Halima Dendegu: Mkuu wa wilaya nne

njiwamanga

Member
Oct 21, 2010
35
3
Hivi unajua kama mwanamama huyo anatawala wilaya nne za Kilosa,Morogoro manispaa,Morogoro Vijijini na Mvomero?

Toka JK apangue wakuu wa wilaya mpaka sasa bado anayezitawala wilaya hizo ni huyo mwanamama.

Je, hakuna wengine wa kumsaidia? Kwanini iwe yeye tu?
 
hivi dc anatakiwa awe na qualification zipi? Na hizi nafasi hutangazwa wapi
 
Kwani kama angekuwa ni mwanaume anayeshikilia nafasi hizo, ingekuwa sawa?

tungehoji pia lakini kwa hili la mwanamke kushika wilya 4 ni maajabu ya tanzania pekee. jamaa yuko bize sana kumtafutia mwanawe dili
 
Hakuna wilaya inayoitwa morogoro vijijini.
Ahsante kwa kujibu mapema, nilikuwa najaribu ku-research kama kweli wilaya hii ipo, maana you never know wilaya na mikoa inavyoongezwa siku hizi. Sie tulishazoea ileee yetu 20 na visiwani 5. Lakini sasa sijui imefikia mingapi.
 
tungehoji pia lakini kwa hili la mwanamke kushika wilya 4 ni maajabu ya tanzania pekee. jamaa yuko bize sana kumtafutia mwanawe dili
Unazidi kunichanganya tu, mwanawe yupi tena huyo? Anayempa ukuu wa wilaya nne? Hebu naomba unifafanulie hapo kidogo. Mie nijuavyo 'jamaa' means Mkuu wa Kaya ana mtoto mmoja tu aliye active kwenye siasa zetu, wengine siwafahamu.
 
Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa mikoa hawana kazi yoyote wanayofanya zaidi ya kuongeza mzigo kwa walipa kodi.

Mtu mmoja anaweza kuwa mkuu wa wilaya au mikoa yote Tanzania na hakutakuwa na tatizo lolote kwa sababu kazi zinafanywa na Wakurugenzi wa halmashauri na maafisa tawala...
 
Hivi unajua kama mwanamama huyo anatawala wilaya nne za Kilosa,Morogoro manispaa,morogoro vijijini na Mvomero?Toka JKapangue wakuu wa wilaya mpaka sasa bado anayezitawala wilaya hizo ni huyo mwanamama.Je hakuna wengine wa kumsaidia?kwanini iwe yeye tu?

Hiyo inathibitisha kuwa hakuna umuhimu wa kuwa na wakuu wa wilaya na hata wale wa mikoa!
 
Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa mikoa hawana kazi yoyote wanayofanya zaidi ya kuongeza mzigo kwa walipa kodi.

Mtu mmoja anaweza kuwa mkuu wa wilaya au mikoa yote Tanzania na hakutakuwa na tatizo lolote kwa sababu kazi zinafanywa na Wakurugenzi wa halmashauri na maafisa tawala...

huwenda ukawa sahihi kwa eneo unalokaa ila kwa eneo nililolopo naona wanaomaliza pesa za kodi zetu ni wabunge wanaoongezewa posho kila kukicha,vijijini hawaonekani.....wakuu wa wilaya busy vijijini kuhimiza kilimo na elimu wakurugenzi busy semina na safari za kikazi
 
Mishahara minne, Posho nne kila kitu nne nne duuuh.
Wakati daily watu wako vijiweni na elimu zao hakuna ajira
 
kumbe hata hatuitaji wakuu wa wilaya wengi, mbona mambo yanaendelea chini ya mkuu wa wilaya mmoja; Mytake: kuna nafasi nyingi za serikali ambazo si budi zifikiriwe upya kwani ni upotezaji wa raslimali za wananchi!!!
 
Anatisha,anhudumia vipi mabwana 4 kwa muda 1?Kama wote wanahitaji huduma kwa wakati 1 itakuwaje?
 
kwanini amepewa wilaya zote hizo aziendeshe? Si angekuwa ni mkuu wa mkoa tu ijulikane moja if she is capable!
 
Back
Top Bottom