Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Baada ya kutangazwa level seat kutokana na kuepuka maambukizi ya corona, ungetegemea crisis kutokea kwa upande wa usafiri wa umma.
Sijui kwa wengine ila jana nilifanya utafiti kidogo nimeona abiria wamepungua sana, lakini biashara ya daladala inaendelea kama kawaida. Hii imeniambia mambo mawili:
Kwanza, inaonyesha biashara ya daladala inalipa sana. Hapo kabla tulikuwa tunarundikwa kama ng’ombe. Yaani basi lilikuwa tayari limejaa lakini litabaki kituoni kusubiri abiria wengine. Wengi tulidhani hawa jamaa hawatengenezi hela ya kutosha tukawa tunawavumilia, kumbe hata level seat, biashara wanaweza kufanya!
Pili, inaonyesha Watanzania wengi huwa hawana shughuli maalumu za kufanya. Sitawaita ni wazururaji ila imekuwa ni kawaida kuanzia asubuhi hadi usiku kwa usafiri wa umma kujaza abiria ila sasa hivi bila hata lockdown abiria wamepungua sana. Hii ina maana kuna watu wengi ambao shughuli zao huwa siyo za msingi sana au hawana shughuli maalumu, ndiyo hao wamepungua kipindi hiki.
Niko tayari kusikia wenye mitazamo tofauti.