Hali za hospitali zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hali za hospitali zetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by measkron, Dec 12, 2011.

 1. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Hospitali ya mkoa Ruvuma wodi ya wajawazito uwezo wake ni vitanda 70, kuna kina mama zaidi ya 200 wanalala nje, ndani hapatoshi na mvua ikinyesha wananyeshewa, jiko dogo wanapika nje, wengi hutokea jimbo la Namtumbo kwani hakuna huduma ya dharura kwa wajawazito... Source TBC News saa 2. My take: vipaumbele ni vipi kama twaweza kuadhimisha miaka 50 ya uhuru kwa pesa nyingi huku tukishindwa kujali huduma muhimu? Viongozi wetu wana mawazo gani ili kuboresha huduma za kijamii?
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Kama nakumbuka vizuri kuna wakati Mwanakijiji alikuwa na effort ya kuongeza vitanda kwa wagonjwa. Sijui iliishaje. Sio lazima kila kitu kiachwe kwa serikali, especially kama serikali yenyewe hopeless.

  Tunafanya nini kusaidia wagonjwa kama Watanzania?
   
 3. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #3
  Dec 12, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wabunge wao hawana habari nao.Wanafikiria kujiongezea posho tu.Sijui nini msimamo wa mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa kuhusu posho wakati mama na dada zake wanajifungulia mavumbini kama panya!
   
 4. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu ninadhani hili hii sio kwa Namtumbo pekee, kule Simanjiro hawana hospitali ya wilaya kina mama wajawazito hulazimika kwenda Hospitali ya Mkoa Kilimanjaro, Mawenzi, kulingana na jiografia ya Simanjiro. Nina ndugu yangu anafanya kazi huko Mawenzi hospitali ananijuza chumba cha upasuaji kilifungwa tangu 27/12/2010, karibu mwaka sasa. Ingependeza kama wanahabari wengine wangeiga mfano wa Ruvuma na kuonyesha mikoa mingine hali ikoje. Serikali legelege, viongozi legelege, maamuzi legelege.
   
 5. The FaMa

  The FaMa Senior Member

  #5
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Tunalipa kodi kwa serikali ambayo nayo hupaswa ku-provide better services kwa wananchi! Je ndicho kinachofanyika? Kodi hatulipi? Kama tunalipa, hazitoshi? Kama zinatosha, zinatumikaje? Jibu= kujiongezea posho, sherehe za 64bn/-, safari za nje zisizokuwa na tija nk nk.
   
 6. R

  React Member

  #6
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hospitali ya Mkoa Iringa imesimamisha huduma za kawaida kwani serikali (hazina) haijapeleka fedha MSD za kutosha kwa miezi mitatu mfululizo. Hospitali ilikuwa inapokea kiasi cha mil 33 kwa mwezi kwa ajili ya madawa , lakini tangu Sept 2011 imepeleka mil 28 tu. Hospitali imeshindwa kujiendesha kama kawaida. Huduma ni kwa zile za dharura tu. (Emergencies)
   
 7. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #7
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,472
  Trophy Points: 280
  wabunge wasipolipwa posho for one day only ..vitanda vinanunuliwa na hospitali inaongezwa...nani wa kuwafunga kengele? ZITTO??
   
 8. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #8
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,315
  Likes Received: 19,472
  Trophy Points: 280
  kwani watu walikuwa wanatibiwa bure?
   
 9. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #9
  Dec 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Upinzani Mi naona ni nzuri sana! Ntarudi baadae kidogo! Maana naona hp mtaani kama kuna kelele ambazo siyo!
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,522
  Likes Received: 81,917
  Trophy Points: 280
  ....Dah!!! Halafu wanaenda kuunguza bilioni 64 kwa sherehe tu!!!! Na kisha kuja na kauli potofu kwamba tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele!!!!!
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Kumbe tunajua serikali yenyewe ni hopeless? Why do we keep voting it in? Mi nadhani sie wenyewe ndo tuna tatizo! Inafika wakati tuvune tulichopanda manake hatujifunzi kutokana na makosa. Hao wamama wanaojifungua nje kwenye mvua walimchagua rais wao,ndo anawatumikia hivyo!
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,522
  Likes Received: 81,917
  Trophy Points: 280

  ....Dr nakubaliana nawe lakini pia mimi nadhani katika uchaguzi uliopita hakushinda huyu ila walitumia vyombo vya dola kuchakachua uchaguzi kwa kiwango cha kutisha, kwenye uchaguzi wa Rais na Wabunge.
   
 13. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Jamani inabidi ifike kipindi tuanze kudeal na wabunge wetu hata kwa kuwapiga au hata kuharibu ili mradi wajue majukumu yao maana kila kitu tunalaumu serikali bila kuangalia ngazi ya serikali ya kuwajibisha.

   
Loading...