ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,543
Kwa hali niliyoshuhudia nilipopanda basi la Gerezani kuelekea Kimara ni ya kusikitisha sana, Kituoni Gerezani abiria waliosubiria gari kwa muda mrefu wamejazana pale miongoni mwao ni wa mama wenye watoto wadogo, wazee na wanafunzi, hatimaye linakuja basi kupakia ilihali ndani wamo abiria waliozunguka nalo!
Kwa vile watu wamechoka kusubiri kituoni wanaamua kuvamia hivyo hivyo basi linajaa kupita maelezo, basi linafika kituo cha msimbazi kundi lingine kubwa linavamia basi na mpaka milango kushindwa kufunga! Hii ni hatari sana, basi linafika kituo cha faya na vingine vifuatavyo kuna wanaolazimisha kuingia ndani wanashindwa na kuna wanaotaka kushuka wanashindwa! Watoto wadogo wanalia kwa kuminywa na tulisikia kuwa hivi karibuni kuna mama mwenye presha alianguka ktk kusukumana akakimbizwa muhimbili maana alianguka presha ikapanda.
Nachoshangaa Sumatra hawaoni shida hizi wao wakiwa wadhibiti na wasimamizi wa vyombo vya usafiri majini na nchi kama?
Au usafiri wa mwendo kasi hauwahusu? Tafadhali Sumatra hatua za haraka zitafutwe kuondoa usumbufu huu.