Elections 2010 Hali ya "ugonjwa wa Kikwete wa Ahadism" yazidi kuwa mbaya

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,093
1,726
Wana Jamvi
Ugonjwa unaomsumbua Rais Kikwete uitwao "AHADIsm" umeendelea kusambaa kwa kasi na hali yake sasa ni mbaya. Wasaidizi wake wanaofuatana naye katika safari za Kampeini wameniambia, hawawezi kutunza kumbukumbu za ahadi zake na idadi yake. Katika mikoa ya Kigoma, ameahidi yafuatayo:
-Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kigoma
-Hospitali ya Rufaa Kigoma
-Hospitali ya kutibu figo Kigoma
-Meli mpya ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa
-Daraja la mto Malagarasi
-Barabara ya lami kutoka Tabora hadi Kigoma
-Hospitali ya Wilaya Ujiji

Jamani mwenye dawa asaidie
-
 
Kikwete aliyoahidi 2005 ameyatekeleza kwa zaidi ya asilmia 80, ndiyo maana wananchi waliowengi wameridhika na hawamuulizi alioyoahidi 2005
======
Kwani anatoa nafasi ya kuulizwa maswali kwenye mikutano ya kampeini ili wamwulize juu ya ahadi za 2005?
 
Kikwete aliyoahidi 2005 ameyatekeleza kwa zaidi ya asilmia 80, ndiyo maana wananchi waliowengi wameridhika na hawamuulizi alioyoahidi 2005

Kati ya hayo 80% mengine siyo yale yaliyokuwa ya kumalizia ya awamu ya tatu? Yeye na serikali yake walitoa ahadi kama 2,000, 3,000 au 4,000 hivi, je zote hizi tayari? Tuwekee kumi tu pamoja na source!
 
WenyeNchi wnanasema 'takwimu hazidanganyi'; wanaaona ('vipofu') ie: wanaNCHI; wanasema 'mwenye njaa, mgonjwa, kijijini halishwi, kutibiwa, kusomeshwa, kuajiriwa au kuvishwa na takwimu'. Toka lini Ikulu ye yote duniani inaweka 'orientation period' ili baada ya uzoefu ofoisini (ambapo pia hukai saaaaaaana) ndipo utimize ma'promise' yako?
 
Baija Bolobi, nadhani is too early to start judging now we could be fare to judge this after 5 years if elected. Tutoe hoja zinazo onyesha tuko matured.

Wana Jamvi
Ugonjwa unaomsumbua Rais Kikwete uitwao "AHADIsm" umeendelea kusambaa kwa kasi na hali yake sasa ni mbaya. Wasaidizi wake wanaofuatana naye katika safari za Kampeini wameniambia, hawawezi kutunza kumbukumbu za ahadi zake na idadi yake. Katika mikoa ya Kigoma, ameahidi yafuatayo:
-Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kigoma
-Hospitali ya Rufaa Kigoma
-Hospitali ya kutibu figo Kigoma
-Meli mpya ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa
-Daraja la mto Malagarasi
-Barabara ya lami kutoka Tabora hadi Kigoma
-Hospitali ya Wilaya Ujiji

Jamani mwenye dawa asaidie
-
 
tatizo si kikwete asilani... anajua watanzania wengi ni masikini sana na ni mambumbumbu wa taarifa, with very short memory

Yeye anachofanya ni kutumia utaratibu tuliojiwekea watanzania... kuahidi bila kutekeleza...
ukienda kwa fundi cherehani, atakupa tarehe isiyotekelezeka
ukimpa fundi mwashi kazi tegemea hichohicho
Ukimpa makenika gari, atakuahidi makubwa
ukiwa unaondoka nyuimbani, utaahidi watoto wako hadi ndege [as if you have money to buy even a cr]
ukiwa kwenye bar, utaahidi kila mtu mambo usiweza hata kukumbuka nk.

It is our disease na si JK pekee

But the time is now for change... charity begins at home
 
Mkuu nimechoka na ahadi za Kigoma. Daraja mto malagarasi... International Airport for what?

Mbayuwayu anabwabwaja tu as if serikali yake ina hela...lol!!

2010, hatudanganyiki.
 
Kikwete aliyoahidi 2005 ameyatekeleza kwa zaidi ya asilmia 80, ndiyo maana wananchi waliowengi wameridhika na hawamuulizi alioyoahidi 2005

Ahadi mama aliyotoa 2005 ni maisha bora kwa wote. Hiyo imetekelezwa kwa asilimia 80?

Hali ya umeme, maji, elimu, uwezo wa kununua mahitaji, ni mbaya zaidi ya ilivyokuwa 2005.
 
Baija Bolobi, nadhani is too early to start judging now we could be fare to judge this after 5 years if elected. Tutoe hoja zinazo onyesha tuko matured.

Kwanini tusi-hukumu sasa ya kile tunachoahidiwa miaka 5 ijayo tukiweka msingi wautekelezaji wa kile tulichoahidiwa miaka 5 iliyopita?

Maturity ni pamoja na kufikiri sahihi na kuchukua hatua katika maamuzi yako. Ukiujua kuwa huu ni oungo; ukomavu ni pamoja na kukataa kudanganywa.
 
Huyu ni rais ahadi na ndio sera kuu ya CCM,hela hwana ila ahadi mpaka zinakera. Mwaka 2000 waliahidi MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, 2005 KASI MPYA, ARI MPYA NA NGUVU MPYA na 2010 KASI ZAIDI, ARI ZAIDI NA NGUVU ZAIDI.Hizi ni ahadi zisizo tekelezeka kwani huwezi huwezi kuwa na vipaumbele 20 kwa mwaka wakait huna hela ya kutekeleza, lazima vipaumbele viwe vichache ambayo vinatekelezeka, hizo ni ahadi za mikoa kama mi4 tu, Je? JK akimaliza mikoa yote TZ atakuwa ameahidi mangapi? Huu ni usanii live, wananchi waliomambumbu watamshangilia na kufarahia ial kwa waelevu wanajua hakuna kitu hapo zaidi ya upopopo.2010 HATUDANGANYIKIIIIIIIIIIIIIIIIIIIII.
 
Kikwete aliyoahidi 2005 ameyatekeleza kwa zaidi ya asilmia 80, ndiyo maana wananchi waliowengi wameridhika na hawamuulizi alioyoahidi 2005

Taja hata tano alizoahidi ambazo leo zimekamilika. Usieleze miradi aliyoanzisha mkapa kama barabara ya kibiti -lindi au dodoma -mwanza kupitia singida, national stadium
 
Taja hata tano alizoahidi ambazo leo zimekamilika. Usieleze miradi aliyoanzisha mkapa kama barabara ya kibiti -lindi au dodoma -mwanza kupitia singida, national stadium

Kwani Mkapa ni CHADEMA?? Kikwete/Mkapa au yoyote wanaongozwa na Ilani ya CCM, so usiseme ahadi za Kikwete bali ni ahadi za CCM. Hizo ndoto zenu na huyo jamaa yenu aliyefukuzwa kanisani zitayayuka baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa
 
Mkuu naona wewe unafuata "chama kwanza, halafu mtu". Hakuna chama chenye sera mbaya siku zote, na kwa kila mtu....! Hakuna chama kitakachoahidi mabaya au machungu. Kila chama huahidi mazuri na matamu kwa wananchi...! La msingi ni utekelezaji wa ahadi hizo...! Tunapaswa kufikiria nani mtekelezaji wa ahadi zake?
 
Back
Top Bottom