NGULI
JF-Expert Member
- Mar 31, 2008
- 4,805
- 630
Wakuu nimesikitika sana na mpasuko wa KISIASA ulioko nchini hivi sasa nilidhani wanayozungumza watu ni ushabiki ila leo yamenikuta, gari niliyokuja nayo kazini kwenye kioo kikubwa, kwenye kioo cha kutazama nyuma kuna benendera ya CCM. Nilivyokuja kupaki walinizuia wale vijana pamoja na waalinzi nikawasalimia wakakataa na kuambulia matusi kuwa mimi ni kijana naoneka mstaarabu kumbe mwizi na tena fisadi papa nilicheka nikizani labda ni mzaha, ndio wakaanza ya nguoni.
Kwa hasira nikapiga simu kwa manager anayehusika na parking na kwa haraka akafika alishuhudia matusi ya waosha magari wale pamoja na mlinzi pembeni na hata anisaaidii karibu nipigwe na mawe kwa hasira. Akawahoji wakasema kama nataka kupaki na gari waioshe basi nitoe bendera ya CCM haraka kwani maisha yamekuwa magumu na kuweka bendera ina maanisha mimi nachangia kwani nai support kuwepo madarakani. Cha kushangaza manager nae akawa support ndio nikaishiwa nguvu ikabidi niitoe bendera/kitambaa cha CCM ndio nika park gari.
Nime report kwenye uongozi wa ofisi nao wamenigeuka wakaniambia nisiwaletee ushabiki wa kisiasa na nikiendelea kujihusisha na siasa nitafukuzwa kazi. Imebidi niombe msamaha yasifike mbali lakini hata hivyo gari sio yangu niliazima yangu ni lizee halikosi siku 2 bila kwenda garage.
Wito wangu elimu ya mpasuko wa kisiasa itolewe ipasavyo si ajabu magari ya watu yakaanza kuchomwa na baadae kuhamia kwenye nyumba za watu.