Hali ya utaifa inatisha

Ccm Mungu anawaona, yaani wananchi wamewakabidhi nchi vizuri kwa amani miaka yote toka uhuru, halafu nyie mmeenda kuikabidhi kwa shetani, Mungu anawaona.
 
Tuanze na ndani. sasa hivi CCM wanafanya mikutano kila mahali, jana tu nimeona mabasi ya wanaccm wamevalia sare zao pale Muhimbili, sijui walifuata nini, kutoa damu? lakini kwa nini hivi sasa. Lakini wenzao wa upinzani hawaruhusiwi kabisa kufanya mikutano japokuwa ndani ya miezi michache ijayo kutakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa. huu ni ubaguzi wa kiwango cha juu sana. hivi Magufuli amesahau kwamba asilimia 6 ya watanzania walipigia kura upinzani katika uchaguzi mkuu wa 2015? hao anawaweka wapi anapofanya hayo anayofanya?. ni kama vile kuna watoto wa mama wakambo na watoto wa kufikia. wa mama kambo wanapewa chakula kizuri, wa kufikia wanapewa ukoko. sasa akija mgeni, au wakipelekwa out, wote wanatazamiwa kushangilia na kutetea maslahi ya FAMILIA. Wakinuna utawalaumu kuanzia wapi?
 
Ubaguzi mnaanza wenyewe kwa kjiita wazalendo namba 1 eti wngine siyo wazalendo na mengine mengi mnayo yafanya kwaakili zenu mnaona mnapatia. keki ya Taifa mnagawana wenyewe na familia zenu na wale watu wasiojulikana je? ''people have tired faces because they are miserable you cant see them''
 
Mtu anashangilia ndugu yake wa damu anapopata matatizo leo unaongelea utaifa! Kila mtu anaukichaa wake kichwani.



MAGUFULI4LIFE
 
Tatizo ni kwamba, kisaikolojia, ukiombewa na viongozi wa dini, hata kwangu mtu nisiyeamini uwepo wa Mungu, kitendo cha mpinzani kuombewa na viongozi wa dini ni kitendo cha kuonesha kwamba mpinzani huyo.

1. Anakubalika na viongozi wa dini.
2. Anahurumiwa na viongozi wa dini.
3. Viongozi wa dini wanamtakia mema.

Sasa kuna watu wanataka wao tu ndio wakubalike, akikubalika mwingine nongwa.

Hapo itaona udhaifu unaoitwa "insecurity". Kimtaa tunasema mkubwa anajistukia na hana kujiamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…