kodi za wananchi ili hali wanachukua posho ya safari hizo. Upuuzi mtupu...
 
sasa alipotufikisha atampa ukuu wa wilaya Mtoto wa Gadafii aliyekabidhiwa kabla ya kifo cha baba yake.
 
sasa alipotufikisha atampa ukuu wa wilaya Mtoto wa Gadafii aliyekabidhiwa kabla ya kifo cha baba yake.
 
hivi dc anatakiwa awe na qualification zipi? Na hizi nafasi hutangazwa wapi

wakuu wa wilaya na mikoa ni wateuliwa wa raisi hakuna kigezo chochote kinachotumika ili mradi ajue kusoma na kuandika tu.nafasi hazitangazwi raisi akijisikia tu anateua yeyote anayemuona yeye anamfaa,ni vyeo vya kisiasa zaidi vinavyolenga kuendeleza chama.nadhani katika mapendekezo ya katiba mpya hili ni jambo la kupendekeza kurekebishwa ili cheo hichi kiwe na tija kwa wilaya au mkoa husika
 
hebu jiridhishe kwanza na chanzo chako cha taarifa manake wilaya zote hizo zina ma DAS ambao kwa sheria ya tawala za mikoa ya mwaka 2007, na ya utumishi wa umma ya mwaka 2006 ndio wanaokaim ukuu wa wilaya.Mkoa wa morogoro unaongozwa na Joel Bendera ambaye kwa sheria hiyo inamtaka kutoa amri na kusimamia maDAS kukaim nafasi ya mkuu wa wilaya kama mhusika hayupo na kuna time limit ya miezi mitatu.mkuu wa wilaya ya mvomero namfahamu yupo na wa wilaya ya morogoro (urban and rural) pia yupo sasa usiandike uzushi wako apa ili kuruhisha nafsi yako.
 
Kazi ya mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa ni kupeperusha kile kitambaa kinachoitwa bendera kwenye magari yao na kutoa amri ambazo hazina kichwa wala mkia,kukata tepe na kumpokea raisi na familia yake
 
Back
Top Bottom